Hayati Magufuli hayuko duniani lakini ana watetezi wengi kuliko wenye fedha walio hai

Huna uhakika na unachoandika. Umeishi kwa story sana zingine za vijiweni tu na wanasiasa. JPM hawezi kuwa muuwaji. Kafa lakini hadi leo watu wanakufa. Zingine ni siasa tu.
Kuna watu ni Wajongs kuliko ujinga wenyewe, wanakufa watu kwa risasi kila siku USA, nenda hapo Kongo, nenda Ukraine, Somalia, taifa lao teule Israel, Iran, na sehemu zote za dunia, juzi Arusha baba kaua binti yake miaka chini ya kumi na nane kwa kipigo, watu wapo na Magufuli tu. Kifo kipo nje nje style tu ndio tofauti, hakijaanza jana na hakitaisha kesho… “nigger watch your back & watch your front”….Tupac.
 
Magufuli (R. I. P), pamoja na makandokando yake utendaji wake huyu bibi PhD hajaweza kuufikia hata robo. Kutwa yeye ni kulalamika tu na kusafiri ndio anachojua. Hana creativity yoyote, in short nchi imeshamshinda. Sasa kama kiongozi mkuu anakuwa wa kulalamika, hao wakuu wa wilaya itakuwaje?. Eti nendeni mkalitizame 😀😀😀😀, nchi hii kwa viongozi wa aina hii kufanikiwa ni ndoto.
 
Mkuu acha kujifariji
 
Ali
takiwa kuwa waziri wa sanaa na michezo awe anakata keki na kina Lady Jay Dee na Marioo kama yule mkerekweche… Binafsi naona IQ ya Joketi ni twenty times better than hers…
 
Kiongozi muovu ndio yukoje au kwa Tanzania kiongozi muovu ni wa awamu ya tano tu ila hao wengine wote chini ya ccm ni viongozi safi?

Kila mtu ana kipimo chake, kwangu mimi alikuwa kiongozi muovu. Kama ni mzuri hiyo ni kwako
 
Iddi amini anatetewa mpaka leo.
 
Jambo zuri ni kwamba Kila anayejaribu kumchafua, anachafuka yeye maradufu. Magufuli ni Oil Chafu
 
SAWA
 
Yeye mbona aliita wengine mafisadi na hawakuwa mafisadi?. Apandacho mtu ndicho atakacho vuna.
Daah!

Unaona sasa mkuu moyoni mwako ulivyotayari kusema lolote juu yake bila hata ushahidi! Kuna faida inapatikana mpango huu usio na ushahidi?
 
Siasa za JPM kulihusu Taifa! Zilikuwa na manufaa makubwa kwa kila mtanzania ukiacha hao ambao walikuwa wamewageuza Watanzania kuwa ngazi ya kupandia!

Wanajua kuwa! Wasipofanya kila ubaya kumhusu huyu marehemu! Hatima yao kisiasa na wizi wanaoufanya itakuwa mbaya zaidi mbeleni

Ili wakubaliwe, wako tayari kupandia kila ovu ili tu umma umchukie huyu mwendazake! Hata hivyo, zote ni porojo tu kwa sababu kila ubaya wanaousema, hawawezi kuutolea ushahidi na hata wakiutoa, bado ni zilezile porojo za wao kutafuta kubaliwa na wananchi

Yaani mtu unasema account iko China pasina mtu huyo huwekwa chini ya ulinzi na kukamatwa?

JPM hayupo 2years Yuko kabrini! Faili zote kaziacha bila kujiandaa itakuwaje kumhusu! Eti bado wanasema alikuwa mwizi?

Ushahidi uko wapi? Bunge linafanya nini kubaini huo ufisadi kama ilivyokuwa kwenye utawala wa nne?

Waweke mambo hadharani tu
 

Hawa ndio baadhi ya wana CCM wakipata raisi mpole.

Jitu alioni ata aibu kutetea mradi wa ovyo yaani linatumia nguvu kweli serikali kuingia mkataba wa kijinga.

Anadhani watanzania wote mapoyoyo kama wale wanaomchangia upatu jumapili. Mwingine Zitto alikuwa anaupigania sana huo mradi wa Liganga na Mchuchuma.

Enzi za mwamba hakuna kada mwenye jeuri ya kutetea upuuzi wa namna hiyo R.I.P Magufuli.
 
Ni kutokana na kifo chake kuacha utata si kama Mkapa na Mwalimu. Lakini pia wanaomsujudia marehemu wamelaaniwa.
 
Hilo la kusema Magu ukatili ndio sifa yake iliyovuma sana mie nakataa, hata sasa ukiangalia wanaoeleza mabaya ya Magu utaona hutumia mafumbo sana huogopa kueleza wazi kwa sababu wanajua watu wengi huko mtaani hawamzungumzii sana Magu kwa mabaya, kwahiyo utaona ni kama inatumika jitahada kuwaonyesha watu kuwa Magu hakuwa hivyo mnavyomdhania hasa humu mitandaoni ndio watu hutumia nguvu kueleza hayo mabaya ili ijulikane kwamba Magu hakuwa mtu mzuri.
 
Kila mtu ana kipimo chake, kwangu mimi alikuwa kiongozi muovu. Kama ni mzuri hiyo ni kwako
Ndio maana nikakuuliza kiongozi muovu yukoje? Jiamini eleza sio unakosa kujiamini na kuanza kusema kila mtu ana kipimo chake, we eleza kiongozi muovu huwa yupo hivi na vile.
 
Hata JK Nyerere alitukanwa Sana mwanzoni alipoacha madaraka na baada ya kufariki.....lakini baadaye waliomba pooo na hata kumwita Baba wa Taifa...
Historia ndivyo ilivyo.....Mimi Nina hakika itakuja kujengwa minara ya Magufuli...I am sure of that...mark my words...hifadhi comment hii...kwa wale wanaofuatilia kinachoendelea mitaani na huko vijijini watakubaliana nami....Ogopa Sana public.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…