Heshima kitu cha bure. Rais Samia ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe

Duh...!.
P
 
Wanabodi,

Heshima Kitu cha Bure, Rais Samia, ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe!.​

Paskali
KIMAMA hiki Samia

Britanicca
Jina hili sii jina la heshima kwa mtu huyu, ila pia jina hilo sio la kweli kwake, ki ni kidogo, kifupi au chembamba, yeye ni mkubwa, mrefu na mnene, hawezi kuwa ki, labda ji...
P
 


Malaya Samuya akibwatuka maujinga yake ya Form Four Failure
Heshima kitu cha bure
P​

 
Nilikufahamu Pascal na kuanza kukufuatilia kupitia Babu Yangu Mika ya 2000 Alikuwa anakukubali mno
(Profesa......)

Ila Leo unanisikitisha sana Mimi mjukuu wa Profesa.
Umekuwa wa ajabu sana.
Sitaki kukuvunjia heshima yako. Lakini unakwaza.
 
Mzee PASKALI nakuomba chonde chonde uwe unatuwekea dibaji kila ukiweka mkeka aka bandiko lako hapa. Hii itatusaidia sisi wavivu wa kusoma, kuamua tuendelee kusoma au tuishie hapo hapo kwenye dibaji.

Sasa turudi kwenye maudhui ya "gazeti" lako Kwa jinsi ulivyomfagilia mama, haiyumkini sasa ni wakati sahihi kupata hata ka-ukuu wa mkoa au hata ka- uenezi wa CCM.
 
Nilikufahamu Pascal na kuanza kukufuatilia kupitia Babu Yangu Mika ya 2000 Alikuwa anakukubali mno
(Profesa......)
Ukinitajia huyo Babu yako, nitakushukuru sana,
Ila Leo unanisikitisha sana Mimi mjukuu wa Profesa.
Nimekusikitisha kivipi kwenye nini?.
Umekuwa wa ajabu sana.
Kivipi?
Sitaki kukuvunjia heshima yako. Lakini unakwaza.
Asante, nimekukwaza kivipi au kwenye nini?.

P
 
Ni kweli kama Raisi wa Nchi anapaswa kuheshimiwa haijalishi ni dikteta au mfuata Sheria na Katiba ya Nchi husika,Huwa Binadamu tunayofautiana jinsi ya kuwasilisha mawazo na maoni yetu
Akiwa kama Raisi wa Nchi nae anaowajibu wa kuwalinda watu wake bila kujali kuwa Wako upande Wake au kinyume chake!
Pia hata Yeye ni lazima achunge anachokisema Kwa Umma, Mfano kuita Wanaharakati ni kama Magaidi,hili kwako mkuu P Mayala limekaaje?
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU (The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:
  • Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.
  • Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.
  • Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.
  • Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.
 
Mwambie huyo mama wa kambo watoto wanaitaka nyumba ya baba yao!
Mama ni mama tuu, sio mama wa kambo!, kuna watu wenye akili fupi, wanadhani kwa vile eneo la iliyokuwa Tanganyika ni eneo kubwa, na Kizanzibar ni kiduchu, wanadhani wenye hakimiliki ya Tanzania ni Watanganyika halafu wanawaona Wazanzibari kama watoto wa kambo!. Ukweli ndani ya muungano watu wote ni sawa!, hakuna watoto wa ndani na watoto wa kambo, hivyo huyu mama Mzanzibari sio mama wa kambo!.
P
 
..Ni aibu sana Mama Abduli kuchangiwa bil 200 za kampeni halafu alizochangiwa na mafisadi?

..Nchi ime-stuck kwasababu ya ukilaza wa Mama Abduli.
Hiyo sifa hapo kwenye bold, sio sifa ya heshima kwa mtu wetu!.
huwezi kumuita nanilii wetu kilaza mbele yetu na sisi tupo tukanyamaza!.
Tuwe na heshima ...
P
 
We muuaji unaeng’ang’ania kiti cha urais bila idhini ya wananchi mpaka ukawatoa roho maelfu ya wananchi unataka uambiwe mara ngapi conditions za maridhiano??????
Mtu hawezi kumuita hivi kiongozi wetu!
Haya basi ngoja dada wa taifa nikusaidie tena maana naelewa uliishia form 4, tena kwa division 0 labda bado huja process in your dumb, evil, killer brain full of urojo.
This is not fair ni udhalilishaji kwa uongo na uzushi, ingawa ni kweli hakupata division 1, lakini pia sio kweli, alipata zero!, mtu ambaye ni kweli alipata zero ni Daudi Albert Bashite, ila baada ya kubadili jina, aliingia tena darasani yeye mwenyewe, akasoma, akafaulu na sasa ni bosi wangu. Msilete uzushi na uongo kuwa tunaongozwa na divisheni zero!, mtu hata ukipata D mbili ni Four na sio zero!, acheni uongo na uzushi!
@SuluhuSamia Sasa nisikusikie tena unasema bado unapokea conditions za “mwenzenu mmoja”.
Hii ni kauli ya dharau!
Mkuu Retired ,
Unapo copy and paste contents za vichaa fulani kutoka nje ya jf, kwa hapa jf, hayo maneno yanakuwa ni yako na sio ya huyu kichaa!, hivyo sasa unahesabika ni wewe ndie unayemuita mtu wetu hivi!,
Ukikutana na toxic contents huko machakani na vichochoroni, soma huko huko na uziache huko huko usituletee humu kutuchafulia jf yetu kuonekana tunatumia toxic contents za hawa vichaa wa mitandaoni.
Ni ushauri tuu.

P
 
Ndiyo maana nime delete some nasty contents, sikuwa na maana ya kusambaza matusi. But statements are true facts nitaziandika au copy and paste. Uongo sitausambaza, hapana.
 
Ndiyo maana nime delete some nasty contents, sikuwa na maana ya kusambaza matusi. But statements are true facts nitaziandika au copy and paste. Uongo sitausambaza, hapana.
Asante ubarikiwe sana!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…