PreGE2025 Heche: Polisi wamezingira nyumbani kwangu na kwa Tundu Lissu

PreGE2025 Heche: Polisi wamezingira nyumbani kwangu na kwa Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

View:






Kwa Mtu yoyote yule ambaye ana uelewa mpana kuhusiana na masuala haya ya Siasa za Ulimwengu juu ya masuala ya Utawala wa nchi, anatambua wazi kabisa kwamba hizi ni dalili za mwisho kabisa kuhusiana na hatma ya Utawala fulani kabla ya Utawala au Dola hiyo kuanguka na kuhitimisha enzi zake, it is The Beginning of the End!

The last kick of a dying horse.
 
BREAKING: Jeshi la Polisi limeizingira nyumba ya Mwenyekiti wa Chadema tangu saa sita usiku. Lengo ni kuingia na kusachi nyumba yake. Mpaka sasa waliomo ndani wamegoma kuwaruhusu polisi kuingia.
majambazi ya ccm genge la wahuni wanataka kumbambikizia madawa ya kulevya
 
Yaani mimi nakenue mpaka gego la mwisho halafu nimeweka kijiti natoa vinyama kwenye meno hahahah. Mlishangilia kifo cha Dkt Magufuli hahahah. Tuliwaambia muomboleze maana aliyeondoka ni mmoja tu wengine wapo hahaha
Kwahiyo unashangilia mwendelezo wa udikteta, you're doomed.
 
Chadema do not know how to deal with savages,

Heche has big mouth
Heche hana kaba anatoa Siri nini watafanya kesho yake
Anachofanya Heche yupo sawa anachotaka yeye ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenda mahakaman, unadhan anaweza kuhamasisha kwa siri anahamasishaje?
 
Makamu mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ameandika kupitia ukurasa wake wa X kuwa nyumba yake imezingirwa na polisi wakiwa na gari nne. Anaandika;

"Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo. Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia."

View attachment 3318341

Hapo awali Heche alieleza pia kuwa polisi wamezingira nyumbani kwa Tundu Lissu ambapo walikuwa wakitaka kuingia ndani lakini ndugu waliwazuia. Heche anaandika;

"Tangu saa sita usiku polisi wamezingira Nyumbani kwa mhe Lissu, wamejaribu kutaka kuingia ndani, lakini ndugu wamewambia kama wanataka kufanya ukaguzi lazima mwenye nyumba awepo."
View attachment 3318343
Soma pia: Wakili Jebra Kambole ahoji kitendo cha polisi kutaka kwenda kupekua nyumbani kwa Lissu bila amri ya mahakama
Hawa wezi hawataki kuachia madaraka kistaarabu, tusali na kufunga Mungu aingilie kati
 
Back
Top Bottom