Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe ndio mnafiki na Hujitambui!

Heche amekuwa akisema hayo tangu akiwa bungeni
Tatizo sio kusema tu.Na empty words. Ni kushughulika na tatizo kwa kutopokea hiyo posho.Huwezi ukawa unahubiri kuhusu maji halafu unakunywa mvinyo.
 
Kwanini ulikua unakubali kupokea na haukuleta hiz hoja wakati ukiwepo bungeni
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Mtumishi wa umma hawezi kukataa mshahara na posho zake anazostahili. Atalipwa tu stahili yako hata aseme nini. Njia pekee ya kuzuia kulipwa ni kuacha kazi. Anachoweza kufanya ni kuupokea na kuutumia kuwahudumia wananchi wenzake na kuendelea kupiga kelele.

Amandla...
Angepokea na kutoa kwenye charity ili kuongeza credibility yake.Kulalamikia jambo ulilokuwa ukifanya una raise doubt.Au at least ange come clean sasa na kusema alipokea hiyo posho kimakosa kwani hakustahili.
 
Hawezi kusema kuwa alipokea kimakosa kwa sababu alistahili kulipwa mshahara na posho hizo kwa mujibu wa miongozo ya Bunge. Sio tu kuwa alikuwa anasaidia jamii yake bali wabunge wa CDM walikuwa wanachangia sana gharama za kuendesha chama chao. Credibility yake kwenye hili suala iko juu.

Amandla...
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Hawezi kusema kuwa alipokea kimakosa kwa sababu astahili kulipwa mshahara na posho hizo kwa mujibu wa miongozo ya Bunge. Sio tu kuwa alikuwa anasaidia jamii yake bali wabunge wa CDM walikuwa wanachangia sana gharama za kuendesha chama chao. Credibility yake kwenye hili suala iko juu.

Amandla...
Na walikuwa wanatumia hizo posho kuchangia Chama chao.Hapo ndio panafanya usiwe credible.Unaposhiriki kwenye kupokea posho na mishahara kwa mujibu wa miongozo iliyopo basi unakuwa part and parcel ya hayo maamuzi.
Wange boycott kuonyesha kwamba wao wapo tofauti ndio wangekuwa credible.Huwezi kushiriki kwenye zoezi unaloamini kwamba sio sawa kwa kisingizio kwamba miongozo inasema hivyo.
Inakuwa vigumu kuaminika unapobadilisha upande.
 
Upo sahihi kiasi

Ila mshahara haumtoshi mtu hata siku moja mkuu...

Hao wabunge wenyewe wana madeni ya kuwatosha na bado wanakopa na wakitoka huko hali mbaya
Hapana. Kila nchi ina takwimu za kiasi gani mtumishi anahitaji ili kukimu maisha. Nchi makini inahakikisha kuwa wanaofanya kazi wanaweza kuishi kutokana na mshahara wao. Kampuni inayoweza kumlipa Meneja milioni 18 haistahili kulipa wafanyakazi wa chini mishahara ya kitwana. Ukiangalia taasisi zote zinalipa mabosi mishahara minono ( TRA, BOT, Tanapa n.k.) hata wale wa chini nao ni alhamdulilah.

Wabunge wengi hawajui thamani ya pesa. Ndio maana mbunge ambae ni mke wa Rais mstaafu, mwenye mtoto waziri anaweza kudai alipwe posho ya ex First lady kwa sababu kipato chake hakitoshi. Na wabunge wenzake wakamuelewa na kuridhia! Na huyu aliwahi kuwa mwalimu kwa hiyo anajua machungu ya walimu wenzake.

Amandla...
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Mnafiki tu huyu.Angelalamika kwamba posho ni kubwa ipunguzwe akiwa mjengoni angekuwa na credibility. Kuwa nje ya mjengo halafu ulalamike ni unafiki tu na hadaa.
Sikiliza video mkuu, Hoja yake sio kuwa posho za wabunge ni kubwa zipunguzwe, hoja yake ni kuwa inawezekana wote kulipwa vizuri, wabunge, walimu wote inawezekana kulipwa vizuri iwapo hao wanaolipwa vizuri bungeni wakiamua kupigania maslahi ya wengine.
 
Na walikuwa wanatumia hizo posho kuchangia Chama chao.Hapo ndio panafanya usiwe credible.Unaposhiriki kwenye kupokea posho na mishahara kwa mujibu wa miongozo iliyopo basi unakuwa part and parcel ya hayo maamuzi.
Wange boycott kuonyesha kwamba wao wapo tofauti ndio wangekuwa credible.Huwezi kushiriki kwenye zoezi unaloamini kwamba sio sawa kwa kisingizio kwamba miongozo inasema hivyo.
Inakuwa vigumu kuaminika unapobadilisha upande.
Unaongea kama vile walikuwa majority. Niambia kupokea kwao stahili zao kuli affect vipi adhma yao ya kusimamia serikali na kuwatetea wananchi wenzake? Ni bora kuendelea kupokea stahili zao kuliko kukimbia mapambano kwa kisingizio kuwa hakubaliani na stahili zake. Hypocrites ndio watasema kuwa amepoteza credibility.

Amandla...
 
"Sisi posho siku moja tu bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4," John Heche Makamu Mwenyekiti CHADEMA
 
Mbona hakusema kipindi anapokea hizo posho?
Kwaiyo kama hakusema kipind anapokea basi ndo kiwe kigezo cha yeye kukaa kimya kufumbia ujinga...hilo linalofanyika wewe unaona ni sahihi?

Embu wakati mwingine tuwe tunajaribu kufikiri kwa kina.
 
Kwaiyo kama hakusema kipind anapokea basi ndo kiwe kigezo cha yeye kukaa kimya kufumbia ujinga...hilo linalofanyika wewe unaona ni sahihi?

Embu wakati mwingine tuwe tunajaribu kufikiri kwa kina.
Hapana ila tunamwona ni mwanasiasa mnafiq anayefanya siasa za hadaa
 
Back
Top Bottom