He! Kumbe Quran nayo ilipangwa vitabu, Machapisho na Ayyah zake na binadamu kama ilivyo kwa Biblia

Kwanza kabisa Qur'an ni Kitabu kimoja , unaposema vitabu vya Qur'an ni makosa ya wazi kabisa labda useme aya za Qu'ran.

Mwisho kabisa hakuna ubaya juu ya kukusanywa kile kilichomo na kukipangilia vizuri ilimradi hakuna kilichotolewa Wala kubadilishwa sawa na kuweka Jalada katika Kitabu kama njia ya kuhakikisha usalama na kupendezesha hilo halibadilishi Contents
Nilishawahi kusikia kwamba Quran ilipokusanywa mara ya kwanza ilikuwa kitabu kikubwa kama nyumba then maswahaba wakapunguza baadhi ya vitu ndo ikawa kitabu kidogo.
Je,ni kweli?
 
Koran 5:3 .......Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu,.....

Surah ya tano kakamilisha Uislamu na Kuna surah zaidi ya 100 mbele ?

Ni ujinga wa Allah au ni waislamu wamebadili ?
Zile sura inasemekana hazijapangwa kuwa eti sura ya kwanza kwenye msahafu ndiyo ya kwanza kwa hiyo inawezekana hiyo aya ni ya mwisho lakini ikawekwa katika sura ya tano
 
Shalom, Salam alaikum.

Baada ya kusoma Biblia kuanzia Genesis Hadi Revelation nikaamua kuanza kusoma pia Quran (Mwaka huu).

Ila Huwa napenda kufahamu chanzo, uandishi Hadi uwasilishaji wa kitabu kabla ya kuanza kukisoma kitabu hicho (Napima uzito).

Na Hiki ndicho nilichogundua kwa upande wa chanzo cha Quran.

Vitabu vya Quran vilivyokuwa vimeandikwa kabla ya kifo cha Mtume Muhammad vilikusanywa na kuunganishwa kuwa kitabu kimoja baada ya kifo chake. Mchakato huu ulifanywa hasa na makhalifa wawili wa mwanzo, Abu Bakr na Uthman ibn Affan. Hapa kuna muhtasari wa hatua muhimu katika uunganishaji wa Quran:

1. Wakati wa Uhai wa Mtume Muhammad: Wakati Mtume Muhammad alikuwa hai, wahyi wa Quran ulipokelewa na kuandikwa na wafuasi wake kwenye nyenzo mbalimbali kama vile ngozi, mifupa, na majani. Wengi walikuwa pia wameuhifadhi katika akili zao.

2. Mchakato wa Abu Bakr: Baada ya kifo cha Mtume Muhammad mwaka 632 CE, baadhi ya wafuasi ambao walikuwa wamehifadhi Quran kwa kuikumbuka waliuawa katika mapigano. Khalifa wa kwanza, Abu Bakr, alihofia kwamba wahyi huo ungepotea, hivyo akaamuru uandikaji wa Quran kuwa kitabu kimoja. Zayd ibn Thabit, mmoja wa wahitimu wa Mtume, aliteuliwa kukusanya na kuandika vipande vya Quran kutoka kwa vyanzo mbalimbali.

3. Uthman na Usawazishaji: Baadaye, chini ya utawala wa Khalifa Uthman ibn Affan (644-656 CE), aliona kwamba katika maeneo mbalimbali kulikuwa na tofauti za usomaji na maandiko. Ili kuleta usawa, Uthman aliamuru kutengenezwa nakala rasmi ya Quran na kupeleka nakala hizo katika maeneo tofauti. Nakala nyingine zilisitishwa ili kuepuka tofauti.

Mchakato huu wa uunganishaji na usawazishaji ulihakikisha kwamba Quran iliifadhiwa katika fomu moja na inayoaminika hadi leo, kulingana na imani ya Kiislamu.
Tofauti kubwa iliyopo kati ya Qur'an na Biblia ni kuwa Quran imehifadhiwa kwa njia za wahyi yaani muongozo kutoka Kwa Allah aliyeiteremsha.
Kabla ya kufa kwa Mtume Saw malaika Jibril alikuwa anashuka na kumsikiliza mtume anavyoisoma kwa usahihi na mpangilio wake maka akaridhika kuwa hakukuwa na tofauti.
Kazi hiyo ilifanywa mbele ya makhalifa hao uliowataja na ambao nao waliihifadhi pamoja na wenzao.Kazi waliyoifanya kuikushanya pamoja pia nayo ilikuwa ni ya kiwahyi ndio maana waliifanya na kujiridhisha kabla ya kufariki kwao wakiwa wameacha nakala ambazo ndizo hizi tulizonazo leo.
Kwa upande wa biblia utamalizia mwenyewe kwa kuwaangalia waliotia mikono yao wenyewe tu bila kizuizi.
 
Kwanza kabisa Qur'an ni Kitabu kimoja , unaposema vitabu vya Qur'an ni makosa ya wazi kabisa labda useme aya za Qu'ran.

Mwisho kabisa hakuna ubaya juu ya kukusanywa kile kilichomo na kukipangilia vizuri ilimradi hakuna kilichotolewa Wala kubadilishwa sawa na kuweka Jalada katika Kitabu kama njia ya kuhakikisha usalama na kupendezesha hilo halibadilishi Contents
Rudia kusoma.

Uthman na Usawazishaji: Baadaye, chini ya utawala wa Khalifa Uthman ibn Affan (644-656 CE), aliona kwamba katika maeneo mbalimbali kulikuwa na tofauti za usomaji na maandiko. Ili kuleta usawa, Uthman aliamuru kutengenezwa nakala rasmi ya Quran na kupeleka nakala hizo katika maeneo tofauti. Nakala nyingine zilisitishwa ili kuepuka tofauti.
 
Kichwa cha habari hakiendani na ulicho andika, Quran haijawahi kua edited rather published, kipi unachotaka kumaanisha.?
Kuyapanga maandiko katika vitabu, surat na aya ndio kuedit kwenyewe huko sheikh
 
Shalom, Salam alaikum.

Baada ya kusoma Biblia kuanzia Genesis Hadi Revelation nikaamua kuanza kusoma pia Quran (Mwaka huu).

Ila Huwa napenda kufahamu chanzo, uandishi Hadi uwasilishaji wa kitabu kabla ya kuanza kukisoma kitabu hicho (Napima uzito).

Na Hiki ndicho nilichogundua kwa upande wa chanzo cha Quran.

Vitabu vya Quran vilivyokuwa vimeandikwa kabla ya kifo cha Mtume Muhammad vilikusanywa na kuunganishwa kuwa kitabu kimoja baada ya kifo chake. Mchakato huu ulifanywa hasa na makhalifa wawili wa mwanzo, Abu Bakr na Uthman ibn Affan. Hapa kuna muhtasari wa hatua muhimu katika uunganishaji wa Quran:

1. Wakati wa Uhai wa Mtume Muhammad: Wakati Mtume Muhammad alikuwa hai, wahyi wa Quran ulipokelewa na kuandikwa na wafuasi wake kwenye nyenzo mbalimbali kama vile ngozi, mifupa, na majani. Wengi walikuwa pia wameuhifadhi katika akili zao.

2. Mchakato wa Abu Bakr: Baada ya kifo cha Mtume Muhammad mwaka 632 CE, baadhi ya wafuasi ambao walikuwa wamehifadhi Quran kwa kuikumbuka waliuawa katika mapigano. Khalifa wa kwanza, Abu Bakr, alihofia kwamba wahyi huo ungepotea, hivyo akaamuru uandikaji wa Quran kuwa kitabu kimoja. Zayd ibn Thabit, mmoja wa wahitimu wa Mtume, aliteuliwa kukusanya na kuandika vipande vya Quran kutoka kwa vyanzo mbalimbali.

3. Uthman na Usawazishaji: Baadaye, chini ya utawala wa Khalifa Uthman ibn Affan (644-656 CE), aliona kwamba katika maeneo mbalimbali kulikuwa na tofauti za usomaji na maandiko. Ili kuleta usawa, Uthman aliamuru kutengenezwa nakala rasmi ya Quran na kupeleka nakala hizo katika maeneo tofauti. Nakala nyingine zilisitishwa ili kuepuka tofauti.

Mchakato huu wa uunganishaji na usawazishaji ulihakikisha kwamba Quran iliifadhiwa katika fomu moja na inayoaminika hadi leo, kulingana na imani ya Kiislamu.
Iliandikwa tena au iliteremshwa?
 
Tofauti kubwa iliyopo kati ya Qur'an na Biblia ni kuwa Quran imehifadhiwa kwa njia za wahyi yaani muongozo kutoka Kwa Allah aliyeiteremsha.
Kabla ya kufa kwa Mtume Saw malaika Jibril alikuwa anashuka na kumsikiliza mtume anavyoisoma kwa usahihi na mpangilio wake maka akaridhika kuwa hakukuwa na tofauti.
Kazi hiyo ilifanywa mbele ya makhalifa hao uliowataja na ambao nao waliihifadhi pamoja na wenzao.Kazi waliyoifanya kuikushanya pamoja pia nayo ilikuwa ni ya kiwahyi ndio maana waliifanya na kujiridhisha kabla ya kufariki kwao wakiwa wameacha nakala ambazo ndizo hizi tulizonazo leo.
Kwa upande wa biblia utamalizia mwenyewe kwa kuwaangalia waliotia mikono yao wenyewe tu bila kizuizi.
Rudia kusoma.

Quran ilihifadhiwa kwenye magome ya miti, mifupa na kumbukumbu za watu (Kichwani).

Baada ya maneno ya Muhammad (saw) kutoka mdomoni mwake (akilini) kwamba yameshushwa na Allah.
 
Iliandikwa tena au iliteremshwa?
Hakuna kuteremshwa shekhe ushahidi unasema iliandikwa na baadae ku-edit-wa na Uthman,

mwisho kabisa Yale Machapisho waliyoona Yana maswali mengi yalichomwa moto.🤔🤔🤔
 
Rudia kusoma.

Uthman na Usawazishaji: Baadaye, chini ya utawala wa Khalifa Uthman ibn Affan (644-656 CE), aliona kwamba katika maeneo mbalimbali kulikuwa na tofauti za usomaji na maandiko. Ili kuleta usawa, Uthman aliamuru kutengenezwa nakala rasmi ya Quran na kupeleka nakala hizo katika maeneo tofauti. Nakala nyingine zilisitishwa ili kuepuka tofauti.
Ndio sijapinga kwani Qur'an ilishuka katika Lahaja mbalimbali za kiarabu kipindi hiko ili kurahisisha usomaji , ilichofaywa ni kisawazisha yaani kuwekwa katika Lahaja Moja ambayo ndio standard na nyinginezo kuchomwa moto ili kuondoa tofauti katika usomaji. Na hiyo Lahaja iliyowekwa ambayo standard hakuzua yeye ilikuwa ni miongoni mwa Lahaja amabazo zilikuja katika Qu'ran kwa hiyo hapo hakuna ubaya wala makosa .

Watu wa maeneo tofauti wakapewa Amri kuwa wasome Qur'an wote katika Lahaja Moja na sio nyingine au kila mtu ajitungie ya kwake , hata bongo lafudhi za kiswahili lakini hayo yanaishia katika mazungumzo yenu ya kawaida na Kiswahili Cha kufundishia darasani ni kimoja Standard kilichonyooka .

Hata kiswahili Mkenya Moja anaita "Moya" na Mtanzania anaita Moja hivyo kimaana inakuwa sawa hakuna tofauti
 
Nilishawahi kusikia kwamba Quran ilipokusanywa mara ya kwanza ilikuwa kitabu kikubwa kama nyumba then maswahaba wakapunguza baadhi ya vitu ndo ikawa kitabu kidogo.
Je,ni kweli?
Chai , Maswahaba (Allaah awaridhie ) hawawezi kufanya kitu kama hiko kama Kuna ushahidi uletwe .

Na kipindi hiko walikuwepo wengi walikuwa wamehifadhi na kuijua sasa watu wangebadilisha lazima kungetokea mzozo na utata.
 
Kuyapanga maandiko katika vitabu, surat na aya ndio kuedit kwenyewe huko sheikh
Mbona hakuonyesha sura ipi alipanga Othman (RA)huwezi kupanga kitu ambacho kilishapangwa huyu anakosa maarifa sahihi kuhusu hilo suala.
 
Koran 5:3 .......Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu,.....

Surah ya tano kakamilisha Uislamu na Kuna surah zaidi ya 100 mbele ?

Ni ujinga wa Allah au ni waislamu wamebadili ?
Mpangilio wa sura na Aya katika Qu'ran (Msahafu) haujapangwa katika order ya jinsi zilivyoshuka na hakuna ulazima wa kuwa hivyo na Wala hakuna ubaya wa kuwa hivyo.
 
Ndio sijapinga kwani Qur'an ilishuka katika Lahaja mbalimbali za kiarabu kipindi hiko ili kurahisisha usomaji , ilichofaywa ni kisawazisha yaani kuwekwa katika Lahaja Moja ambayo ndio standard na nyinginezo kuchomwa moto ili kuondoa tofauti katika usomaji. Na hiyo Lahaja iliyowekwa ambayo standard hakuzua yeye ilikuwa ni miongoni mwa Lahaja amabazo zilikuja katika Qu'ran kwa hiyo hapo hakuna ubaya wala makosa .

Watu wa maeneo tofauti wakapewa Amri kuwa wasome Qur'an wote katika Lahaja Moja na sio nyingine au kila mtu ajitungie ya kwake , hata bongo lafudhi za kiswahili lakini hayo yanaishia katika mazungumzo yenu ya kawaida na Kiswahili Cha kufundishia darasani ni kimoja Standard kilichonyooka .

Hata kiswahili Mkenya Moja anaita "Moya" na Mtanzania anaita Moja hivyo kimaana inakuwa sawa hakuna tofauti
Kwamba Quran iliposhushwa ilikuwa na lahaja mbali mbali ila akatokea raia mmoja mwenye nguvu kuliko Allah (mleta lahaja mbalimbali) na Muhammad (saw) msimuliaji akaamua itengenezwe Quran yenye lugha na lahaja Moja.?🤔🤔🤔
 
Chai , Maswahaba (Allaah awaridhie ) hawawezi kufanya kitu kama hiko kama Kuna ushahidi uletwe .

Na kipindi hiko walikuwepo wengi walikuwa wamehifadhi na kuijua sasa watu wangebadilisha lazima kungetokea mzozo na utata.
Na zilivyopangiliwa sura kwenye Quran na Allah naye alizipanga hivyo?
 
Mpangilio wa sura na Aya katika Qu'ran (Msahafu) haujapangwa katika order ya jinsi zilivyoshuka na hakuna ulazima wa kuwa hivyo na Wala hakuna ubaya wa kuwa hivyo.
Yaani Allah apangilie vingine halafu atokee binadamu apangue halafu aseme "hakuna ulazima wa kuwa hivyo na Wala hakuna ubaya"

Ila Quran inapotaka kutafsiriwa kwa kiswahili na lugha zingine eti mnasema "kunaubaya sana" 🤔🤔🤔
 
Kwa mujibu wa imani ya Kiislamu ya jadi, hakuna Aya wala Surah tukufu zilizoondolewa kwenye Qur’an wakati wa usawazishaji wa Khalifa Uthman. Kilichofanywa na Uthman hakikuwa kuondoa sehemu za Qur’an, bali ilikuwa ni kuondoa tofauti katika namna ya kusoma na kuandika, ili kuhakikisha umoja wa Waislamu.

Hapa ni ufafanuzi wa kile kilichofanywa:
Kilichofanywa na Khalifa Uthman:

1. Usawazishaji wa lahaja (qira’at):
Qur’an ilikuwa inasomwa kwa lahaja tofauti tofauti (sababu ya kuruhusiwa kwa "Ahruf Saba’a" – njia saba za kisomaji zilizoruhusiwa na Mtume Muhammad). Uthman alichagua lahaja ya Kikuraishi (lahaja ya Mtume) kama ya msingi, na kuandika Qur’an kulingana na hiyo.
Umemaliza

Uzi ufungwe
 
Mpangilio wa sura na Aya katika Qu'ran (Msahafu) haujapangwa katika order ya jinsi zilivyoshuka na hakuna ulazima wa kuwa hivyo na Wala hakuna ubaya wa kuwa hivyo.
Kwa hiyo nani aliwapa mamlaka waislamu wabadili mpangilio wa Allah

Na walivyobadili waliona waweke surah ya 5 uislamu ukamilike kwa nini?
 
Koran imepangwa tofauti na Muhammad alivyoipanga

Mfano

Koran 5:3 .......Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu,.....

Surah ya tano kakamilisha Uislamu na Kuna surah zaidi ya 100 mbele ?

Ni ujinga wa Allah au ni waislamu wamebadili ?
Ukiwa mjinga na kujitoa ufahamu kiasi hiki itabidi nikupuuze tu like your fellow Pathetic Scumbags.

Mbona watu kwenye makabati Yao nguo hawapangilii kutoka ya Zamani mpaka mpya bali wengi hupanga randomly ?

Aya hiyo ya kukumilishwa dini kuwa katika sura za Mwanzo sio hoja kama haikutakiwa kupangiliwa hivyo sawa mtu adai Mwenyezi Mungu hayupo au kumtoa dosari kisa uwepo wa Maradhi na umasikini lakini kumbe kuwepo kwa vitu hivyo sio alama ya udhaifu kwa Mwenyewezi Mungu ni katika hekima zake ila ukiwa na akili finyu kama zako utawaza negatively.

Ukisema imepangwa tofauti weka ushaudi , sio kwa tu Aya hiyo kuwa mwanzo kwani umbeambiwa ni makosa au yeye hawezi kupanga hivyo? ukisema jambo weka na ushahidi .

Ujinga uliopo kwenye mfano wako ni sawa na Mimi Leo nimuone Rais Samia anatembea kwa miguu niseme sio yeye Rais hawezi kutembea vile lazima abebwe na magari ya kifahari , sasa wapi Kuna makosa kutembea kwa miguu , wapi kasema hawezi kufanya hivyo au alipokatazwa ?

Kama una ona hiyo Aya kuwa hapo ni shida yako kutokana na ujinga wako au ubishi Wala hakuna tabu yeyote kwa Wasomi na Wenye akili.
 
Na zilivyopangiliwa sura kwenye Quran na Allah naye alizipanga hivyo?
Ndio , mpangilio kuwa Aya fulani ikae katika sura Fulani na ipi ikae wapi ni ufunuo kutoka kwa Allah kupitia Malaika Jibril finally kwa Mtume Muhammad (ﷺ) na hakuna aliyepanga kwa matashi yake.

Hapo nimezungumzia Aya (verses )maana haikuwa zikija sura full mara nyingi zilikuwa zinashuka Aya fupi fupi au ndefu , kwenye sura(chapters )kupangilia kama hii ya kwanza na hii ya mwisho hapo sina Elimu nalo mpka nifuatilie .
 
Back
Top Bottom