Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Hoja nzuri ni ile inayotolewa kwa lugha nzuri na staha. Huwezi kumjadili Mhe. Rais na CI kirahisi na lugha isiyo na staha! Uhuru wa maoni ni jambo chanya la maendeleo siyo jinai.🙏🙏🙏
Heshima nzuri ya rais inapatikana kupitia uchaguzi wa heshima. Kwa ule uhayawani uliofanyika uchaguzi wa 2020 sioni hii kutaka heshima inatoka wapi. Labda kama unaongelea nidhamu ya woga.
 
Wanabodi,
makala ya leo ni makala elimishi ikielimisha kuhusu heshima ni kitu cha bure, hivyo kuwaelimisha wana jf na mitandao ya kijamii, kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote, lakini ni lazima aheshimiwe na wote kwasababu mtu akiishakuwa rais wa nchi, hapo hapo ana assume dual personality, yaani wanakuwa ni watu wawili in one!, hivyo rais wa nchi ni lazima aheshimiwe kwa heshima ya lazima ya kimamlaka, akosolewe kwa lugha ya staha, asitukanwe wala asitusiwe!.
P
Yapo mashetani ya kike, huyu Mzanzibari ni mmojawao
Mkuu Gulwa ,ni katika kukumbushana tuu,kuwa heshima ni kitu cha bure,na kuna heshima ya lazima ya utii kwa mamlaka halali
P
 
Mkuu Gulwa ,ni katika kukumbushana tuu,kuwa heshima ni kitu cha bure,na kuna heshima ya lazima ya utii kwa mamlaka halali
P
Muuaji wa vijana wasio na hatia, fikilia wangekuwa ni wanao au ndugu zako. Mimi ni Yohana mbatizaji, nakemea maovu bila kujali matokeo yake kwangu. Niko tayari kwa lolote. "Bwana asipoulinda mji, waulindao wakesha bure"
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni makala elimishi ikielimisha kuhusu heshima ni kitu cha bure, hivyo kuwaelimisha wana jf na mitandao ya kijamii, kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote, lakini ni lazima aheshimiwe na wote kwasababu mtu akiishakuwa rais wa nchi, hapo hapo ana assume dual personality, yaani wanakuwa ni watu wawili in one!, hivyo rais wa nchi ni lazima aheshimiwe kwa heshima ya lazima ya kimamlaka, akosolewe kwa lugha ya staha, asitukanwe wala asitusiwe!.

Hoja hii ni kufuatia mjadala mingi kwenye mitandao ya jamii kwenye issue ya Bandari yetu na DPW, kuna watu wamevuka mipaka na kumkosea heshima Rais Samia na kumkosoa kwa lugha kali, kumtweza, kumkashifu na wengine kuvuka mipaka kwa kumtukana hadi matusi ya nguoni!, this is not right!.

Angalizo la Uzalendo Uchawa Vs Uzalendo Halisi!.

Kufuatia kuibuka kwa dhana ya uchawa, kuna watu wanajiita kabisa chawa wa Mama, hivyo mtu kama mimi nikijitokeza kutaka Rais Samia aheshimiwe wote, watu wenye akili fupi hawachelewi kuniona chawa!. Mimi sio chawa na hili sio bandiko la uchawa! ni bandiko la kukumbushana heshima ya kiasili ya Kiafrika ya heshima kitu cha bure, mkubwa kumheshimu mdogo, na mdogo kumheshimu mkubwa, heshima kwa wote.

Declaration ya Kutosaka Uteuzi.
Kumezuka mtindo wa sisi waandishi wa habari na watu wa media, tukiusifu utawala kwa mazuri au tukisifu viongozi, tunaonekana kuwa tunasaka uteuzi, naomba niwahakikishie tena Paskali hasaki uteuzi wowote na hili Paskali aliisha mueleza mteuzi mwenyewe face to face Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

The Duality of President. heshima ya lazima ya kimamlaka!, Akosolewe kwa Staha na Asitukanwe!.
Duality ni kanuni ya mtu mmoja ku na personalities mbili kwa wakati mmoja.
Rais wa nchi ni dual personality ana personalities mbili ambazo ni duality but they exist in one!. Yaani ni mtu mmoja mwenye two personalities ambazo zina exist in one and at the same time.

Kanuni hii ya double personalities au dual personality imezungumzwa vizuri na Mwana Saikolojia mahiri wa Marekani, Dr. Segmund Freud katika kukichambua kitabu cha Dr. Jekyll and Mr. Hyde, kilichoandikwa na Dr. Robert Luis Stevenson aliyeandika pia kitabu cha Kisiwa chenye Hazina, Treasure Island, ambapo mtu mmoja mwenye double personality mchana yuko vingine na usiku yuko vingine kama watu wawili tofauti.

Hii duality ipo sana kwa binadamu wote, yaani nafsi na roho, au me & I. mambo kama ya de javu, third eye, physical body na astra body, mambo ya ying na yang, vyote hivi vinatumia kanuni ya duality.

Wanawake wengi wanalelewa kwa kuandaliwa kuwa wife materials, ili kupata mchumba hivyo katika kusaka ndoa anakuwa na one personality na akiisha pata ndoa na kuolewa, ana change na ku show her true colours!.

Jamii zetu nyingi za kiasili za Kiafrika kina watu wanaishi double life mfano mzuri ni wanga, wachawi na washirikina, ukiwaona mchana ni watu wa kawaida, lakini usiku ni watu wengine kabisa!.

Na kwenye siasa ndio usiseme!.

Persnality ya kwanza ya Rais wa nchi ni human personality, yaani rais ni binadamu, a human being kama binadamu mwingine yoyote wa kawaida anayestahili mahitaji tote ya kibinadamu, hivyo rais wetu Samia ni mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan, Huyu ni human being, she has all human needs including feelings, love and compassion na ana mahitaji mengine yote ya kibinaadamu ikiwemo kupenda, kupendwa na heshima, love and dignity and can make mistakes just like any other human beings. Hivyo huyu Samia ambaye she is only a human, unaweza kumpenda au usimpende, unaweza usimkubali, unaweza kumbeza, unaweza kumtukana na kumdhalilisha au kusema chochote kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan na hakuna tatizo!. Mfano mzuri wa hili ni huyu mtu niliyemzungumzia hapa Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? bandiko kama hili liliwezekana kupandishwa kwasababu she is just a human na enzi hizo alikuwa na single personality, sasa with dual personality bandiko kama hili haliwezi kupanda.

Jee ni lazima kumpenda Rais?.
Kumpenda mtu yoyote ni person preferences, mtu yoyote anaweza kumpenda mtu mwingine yeyote, kwa sababu zozote au bila sababu, au unaweza usimpende kwa sababu zozote, au bila sababu, na hakuna kosa lolote kutompenda yeyote lakini hata ikitokea mtu fulani humpendi, bado una wajibu wa kumheshimu na kuulinda utu wake.

Hivyo watu wako huru kumpenda Rais Samia ama kutompenda, it's an option lakini kumheshimu is not an option ni wajibu ndio maana kumtukana mtu ni kosa.

Personality ya pili ya Rais Samia, ni rais wa nchi, hivyo huyu binadamu anaitwa Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwa ni rais wa nchi ana, assume kitu kinachoitwa presidential personality, huyu sasa sio mtu binadamu, ni mtu taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ndani ya JMT, hivyo rais wa nchi kwa personality yake ya urais, ni lazima aheshimiwe, utii kwa mamlaka, huwezi kumtukana, huwezi kumdhalilisha, itakuwa ni kuitukana taasisi ya urais. Dini zote zinafundisha utii kwa mamlaka, iwe ni mamlaka halali au haramu, una wajibu wa kutii mamlaka, ndio maana hata enzi za yule Blaza wangu, kabla hajagombea urais, toka ile 2014 nilipoambiwa ni yeye, nilileta angalizo humu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli baada tuu ya kushinda nikatoa ushauri huu Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! na pia nikatoa angalizo hili Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!
Hivyo despite all the odds heshima na utii kwa mamlaka ni jambo la wajibu!.

Rais Samia kama taasisi ya urais, huhitaji kumpenda lakini ni lazima kumheshimu!. Rais Samia kama taasisi ya urais, she is not human, hawezi kufanya makosa ndio maana hawezi kushitakiwa!.

Wito kama huu niliwahi kuutoa enzi za utawala wa JK, Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim! na wakati wa Magufuli pia nilishauri Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli
Hivyo sasa tuko na Samia, tunaweza tusimpende lakini lazima tumuheshimu na ukitokea ukosoaji, tumkosoe kwa lugha ya staha na sio kumtukana na kumdhalilisha.

Niliwahi kushauri humu kuwa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda unaweza usimpende lakini ni lazima kumheshimu.

Hitimisho
Rais Samia ni rais wetu, tumpende, tumheshimu, tumsuport, na hata ikitokea, kuna sehemu anakosea tumkosoe kwa heshima na staha.
Kwa sisi wengine ambao tunamkubali Samia kama Mama, mzazi wako, hata akukosee vipi, kamwe huwezi kumtukana!. Samia ni Mama wa Taifa, tumheshimu.

Namalizia kwa msisitizo huu

Heshima Kitu cha Bure, Rais Samia, ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe!.​

Paskali

"lakini ni lazima aheshimiwe na wote?" Ondoa ? ili lisiwe swali uwe wajibu wa kibinaadamu.​

 
Muuaji wa vijana wasio na hatia, fikilia wangekuwa ni wanao au ndugu zako. Mimi ni Yohana mbatizaji, nakemea maovu bila kujali matokeo yake kwangu. Niko tayari kwa lolote. "Bwana asipoulinda mji, waulindao wakesha bure"
Kuna kitu kinachoitwa utii kwa mamlaka。 Mamlaka ya kwanza kutoka chini ni ngazi ya familia,mkuu wa familia ni baba lazima aheshimiwe。 Ngazi ya taifa ni rais,na mamlaka Kuu ni Mungu mwenyewe。Huwezi kumuita hivyo kiongozi wako。
P
 
Kuna kitu kinachoitwa utii kwa mamlaka。 Mamlaka ya kwanza kutoka chini ni ngazi ya familia,mkuu wa familia ni baba lazima aheshimiwe。 Ngazi ya taifa ni rais,na mamlaka Kuu ni Mungu mwenyewe。Huwezi kumuita hivyo kiongozi wako。
P
Kuna mamlaka halali na haramu. Watu wanaoingia madarakani kwa udanganyifu hawastahili kupewa heshima hata kidogo , labda kwenu nyie machawa wao
 
Kuna mamlaka halali na haramu. Watu wanaoingia madarakani kwa udanganyifu hawastahili kupewa heshima hata kidogo , labda kwenu nyie machawa wao
Kuna aina mbili za tawala
za mataifa, defacto na
dejure, zote mbili zinawekwa na Mungu, hata madikiteta ni Mungu huwaweka na huwaondoa.
P
 
Labda huyo ni Mungu msukuma, Mungu wa kweli ni wa haki tu
Mungu ni mmoja tuu, The One and Only, hakuna Mungu wa Wasukuma wala wa kabila lolote.

Pia ni kweli, japo Mungu wa kweli ni Mungu wa haki, lakini kuna wakati anaacha watu wake wale kichapo.
P
 
Mungu ni mmoja tuu, The One and Only, hakuna Mungu wa Wasukuma wala wa kabila lolote.

Pia ni kweli, japo Mungu wa kweli ni Mungu wa haki, lakini kuna wakati anaacha watu wake wale kichapo.
P

,
Hakuna Mungu wa double standard, huyo ni shetani
 
Hakuna Mungu wa double standard, huyo ni shetani
Ni kweli Mungu ni mnyoofu
Ila kuna vitu vibaya vinatokea ni Mungu anaviruhisu, zikiwemo tawala dhalimu au viongozi madikiteta, wanawekwa na Mungu.

Fuatilia wakati anawatoa wana Israel kutoka Misri, alimfanya nini Farao, wazaliwa wa kwanza wanakosa gani?

Unajua aliwatuma wanawake wa Israel wakaazime vito vya gold, silver, fedha na shaba za wa Misri kwa ahadi watarudisha, wakalala nazo mbele!.

Hata Mfalme Daud kumtamani mke wa Uriah, Berthsheba, akamuua mumewe akamtwaa, ndie mama wa Mfalme Suleiman.
P
 
Kwa hiyo hata dhambi ni kazi ya Mungu!
No dhambi sio kazi
ya Mungu, dhambi zote ni kazi ya shetani ila ni Mungu ndiye anaruhusu na kumruhusu shetani, hata kule bustanini
Mungu alimuona alimuona shetani akimtempt Eva, akaona yote tangu tunda linachumwa, lina megwa Eva alivyo enjoy, akampelekea Adam, akamega wakaenjoy na kuishia zao usingizini, Mungu aliona yote na akaruhusu!.

Hata kusulubiwa kwa Yesu, ni Mungu aliruhusu The Role of Yuda Eskarioti Kwenye Ukombozi wa Dunia: Je, Yuda alaumiwe, alaaniwe au apongezwe?!

P
 
Mungu ni mmoja tuu, The One and Only, hakuna Mungu wa Wasukuma wala wa kabila lolote.

Pia ni kweli, japo Mungu wa kweli ni Mungu wa haki, lakini kuna wakati anaacha watu wake wale kichapo.
P
Paschal, mungu sio mmoja, wapo miungu wengi, India peke yake kuna miungu zaidi ya alfu kumi, uarabuni kuna mungu allah, hata hapa kwetu kuna vimiungu kadhaa. isipokuwa, MUNGU WA KWELI NDIYE MMOJA TU, naye ni Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, yaani Mungu wa Israel. miungu mingine yote ni ya uongo kwa sababu ni mapandikizi au maajenti wa shetani, ni kazi za shetani. miungu mingine yote hata kama ipo, haina nguvu kumzidi huyu Mungu wa Kweli. hata wasukuma wana vimiungu vyao kibao huyo simiyu ambako ukivuka nyumba 10 katikati kuna nyumba ya mganga wa jadi. mikoa yote pia. labda ungemfafanulia hivyo.
 
No dhambi sio kazi
ya Mungu, dhambi zote ni kazi ya shetani ila ni Mungu ndiye anaruhusu na kumruhusu shetani, hata kule bustanini
Mungu alimuona alimuona shetani akimtempt Eva, akaona yote tangu tunda linachumwa, lina megwa Eva alivyo enjoy, akampelekea Adam, akamega wakaenjoy na kuishia zao usingizini, Mungu aliona yote na akaruhusu!.

Hata kusulubiwa kwa Yesu, ni Mungu aliruhusu The Role of Yuda Eskarioti Kwenye Ukombozi wa Dunia: Je, Yuda alaumiwe, alaaniwe au apongezwe?!

P
Je unajua kwa nini Mungu alimkataa mfalme Sauli na kumbariki Daudi badala yake? Mfalme au mtawala asiyetenda haki hukataliwa na Mungu na wanadamu pia
 
Samia hawezi kuwa serious na 4Rs kwa mfano kuhusu kifo cha Mzee Kibao "kifo ni kifo tu".

Is she stupid, malicious or both?
Mkuu @kiranga,heshima kitu cha bure,rais wa nchi ni kama baba kwenye familia na akiwa ni mwanamke ni kama mama yako wa kukuzaa,kuna things you can't say about her even if she is!
P
 
Wanabodi,

Zawadi yangu kwa Birthday ya Mama nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.


Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
HBD Rais Samia!.
P
 
Back
Top Bottom