Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

As much as I agree na wewe ila ungeanza kuwakumbusha kwanza hao kufanya wajibu wao. Comparison ya Mzazi na Rais doesn't hold water.

Mzazi sikumchagua. Rais anachaguliwa.

Mzazi hanilipishi kodi. Rais na serikali yake wanakula kodi zetu bila kutimiza wajibu wao.

Afu sifa zote mnampa rais ila lawama mna deflect. You seem to have selective competence.
Dhahabu kwenye shamba lako mali ya jamhuri ila bangi za kwako. Hii theory wanai apply kila sehemu.

Sifa njema, mama kaupiga mwingi. Vikivurundwa basi 'mama' hausiki.
 
Tusichaguliane marafiki au maadui. Pia tusichaguliane upande katika mirengo ya kisiasa. Kila mtanzania ana uhuru wa kuchagua kile anaamini ni sahihi kwake. Sio kwa kuwa flani ni CCM atulazishe tuchukie Chadema au Chadema atulazimishe tuchukie CCM. Tutakae kuwa mavuvuzela wa wanaharakati.
 
Shida ya wanaharakati wa UFIPA wanadhani wanashikia akili watu. Yaani kama ambavyo wao wameshikiwa akili na viongozi wao basi wanaamini kabisa wana haki ya kuamua nani aseme nini na nani asisemi nini kwa wakati gani..
 
Acheni siasa nyepesi eti kukosoa kwa stara hicho kitu hakina mantiki.
Kale ka dc ka kisarawe kana ka msemo wake ukija kihuni unajibiwa kihuni na ndivyo inavyotakiwa.
Sasa mtu ukose ujibiwe kwa stara huo upumbavu haukubaliki.
Tena ukiwa kiongozi wa serikali una disposal ya resources kibao kusapoti shughuli za serikali sasa ufanye makosa ya kijinga ukikosolewa useme nikisoe kwa stara huo upumbavu nausikia Tanzania tu na ndio unafanya viongozi wajisikie miungu watu.
Hata madhabahuni wachungaji wanakemea mapepo kwa lugha kali hauwezi kusikia mchungaji anasema eti anakemea mapepo kwa stara.
Huu msamiati mpya wa kukosoa kwa stara ni msamiati wa kishenzi ,kijinga na kipumbavu na wote wanaoutetea ni washenzi wapumbavu na wajinga
 
Wanaukumbi.

Vijana wa Tanzania, taifa linalotilia mkazo maadili mazuri mnawezaje kumtukana Rais SuluhuSamia matusi mazito?

Kuna uhusiano gani kati ya kudai haki au kukosoa Utendaji wa Serikali na matusi? Kwani mama au baba zenu wakikosea huwa pia mnawatukana? Badilikeni, matusi sio uungwana.

Kundi la watu wanaojiita wanaharakati ("Team Space") wanatuumia

Nguvu kubwa kugawa watanzania "Divide and Rule" ili Watanzania wasiwe na sauti moja. Matokeo yake mnakuwa kama lugha gongana "mlima babeli"

Harakati hizi ni kwa manufaa ya wachache, haziwezi leta mabadiliko, kamwe!

Haki haipiganiwi kwa matusi au kutweza utu wa wengine. Ni muhimu kukumbusha vijana kwamba hakuna harakati za demokrasia na haki zilizowahi kushinda bila watu kupendana, kuwa wamoja na kuwa na sauti moja. Team Space inatengeneza "DIVIDE AND RULE" harakati za maslahi kupiga hela

PIA SOMA
- Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
Nionavyo mimi matusi hayaelekezwi kwa Rais peke yake napendekeza tuwe na mjadala wa kitaifa kuhusu maadili kwa wote

Tanzania kuna matabaka kunawale wenye haki ya kusema chochote tena wakatoa hata mapovu mdomoni lakini hawatakamatwa, sita wataja kwa maana nikiwataja wanaweza wakawa wasiojulikana taraji kwangu, tabaka lingine la wale waliochoka kuonewa ama mawazo mbadala hawa watapigwa vilungu na kufanyiwa unyama ambao haufai hata kuelezea hapa

Tuliandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukivihoji kwenye ngazi hiyo unaweza ambiwa kama umekua uondoke matokeo yake ni kwamba athari za kukataa kuhojiwa zimebebwa na jamii kwenye ngazi zote za maisha yetu, kwa sasa washika tonge hawakubali kunyang'anywa tonge mdomoni kisa kuhoji na ndiyo maana wanaahirisha kufikiri kwa nafsi.

Hii tabia kwasasa inatumika vizuri na baadhi ya wanao pewa dhamana wanaahirisha kufikiri kizalendo a.k.a kujizima data, yaani unyumbu, mimi hii tabia nina maelezo yake kama yafuatayo, unyumbu ni tabia ya wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii

Unyumbu kwa mtizamo wangu ndiyo sababu kubwa ya kuligawa taifa mambo mengi hayaendi ipasavyo na hayatakuwa kwasababu ya tabia ya unyumbu, (kuahirisha kufikiri kizalendo) sitakosea kusema ufisadi ni zao la kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.w kujizima data

Hawa wenye tabia ya unyumbu ukiwaambia tuwe na mjadala wa kitaifa kuhusu kuahirisha kufikiri kizalendo watapata kigugumizi mfano hai kuna mdau alisema walienda maporini,................, mwingine eti anaye fikiri kizalendo, (propaganda), alienda mwenyewe maporini kuchimba dawa hakutumwa.
 
Utumishi wa umma hauwezi kulinganishwa na u baba/mama kwenye familia, kufanya hivyo ni sawa na kutafuta huruma nyepesi kwenye masuala magumu. Ukiona utumishi wa umma una matusi mengi sio dhambi kuachia ngazi na kuendelea kuwa mama/baba wa familia yako, unapoamua kuwa muajiriwa wa watu zaidi ya milioni 60 ni vyema ukajiandaa kupokea hata matusi kutoka kwa waajiri wako maana si wote wenye akili za kufanana. Hautumikii miti unatumikia watu
 
Back
Top Bottom