NeverExisted
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 406
- 619
Eti "tulikosea kwa Kikwete,tukaendelea na makosa hayo kiasi kwamba hayo makosa...." ooh mkuu atukupangii cha kusema lakini si ungesema tu kuwa tulikosea kwa Kikwete na Magufuli...then blah blah! Hao watu hawakuwahi kuwa caliber na kuwa marais. Tuwe wakweli, uwezo wao ni mdogo kwenye maeneo mengi tu..mwingine mtu mzima hajui hata kuwa Kuwait ni kingdom na Sadam Hussein hajawahi kuwa rais wa hiyo nchi! Na kwamba Iraq iko na presidential system. Uwezo wa kutumia lugha mbili zinazotumika serikalini (swahili na kiingereza) upo chini kabisa, english usiseme mpaka mzee wa zaidi ya miaka sabini (Museveni) alibidi asaidie kujibu swali la kolapsheni! Busara na hekima, utulivu wa kimawazo kwenye kufanya maamuzi ni shida..ni mwendo wa kukurupuka na misifa. Nyerere alipenda kujisomea vitabu na majarida mbalimbali ( Newsweek, Washington Post, The economist, African Events, Africa Now) na yeye pia alikuwa ni 'author' na akizungumza tu unaona kabisa huyu ni intellectual...Lakini hawa wa sasa wakizungumza wewe ndio unaona aibu.Rais wa nchi unapiga simu kwenye kituo cha redio halafu unasema unapenda kipindi chao cha shilawadu..kweli shilawadu!Miaka ya nyuma Mtu anayegombea Urais wa Tanzania alikuwa anaangaliwa kwa umakini na kupimwa kwa akili,uwezo,busara na weledi wake.
Miaka hii hali hiyo imebadilika hasa baada ya kuonekana kuwa mtu yeyote anaweza kuwa Rais wa Tanzania ili mradi CCM imeamua.ikasababisha every tom,dick and harry kuwa na that feeling ya kuwa Rais.
Tulikosea kwa kikwete,tukaendelea na makosa hayo kiasi kwamba hayo makosa yamekuwa ni sehemu yetu ya kuchagua marais.tumefikia hatua tunadharauliana kiasi kikubwa sana na kuonana hatuna hata common sense.
Ni aibu kutaka MEMBE awe Rais wa Tanzania. ni aibu kutaka MAKAMBA awe Rais wa Tanzania. Ni dharau sana kwetu wenye utashi na akili timamu.dharau hizi zitaendelea kuna siku watu watakuja sema Bashite au Kibajaji awe Rais wa nchi hii.Matusi makubwa sana.
Sababu tu wanapata vijicent toka kwa watu hawa.unadhan mtu kama malecela anashindwa kupiga debe kuwa bashite awe rais wa nchi hii na akakosa waungaji mkono ndani ya watanzania zaidi ya mil 50?
Lakini hii ndo dharau yenyewe sasa.mtu kama membe uwezo wa kiuongoz hana alibebwa sana na bado alipwaya.Makamba hana akili ya kuwa rais...nyie kuleni pesa zao lakin msije kututukana sisi wenye akili humu JF. TUSHAONA MADHARA YA WATU WALIOBEBWA KWENYE UONGOZI HATUTAKI TENA. waliobebwa hukosa kujiamini,hutaka kuonekana wana nguvu ilhali hawana.hutaka ficha udhaifu wao kwa hali na mali.
Fikieni hatua mtuheshimu hata kidogo.matusi na dharau zenu zimefikia hatua mbaya.kuwa membe awe rais wa tanzania?makamba awe rais wa tanzania?keshokutwa mtasema nani?bashite?kibajaji?muro?
Hizo ni dharau kubwa sana kwa wananchi wa tanzania.najua njaa inaweza mfanya mtu aimbe chorus yoyote atakayopewa lakini basi usiimbe wimbo wa hata kuwatukana wazazi wako sababu ya njaa.