Hii Dharau na Matusi kwa Watanzania mpaka lini? Tukatae kuwa sasa Inatosha

Hii Dharau na Matusi kwa Watanzania mpaka lini? Tukatae kuwa sasa Inatosha

Kaka hapa tulipo uwezekano wa kupata katiba mpya ni capital NO; kwa bahati mbaya hata katiba mpya hatuhakikishii wigo mpana wa kidemokrasia kwa sababu hata hii tuliyonayo ya 1977 inajitisheleza kiasi fulani kama ingetekelezwa na kuheshimiwa kwa sababu hakuna mahali popote katika katiba hiyo inaporuhusu matumizi ya vyombo vya ukandamizaji kuhujumu chaguzi mbali mbali au Rais kuwaagiza watendaji kwamba "nikuteue halafu uniambie mpinzani ameshinda? Kwa hiyo kama hakuna utashi wa kisiasa kuheshimu katiba, katiba mpya 10 haziwezi kutusaidia na hili linatokana na ujio wa tabaka jipya la "wajasiriamali wa kisiasa" ambao lengo lao kuu kwenye siasa ni maslahi binafsi, na hao ndio wanashinikiza kukosekana kwa uwanja linganifu kwenye siasa zetu na kusiginwa kwa haki za binadamu na kukosekana kwa utawala bora, wajasiriamali wa kisiasa wanaitafsiri demokrasia wapendavyo kwa manufaa yao.
 
Nmejaribu kusoma hii thread yangu sijaona kama kuna sehemu namsifia magufuli. Unaposoma tuliza akili usisome kwa macho tu.tumia na akili hata kidogo.sina ninayemsifia na nadhani ni bora kuwa na magufuli kuliko membe au makamba.

Mkuu kila uchao unafungua nyuzi za kumsifia magufuli... kwa taarifa yako MAGUFULI HATUMTAKI HATA KIDOGO.. NI WAPUMBAVU TU NDIO WANAMUELEWA..
 
Miaka ya nyuma Mtu anayegombea Urais wa Tanzania alikuwa anaangaliwa kwa umakini na kupimwa kwa akili,uwezo,busara na weledi wake.

Miaka hii hali hiyo imebadilika hasa baada ya kuonekana kuwa mtu yeyote anaweza kuwa Rais wa Tanzania ili mradi CCM imeamua.ikasababisha every tom,dick and harry kuwa na that feeling ya kuwa Rais.

Tulikosea kwa kikwete,tukaendelea na makosa hayo kiasi kwamba hayo makosa yamekuwa ni sehemu yetu ya kuchagua marais.tumefikia hatua tunadharauliana kiasi kikubwa sana na kuonana hatuna hata common sense.

Ni aibu kutaka MEMBE awe Rais wa Tanzania. ni aibu kutaka MAKAMBA awe Rais wa Tanzania. Ni dharau sana kwetu wenye utashi na akili timamu.dharau hizi zitaendelea kuna siku watu watakuja sema Bashite au Kibajaji awe Rais wa nchi hii.Matusi makubwa sana.

Sababu tu wanapata vijicent toka kwa watu hawa.unadhan mtu kama malecela anashindwa kupiga debe kuwa bashite awe rais wa nchi hii na akakosa waungaji mkono ndani ya watanzania zaidi ya mil 50?

Lakini hii ndo dharau yenyewe sasa.mtu kama membe uwezo wa kiuongoz hana alibebwa sana na bado alipwaya.Makamba hana akili ya kuwa rais...nyie kuleni pesa zao lakin msije kututukana sisi wenye akili humu JF. TUSHAONA MADHARA YA WATU WALIOBEBWA KWENYE UONGOZI HATUTAKI TENA. waliobebwa hukosa kujiamini,hutaka kuonekana wana nguvu ilhali hawana.hutaka ficha udhaifu wao kwa hali na mali.

Fikieni hatua mtuheshimu hata kidogo.matusi na dharau zenu zimefikia hatua mbaya.kuwa membe awe rais wa tanzania?makamba awe rais wa tanzania?keshokutwa mtasema nani?bashite?kibajaji?muro?

Hizo ni dharau kubwa sana kwa wananchi wa tanzania.najua njaa inaweza mfanya mtu aimbe chorus yoyote atakayopewa lakini basi usiimbe wimbo wa hata kuwatukana wazazi wako sababu ya njaa.
Gudume umesema la msingi sana nchi inanajisiwa hovyo hovyo kwa sababu ya njaa za wachache tu
 
Unajua magufuli kafaidika kwa vita ya membe na lowassa nami niliona ni bora magufuli kuliko membe.membe is the disaster... Acheni kabisa.hii inch ingekongoroka hasa na ni mtu wa visasi sana. Na alishasema siku akiwa Rais ana watu wake ambao wangemwelewa vizur yeye ni nani.hata busara hana...ni mtu wa hovyo hovyo.huyu ambaye alitamba kipindi kile kuwa nchi ya libya haiwez kupinduliwa na land cruiser mkonga akimtetea ghadaf na baada ya mapinduzi akaungana na waliopindua...ni mtu hopeless kabisa.

Kwa kuwa watanzania wana sifa ya kumsahau historia, tayari wamesahau hilo la Membe na pesa za Libya alizozitafuna.

Wanajifanya wamepotezea, akili za mtu maskini wa kufikiri hizo.

Tuache dharau "ignorance" tukubali ukweli.
 
CCM wana utaratibu wa kupokezana vijiti baada ya awamu mbili za utawala,sasa hiyo nguvu ya kumchallange mwenyekiti wa CCM na raisi wa jamuhuri wameipata wapi?
Kama Membe ana nia ya kweli ya kuongoza taifa hili siku za usoni itambidi kwanza ajisahihishe,azaliwe upya kisiasa vingibevyo ataamblia moshi kama maganda ya korosho.
 
Thread yako ina kila aina ya ukweli na busara. Asante sana. Eti Membe awe rais? Makamba awe rais? Watanzania tuache huu utani!
Taifa limepoteza mwelekeo.
Ni sawa na Mtoto asiyemjua baba yake kila atakayempa pipi barabarani atamwita baba.
Ujinga wetu ndiyo kula yao.

Tusipoamka tutazikwa tukiwa hai
 
kuna vijitu vijingavijinga vinataka kutuaminisha wao ndio vichwa wanaoweza kutuletea marais, ndio hao wanaoshinda mtandaoni wakituletea majina ya makamba, membe na wengineo ambao wamechukua vijisenti kwao.Vijitu hivi vinaweza kufanywa chochote ili mradi vimepewa pesa na ndio huwa wa kwanza pale mtu wao akichaguliwa na kutenda sivyo vinaanza kupiga kelele kama wana mahaba na hao watu kwanini wasiolewe nao kwani Urais ni taasisi kubwa ambayo inakosa heshima sababu ya watu kama hao

Hizo pesa zilikuwa zikiwekwa miaka 10 ya JK mahala na sasa zimetoka zinagawiwa kwa hao unawaona wanakuja hapa na mada zao mbalimbali kuhusu Membe.

Wameona mambo yao hayaendi.
 
Thread yako ina kila aina ya ukweli na busara. Asante sana. Eti Membe awe rais? Makamba awe rais? Watanzania tuache huu utani!
Siasa haizalishi tena viongozi Bali inazalisha maharamia wa kisiasa. Wanatumia kila silaha waliyonayo kutuchapia wapore vilivyo vyetu inauma sana.

Membe ? Makamba ? We can't be serious
 
Siasa haizalishi tena viongozi Bali inazalisha maharamia wa kisiasa. Wanatumia kila silaha waliyonayo kutuchapia wapore vilivyo vyetu inauma sana.

Membe ? Makamba ? We can't be serious

Hamna kitu hapo wanacheza tu na pesa zinaliwa.

Mazee wanawaangalia tu, kama wewe ni mfuatiliaji basi fuatilia ukaribu wa yule mzee wa zamani wa suti nyeusi na Lowasa uliishai wapi.
 
Hamna kitu hapo wanacheza tu na pesa zinaliwa.

Mazee wanawaangalia tu, kama wewe ni mfuatiliaji basi fuatilia ukaribu wa mzee wa zamani wa suti nyeusi na Lowasa uliishai wapi.
Inaiwe hivyo maana inakofikia sasa nchi itageuka demu wa kijiji kila mtu anajifunzia kugonga
 
Mbona umeishia kusema tulikosea kwa Kikwete, ulitakiwa kusema na kwa Magufuli pia tulikosea, woga wa watu kama wewe ndio umetufikisha hapa mnaogopa kusema ukweli kuwa huyu wa sasa ni afadhali ya Kikwete.
Huyu jamaa anachuki sana na Kikwete, nilikuwa najua ni great thinker anachambua vitu bila upendeleo ila nimeona anachuki binafsi na watu hasa Kikwete na walio karibu nae andiko lake la juzi limizihisirisha hicho, kiukweli mie nimempuuza
 
Hizi ni moja kati ya athari za vita dhidi ya upinzani
Upinzani ukifa nje ya chama tawala
Utazaliwa ndani ya chama tawala.
Na huenda ukawa mbaya kuliko ule uliokuwa nje.
Msidhani Nyerere alikuwa mjinga kuruhusu siasa za upinzani aliyaona haya
 
Membe na January ni watanzania wameshika nyadhifa za uwaziri sasa inakuwaje iwe aibu kwao kugombea? Wewe mwenyewe una uwezo wa kuwazidi hao hadi useme ni aibu? Acheni fitina jamani kila mmoja ana haki katika nchi hii
 
Membe na January ni watanzania wameshika nyadhifa za uwaziri sasa inakuwaje iwe aibu kwao kugombea? Wewe mwenyewe una uwezo wa kuwazidi hao hadi useme ni aibu? Acheni fitina jamani kila mmoja ana haki katika nchi hii

Membe na Makamba ni wana CCM lakini nao ni mafisadi kama alivyokuwa Lowasa.

Wametumiwa ssna na wafadhili wao wa ndani na nje ya Tanzania na sasa wanakazana sana ili waje kurudisha fadhila.

Hali hii haiwezi kutokea tena Tanzania inabidi ninyi baadhi ya watanzania muanze angalau kujisahaulisha kushabikia Ufisadi na mafisadi.
 
Mi naona mngejadili kwa hoja na sio mipasho ili wanajf na wananchi wajue wapi pa kupeleka sapoti.
Na sio kuweka mitazamo yule hamna huyu ndiye bila hoja nukushi
 
Mimi nina chuki na maharamia wote wa taifa hili.wote waliotufanya tuwe hapa tulipo leo.hawa walipaswa kuchomwa moto.walioliibia taifa hili pesa kwa miradi bubu na mikataba ya kimangungo.yaliyotufanya leo hii kisiasa tuwe hapa.

Mafisadi hayo yaliyolea mafisadi yenzao nayachukia na katika hili sina mswalie mtume.i wish wangelipa.kwa mauaji waliyoyafanya,kwa kuumiza wananchi mpaka leo hii.nayachukia matendo yao na chuki yangu ni halisi.siwezi penda uhuni waliofanya.haijalishi dini,rangi,kabila,vyama vyao.nitasimama kama mtanzania.ila hawa nitawasema hawafai.

Huyu jamaa anachuki sana na Kikwete, nilikuwa najua ni great thinker anachambua vitu bila upendeleo ila nimeona anachuki binafsi na watu hasa Kikwete na walio karibu nae andiko lake la juzi limizihisirisha hicho, kiukweli mie nimempuuza
 
Mkuu MTK, tatizo letu ni kuwa hatuna "Non partisan system or institutions". Wakati wa chaguzi au teuzi taasisi hizi zingeweza kusaidia upatikanaji wa "the best and clean candidates" kwenye kila nafasi na hivyo kuondokana na kuwa na watu kwenye nafasi hizo za uongozi wasiokuwa na sifa!
Kinachotokea kwetu hapa ni kuwa "system" inabadilika kila baada ya uchaguzi au uteuzi kiasi cha kwamba ule weledi wao pia umekuwa ni mhanga wa uchaguzi na teuzi hizi. Katika mazingira haya tusitegemee kupata "unbiased vetting" ya watumishi wa umma kwenye ngazi mbali mbali! Tatizo linarekebishika kwa kuibadili katiba ili kuzifanya taasisi hizi ziwajibike kwa Bunge badala ya kuwa chini ya Mamlaka za Uteuzi. Ni mawazo yangu tu.
National nobel prize is for people like you
 
Kila mmoja ana haki lakini si kila mmoja anastahili.wameshika uwaziri sababu ya mfumo mbovu unaoweka mawaziri hao.hata wewe rais akiamua uwe waziri unakuwa.hata akiamua jiwe liwe waziri linakuwa.lakini haimaanishi lina stahili. Tafuteni watu wenye kustahili wawe wagombea wenu.

Membe na January ni watanzania wameshika nyadhifa za uwaziri sasa inakuwaje iwe aibu kwao kugombea? Wewe mwenyewe una uwezo wa kuwazidi hao hadi useme ni aibu? Acheni fitina jamani kila mmoja ana haki katika nchi hii
 
Kwanza tubadilishe katiba ilingane na matakwa ya wananchi wa sasa.Tukiendelea na mfumo wa sasa wa kuifadhi matakwa ya viongozi waliopita,wa leo,na wanaotarajiwa (yaani to maintain status qou)tunajidanganya kuendelea kupalilia ubinafsi,umimi mambo haya yaweza kuzaa ukabila,udini ubaguzi nk We should not ignore peoples views let us share eventually get good governance of beloved country Tanzania.
 
Back
Top Bottom