Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

View attachment 3225842

Hatimaye!
Baada ya sarakasi nyingi, Msanii Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekata shauri la kumuoa mpenzi wake ambaye ni msanii ndani ya lebo yake ya muziki (WCB) Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’

Uamuzi huo umekuja huku kukiwa na sintofahamu nyingi juu ya mahusiano yao ambapo mwishoni mwa mwaka jana Zuchu alitangaza kwa mara nyingine kuachana kwao japo amekuwa akifanya hivyo mara nyingi na baadaye kurudiana.

Safari hii mambo yamekuwa tofauti kidogo baada ya majuzi kuibuka ugomvi ndani ya kampuni upande wa redio kwa Zuchu kuwashutumu wafanyakazi wa Diamond kumvunjia heshima.

Zuchu ameonekana ‘kukaza’, hajacheka na yeyote akiwemo Diamond mwenyewe na pengine hili limesogeza karibu ndoa yao.

Zuchu ameshinda vita iliyowashinda wengi?…
The mother in law from hell, Mama Diamond amekuwa mwiba mchungu takribani kwa kila mwanamke aliyetoka kimapenzi na Diamond.

Amesemekana kikwazo kikuu kwa Diamond kuoa, hivyo posa hii kwa Zuchu inatuacha njia panda kwamba Mama Dangote kapata kiboko yake? Je posa hii ina baraka za mama yake Diamond?

Ndoa ni kabla ya Ramadhani…
Mwezi uliopita Diamond akiwa na msanii mwenzie Nandy katika mkutano mkuu wa CCM, alionekana akisema atamuoa Zuchu kabla ya Ramadhani ya mwaka huu ambayo inategemewa kuanza mapema mwezi Machi.

Diamond amekuwa akitoa ahadi nyingi hivyo wengi hatukuchukulia tamko lile kwa uzito, nimeshtuka baada ya kupewa taarifa za uhakika kuwa ni kweli na posa hiyo itapelekwa nyumbani kwa Bi Khadija Kopa Ijumaa ya kesho kutwa tarehe 7.

Haya jamani, mambo ndio yako hivyo na hii ni habari endelevu nitakuwa hapa kuwajuza mapema kadiri nitakavyopokea taarifa.

Straight From The Horse’s Mouth,

Nifah.
Dada wa za ndaaaaanii
 
Zuchu mahari katolewa saa ngapi, jana Daimond kashinda kwenye harusi ya Jux
Posa ni barua ya uchumba baby, na sio kwamba ni siku nzima unaweza kutumia hata nusu saa tu.

Tulieni jamani, nimeshasema nitawapa updates hata kama imeshindikana nitawaambia tu.
cocochanel
 
Nipo hapa nasubiri mrejesho...... 😄 🤣 😂 😆 😄 🤣 😂 Zuu sijui alimkosea nini Mungu
 
Sasa na wewe uposwe uache kutujazia server kwa habari za kipuuzi. Sema tu mimi nimeshaposa lidada la kibantu.
 
Posa ni barua ya uchumba baby, na sio kwamba ni siku nzima unaweza kutumia hata nusu saa tu.

Tulieni jamani, nimeshasema nitawapa updates hata kama imeshindikana nitawaambia tu.
cocochanel
Uko sahihi posa wanaweza kuja hata mtu mmoja kupeleka posa. Hata maji asinywe akaondoka.
 
Kuwe na utaratibu wa kuomba radhi iwapo taarifa tulizoleta si sahihi.
Kwani umetozwa hela hadi uombwe radhi?

Jamani nikileta habari simlazimishi mtu kuamini, uamuzi huo ni juu yako.
 
Umbeya una matokeo mawili Uongo au ukweli. Haina haja ya kuomba radhi wakati unajua matokeo yake -ve au +ve.
Hakuna uongo katika habari niliyowaletea, chanzo changu ni mojawapo ya waliokuwa waende na Diamond kutoa posa.

Kuna mengi yametokea, nyie subirini tu nitawajuza.
 
Hakuna uongo katika habari niliyowaletea, chanzo changu ni mojawapo ya waliokuwa waende na Diamond kutoa posa.

Kuna mengi yametokea, nyie subirini tu nitawajuza.
Tulimjibu huyo anayetaka kuombwa radhi. Mi najua taratibu za ndoa za kiislam vizuri sana.
 
Kwani umetozwa hela hadi uombwe radhi?

Jamani nikileta habari simlazimishi mtu kuamini, uamuzi huo ni juu yako.
Hapa sio chumbani binti...

Ukileta tarifa kwenye jukwaa la wazi kama hili ni lazima ijadiliwe na ipimwe...

Ikijaa kwenye vipimo vya ukweli, wasomaji tunatoa credit na credibility ya mtoa habari inapanda...

Ukileta tarifa ya uongo ni busara kuomba radhi japo sio lazima, lakini ukiomba radhi utapewa credit na credibility yako itabaki juu.
 
Back
Top Bottom