Hii Dharau na Matusi kwa Watanzania mpaka lini? Tukatae kuwa sasa Inatosha

Eti "tulikosea kwa Kikwete,tukaendelea na makosa hayo kiasi kwamba hayo makosa...." ooh mkuu atukupangii cha kusema lakini si ungesema tu kuwa tulikosea kwa Kikwete na Magufuli...then blah blah! Hao watu hawakuwahi kuwa caliber na kuwa marais. Tuwe wakweli, uwezo wao ni mdogo kwenye maeneo mengi tu..mwingine mtu mzima hajui hata kuwa Kuwait ni kingdom na Sadam Hussein hajawahi kuwa rais wa hiyo nchi! Na kwamba Iraq iko na presidential system. Uwezo wa kutumia lugha mbili zinazotumika serikalini (swahili na kiingereza) upo chini kabisa, english usiseme mpaka mzee wa zaidi ya miaka sabini (Museveni) alibidi asaidie kujibu swali la kolapsheni! Busara na hekima, utulivu wa kimawazo kwenye kufanya maamuzi ni shida..ni mwendo wa kukurupuka na misifa. Nyerere alipenda kujisomea vitabu na majarida mbalimbali ( Newsweek, Washington Post, The economist, African Events, Africa Now) na yeye pia alikuwa ni 'author' na akizungumza tu unaona kabisa huyu ni intellectual...Lakini hawa wa sasa wakizungumza wewe ndio unaona aibu.Rais wa nchi unapiga simu kwenye kituo cha redio halafu unasema unapenda kipindi chao cha shilawadu..kweli shilawadu!
 
Nmejaribu kusoma hii thread yangu sijaona kama kuna sehemu namsifia magufuli. Unaposoma tuliza akili usisome kwa macho tu.tumia na akili hata kidogo.sina ninayemsifia na nadhani ni bora kuwa na magufuli kuliko membe au makamba.
Nchi inarudi nyuma kwa kasi sana.. mabenki yanayumba sana kiasi kwa hata reserve zake BOT ziko mashakani... Soko la hisa linapumulia mashine.. hatuna ushirikiano nzuri na mataifa ya nje.. Ubabe usio wa lazima, haki za kujieleza hakuna, kila uchao matamko ya ajabu, UKANDA, mishahara imegota haiongezwi mwaka wa tatu huu... madogo wanakaa tu makambini huku hawana ajira.. Sare za jeshi hakuna tena.. mtu analazimika kwenda kununua mwenyewe kwenye maduka ya jeshi na zinauzwa 50000..
Miradi isiyokuwa na upembuzi yakinifu,
Utekwaji nyara watu kibao..
 
😁😁😁😁.... MEMBE NO WAY. NI BORA KUTOKUWA NA RAIS LAKINI SI MEMBE.


 
Sema wewe mkuu. Yaani vitu vingi vimevurugwa kwa namna ya ovyo kabisa mpaka vitu visivyokuwa na risk kibiashara kama Hatifungani za serikali na zenyewe eti hazihuziki. Si mabenki,ajira, kilimo wala biashara kote ni maumivu, uchumi umedolora haswa na ni kwa sababu ya maamuzi ya hovyo hovyo. Halafu mtu anasema eti bora Jiwe kuliko fulani, huyo fulani hajawahi hata kuwa rais! Sijui unampima vipi?
 
Nyerere alikuwa kiongozi mzuri lakini alituachia kizazi cha hovyo sana kuwahi kutokea.

Mzee mwinyi alikuja akafungua milango ya ufisadi kila sekta ikaanza kutawaliwa na ufisadi hata misingi kidogo aliyokuwa ameijenga mwalimu yeye akaanza kusambaratisha kwa nyundo.

Mzee mkapa kaja kauimarisha ufisadi na kuanza kutunga visheria vya hovyo hovyo vinavyouhalalisha ufisadi ametoka madarakani anaanza kulalamika wakati akiwa madarakani alikuwa na nafasi ya kuyatatua.

Mzee kikwete yeye ndiye kabisa kwenye utawala wake tuliyashuhudia matokeo ya ufisadi na mwendelezo wa taifa kupoteza mwelekeo kwa kila kitu.

Huyu mzee wetu naye hata hatuelewi anatupeleka wapi na yeye hana uhakika hata huko tuendako kama anapajua au hata njia tu ya kufikako. Sasa hivi maendeleo tunayafsiri kwa vitu ilhali wananchi wakiwa dhooful hali.

Tuna wasomi wengi sana ambao wakiwa nje ya mfumo wanapayuka Kweli ila wakiingia kwenye mfumo hata akili zao hupotea kabisa.

Nyerere baba kwanini hukuondoka na watu wako wote tukaanza upya tu ???
 
Ametuachia mijitu inajali matumbo yao tu, inagawa mpaka nyumba za serikali kwa mahawara zao.
 
Ametuachia mijitu inajali matumbo yao tu, inagawa mpaka nyumba za serikali kwa mahawara zao.
Mkuu hatari sana japo wanasema zimwi likujualo halikuli likakwisha hili letu halitujui litatumaliza.
 
Halafu et baadae tunasema ni mapenz ya Mungu
 
Mnafanya masikhara katika mambo ya msingi.yaani siku moja unaamka unasema rais wako ni january makamba?nyie watu mtakuwa ni division 5. Hamwezi kuwa serious hata kidogo.kwa style hii acha sasa tuanze kupiga kampeni dr magufuli aongeze miaka.maana badala ya kutafuta mgombea mwenye akili mnatuletea vilaza wengine

Safi sana, mpe makavu
 
Mkapa alianza vizuri kabla ya kukengeuka na kuanza ifisadi nchi.angeendelea na mwanzo alianza jenga uchumi imara.baadaye akaanza kufanya mambo ya hovyo.bank ya nbc,nyumba za serikali n.k

Kikwete... Huyu jamaa miaka yake yote hakuwah kuumiza kichwa.alikuwa anazunguka tu duniani na kuacha nchi ijiendeshe.yeye akila na walio na visu vikali wakijikatia nyama.huyu aliimaliza nchi na kuwauzia mafisadi.akianzisha miradi bubu ya kupigia pesa.kama mchakato wa katiba.hakustahili kabisa kuwa alipp sasa.

 
Wakuu mbona 2025 bado sana,,,,,,!!!!!!
Ni miaka kumi,,,,,, kama ilivyo ada.
 
Huyu fisadi anakwapua fedha za korosho,anayejenga vitu vya kipuuzi kijijini nae vp?
 
Kinacho nitisha na kuniogopesha wanao mpigia debe Membe kuwa raisi ni vijana wa bavicha. Hii ni hatari sana.
 
sasa mtu sahihi ni Nani? Au huyu wa sasa ambae Kila Siku yeye hajifunzi kutokana na makosa, alianza kuwafokea watu wa sukari, matokeo yake hadi Leo sukari si chini ya Tsh 2500, Jana tena naona anawatisha wafanya biashara, kwamba ni lazima wanunue korosho sio chini ya Tsh 3000, Kama hawawezi serekali itazununua, tunajua nia ni mzuri lakini aproching anayotumia sio mzuri, mfanya biashara una bargain nae sio unamfokea fokea Kama mfanya kazi wako vile.
 
Je unakumbuka ķifo cha huyu aliyesema haya? Hakikuwa cha kawaida! Jihadhari yasije yakakukuta na wewe.
 
Kama hawa kina Makamba unasema hawana akili za kutuongoza unamaanisha ni nani wenye akili ya kutuongoza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…