Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Ama baada ya Salamu hizo za upendo, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Kama Mtanzania Mzalendo kwa nchi yangu (na uzalendo ni pamoja na kuusema ukweli kama ulivyo), nimeona niongelee hii kero ya usafiri wa Mwendokasi (japo nina ukakasi na hilo jina maana kiukweli halisadifu kabisa), hasa hasa nyakati za jioni na asubuhi wakati wa watu kutoka au kwenda kazini, kumekuwa na mrundikano mkubwa sana wa abiria hasa hasa kwenye vitu vikuu vya Gerezani, Kivukoni, Kimara na Mbezi. Hali hii imekuwa ikiwapa tabu sana abiria na walinzi uchwara (mara nyingi wamekuwa wakizidiwa nguvu na abiria) ambao wamewekwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa. Hali hii hupelekea abiria kugombania kuingia ndani huku wakisukumana hatari! Yaani jioni kama una Afya mgogoro, bora tu uangalie aina nyingine ya usafiri na wala usijiangaishe na huo unaoitwa Mwendokasi.
Hadi wakati mwingine unabaki unashangaa kwamba hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinalipwa na kodi zetu havilioni hili au mpaka maafa matokeo ndo wachukue hatua?
Hivi ule utaratibu wa kwamba hadi abiria wawe wengi ndo basi liletwe uliwekwa na nani? Na kama yupo, nathubutu kumwita ni mpumbavu kwa sababu kwanza anahatarisha maisha ya Watanzania na pili, anawachelewesha watu aidha kwenda kujitafutia riziki zao na au kurudi nyumbani mapema kujumuika na familia zao wakiwamo watoto kabla hawajalala.
Maombi yangu kwa serikali pamoja na vyombo vyake:
1. Hebu leo jioni/usiku nendeni wenyewe mkashuhudie hili ninalolisema
2. Shughulikieni kero mtakazozishuhudia
Ahsanteni sana.
Nawapenda nyote.