PreGE2025 Heche: Polisi wamezingira nyumbani kwangu na kwa Tundu Lissu

PreGE2025 Heche: Polisi wamezingira nyumbani kwangu na kwa Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ameandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa nyumba yake imezingirwa na polisi wakiwa na gari nne. Anaandika;

"Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo. Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia."

View attachment 3318341

Hapo awali Heche alieleza pia kuwa polisi wamezingira nyumbani kwa Tundu Lissu ambapo walikuwa wakitaka kuingia ndani lakini ndugu waliwazuia. Heche anaandika;

"Tangu saa sita usiku polisi wamezingira Nyumbani kwa mhe Lissu, wamejaribu kutaka kuingia ndani, lakini ndugu wamewambia kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo."
View attachment 3318343
Soma pia: Wakili Jebra Kambole ahoji kitendo cha polisi kutaka kwenda kupekua nyumbani kwa Lissu bila amri ya mahakama
Wakili JK, wewe uko nchi gani? Polisi hapa kwetu sasa hivi ndiyo kila kitu....wanaweza kukuvunja miguu, mikono, makalio na hata kukuua na hakuna atakayewauliza kitu.
 
Kwahiyo unashangilia mwendelezo wa udikteta, you're doomed.
Hapana ila sisi tuliwaambia wahuni hawa akina Lisu waache kushangilia kifo maana aliyekufa ni mtu mmoja tu ktk mfumo na alikuwa hahusiki kutoa amri ya watu kukamatwa. Ila wao wakashupaza shingo hahaha acha washughulikiwe
 
Madness, unazingira nyumba ya mtu ambaye teyari unamshikilia.
 
Watanzania waoga sana.Sisi kwetu Congo tulikinukisha Hadi serikali wameacha mambo Yao ya kijinga kama haya ya polisi kukiuka taratibu zao za kazi
 
Makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ameandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa nyumba yake imezingirwa na polisi wakiwa na gari nne. Anaandika;

"Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo. Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia."

View attachment 3318341

Hapo awali Heche alieleza pia kuwa polisi wamezingira nyumbani kwa Tundu Lissu ambapo walikuwa wakitaka kuingia ndani lakini ndugu waliwazuia. Heche anaandika;

"Tangu saa sita usiku polisi wamezingira Nyumbani kwa mhe Lissu, wamejaribu kutaka kuingia ndani, lakini ndugu wamewambia kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo."
View attachment 3318343
Soma pia: Wakili Jebra Kambole ahoji kitendo cha polisi kutaka kwenda kupekua nyumbani kwa Lissu bila amri ya mahakama
Wanataka wapike details za ushahidi wa uongo
 
Yaani mimi nakenue mpaka gego la mwisho halafu nimeweka kijiti natoa vinyama kwenye meno hahahah. Mlishangilia kifo cha Dkt Magufuli hahahah. Tuliwaambia muomboleze maana aliyeondoka ni mmoja tu wengine wapo hahaha
Before kuingia kwa magufuli , hawakuwah kujua namna ya kutumia hivi vyombo ku suppress political opponents. Maguful akaja akawaonyesha how to do it, for their advantage aka yeye ndio muasisi.

Despite yule baba alikuwa na mazuri yake pia, alifanya mengi. But kwenye politics mambo yalikuwa magum
 
Back
Top Bottom