Yqpo mambo mawili yatakayo kufanya usisahaulike duniani,mema uliyoyafanya yatazungumzwa kama sehemu ya urithi ulioacha ambao jamii inapaswa kuiga toka kwako (legacy). Jambo la pili ubaya ulioutengeneza utazungumzwa kama tahadhali kwa mabaya yasiyo ipendeza jamii,Magu ana sura mbili unyenyekevu na ukatili lakini ukatili umevuma sana kuliko unyenyekevu kwa msingi huu,alitumia nguvu kubwa kudhibiti sauti ya watu walio nyikani,akiyatumia mamlaka kimabavu,na unyenyekevu ulitumika kama silaha kuficha ubaya uliokithiri. Kwa mantiki hiyo utaona sura zote mbili zilimtengeneza katika umbile gani.