PreGE2025 Heche: Polisi wamezingira nyumbani kwangu na kwa Tundu Lissu

PreGE2025 Heche: Polisi wamezingira nyumbani kwangu na kwa Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ameandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa nyumba yake imezingirwa na polisi wakiwa na gari nne. Anaandika;

"Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo. Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia."

View attachment 3318341

Hapo awali Heche alieleza pia kuwa polisi wamezingira nyumbani kwa Tundu Lissu ambapo walikuwa wakitaka kuingia ndani lakini ndugu waliwazuia. Heche anaandika;

"Tangu saa sita usiku polisi wamezingira Nyumbani kwa mhe Lissu, wamejaribu kutaka kuingia ndani, lakini ndugu wamewambia kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo."
View attachment 3318343
Soma pia: Wakili Jebra Kambole ahoji kitendo cha polisi kutaka kwenda kupekua nyumbani kwa Lissu bila amri ya mahakama

Kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo (punto!)
 
Mama kaamua kuleta mambo ya Museveni na Besigye Tanzania.

SAMIA MITANO TENA.
 
Sijawahi kuiba upuuzi kama huu eti mnaenda kupekuwa nyumba ya mtu huku mwenyewe hayupo.
Akili ya Dikteta Uchwara toka Oman.
 
Dikteta Sami na Dj Mbowe kwenye 1 na 2
Dj kweli mtu mbaya sana alimchonganisha Jiwe na Marehemu aliyekuwa anafuatilia PhD Mbowe alikuwa anamfadhili kijana yule
Kumbe yote Yale Mbowe ni project!!

MUNGU atajibu!!
 
Anachofanya Heche yupo sawa anachotaka yeye ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenda mahakaman, unadhan anaweza kuhamasisha kwa siri anahamasishaje?
Kuhamasisha ni vizuri ila siyo kuweka ufafanuzi wenye mgangano wa kimasilahi hata hivyo viongozi wa kitaifa inatakiwa watunze na kuzichunga kauli zao

Silence surrenders public responsibilities

Kunyamaza siyo amani ball ni kusalimu amri kwa majukumu ya kijamii ama kitaifa
 
Mbona CCM wanatumia nguvu kubwa sana na raslimali watu bila sababu?
Siku zote yana mwisho na mwisho huwa sio mzuri bali aibu.
 
Tangu saa sita usiku polisi wamezingira Nyumbani kwa mhe Lissu, wamejaribu kutaka kuingia ndani, lakini ndugu wamewambia kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo.

#John Heche.

Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo.

Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia.

#John Heche.
Vilaza kabisa na hii mvua inayonyesha usiku kuchwa unakesha kwenye geti na mwanaume mwenzio unamuacha mkeo

Kazi zingine laana Sana
 
Makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ameandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa nyumba yake imezingirwa na polisi wakiwa na gari nne. Anaandika;

"Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo. Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia."

View attachment 3318341

Hapo awali Heche alieleza pia kuwa polisi wamezingira nyumbani kwa Tundu Lissu ambapo walikuwa wakitaka kuingia ndani lakini ndugu waliwazuia. Heche anaandika;

"Tangu saa sita usiku polisi wamezingira Nyumbani kwa mhe Lissu, wamejaribu kutaka kuingia ndani, lakini ndugu wamewambia kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo."
View attachment 3318343
Soma pia: Wakili Jebra Kambole ahoji kitendo cha polisi kutaka kwenda kupekua nyumbani kwa Lissu bila amri ya mahakama
Sawa. Mimi bado nipo kwa Moses Mabhida Stadium Durban Africa Kusini tukipanga safari ya kurudi nyumbani kibabe baada kukamilisha kazi kazini. Nikirudi nitalifuatilia hilo suala lako
 
Back
Top Bottom