Hii hali ikiendelea, tutarajie majanga kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka aka Mwendokasi

Usafiri wa umma Dar es salaam ni wa kidhalilishaji.

Watu wanasokomezwa kila kituo mwishowe mnajikuta mnapumuliana visogoni na mgongoni hata ng'ombe wakienda machinjioni hawabanani vile.

Huo mradi wangempa mwekezaji auendeshe, serikali imeshindwa.
Kwakweli !
 
Sahihi, lakini sasa, wingi wa hao watu kwenye jiji unatokana na wingi wa wakazi wa jiji husika sio?

Nigeria ina eneo dogo kidogo kulinganisha na Tanganyika sio? Population yake ni zaidi ya watu 220m ilhali Tanganyika ni 62m.

Lagos pekee ina 16m, na ukubwa wa ardhi ni ndogo kuliko Dar. Huoni hapa kuwa ukifika Lagos lazima ujue mji umezidiwa ukilonganisha na Dar?

Vituo vitakuwa vinafurika kulingana na population ya mji!
Hao mwendokasi wanatumia njia zao kwahiyo hawana foleni kama usafiri mwingine, kwanini wasiongeze mabasi kulingana na mahitaji ??
 
Nikumbushe huduma yoyote ya kijamii unayodhani imekidhi mahitaji ya jamii kwa 100% hapa Tanganyika!
 
Sahihi, lakini sasa, wingi wa hao watu kwenye jiji unatokana na wingi wa wakazi wa jiji husika sio?

Nigeria ina eneo dogo kidogo kulinganisha na Tanganyika sio? Population yake ni zaidi ya watu 220m ilhali Tanganyika ni 62m.

Lagos pekee ina 16m, na ukubwa wa ardhi ni ndogo kuliko Dar. Huoni hapa kuwa ukifika Lagos lazima ujue mji umezidiwa ukilonganisha na Dar?

Vituo vitakuwa vinafurika kulingana na population ya mji!
Acha kamba, aliyekwambia Nigeria ni nchi ndogo kwa Tanganyika nani? ongea mambo ukiwa na data sahihi siyo porojo.
 
kama Abiria ni wengi maana yake biashara hiyo ni nzuri, kwanini wasiongeze mabasi ??!!
Kwanini isiwe huria, kila mwenye kuweza kuingiza gari lake alete?

Maximizing margin ndio lengo! Na monopoly inahakikisha flow ya cash kwa kingpin!

Unadhani tungekuwa na maTanesco ya binafsi, leo Januari angeweza kufanya uhuni wake?
 
Acha kamba, aliyekwambia Nigeria ni nchi ndogo kwa Tanganyika nani? ongea mambo ukiwa na data sahihi siyo porojo.
Acha kamba, aliyekwambia Nigeria ni nchi ndogo kwa Tanganyika nani? ongea mambo ukiwa na data sahihi siyo porojo.
Nigeria is situated in the West African region and lies between longitudes 3 degrees and 14 degrees and latitudes 4 degrees and 14 degrees. It has a land mass of 923,768 sq.km.

Tanganyika ni 945,087 sq.km

Bisha ukiwa na data sahihi, SIYO POROJO
 
Kwanini isiwe huria, kila mwenye kuweza kuingiza gari lake alete?

Maximizing margin ndio lengo! Na monopoly inahakikisha flow ya cash kwa kingpin!

Unadhani tungekuwa na maTanesco ya binafsi, leo Januari angeweza kufanya uhuni wake?
Hapo sasa !
 
Mwendokasi hovyo sana hasa wadada wa posta wale hata wakikuta limejaa wanaingia
Yani unawekewa jungu mbele hapo unabaki kusemaa hiiiiiiih kazi kwer kwer
 
Kweli hii huduma ilipoanzishwa ilizingati ubora na wengi iltupa matumaini ya kuleta mageuzi na ustaarabu wa usafiri wa umma mijini. Wengi tuliamini matumizi ya usafiri binafsi utapungua
 
Kiukwel usafr wa mwendo Kasi jiji dar ni kipengele kwa sasa , Tulipotoka na tulpo sasa ndio mbaya zaid labda tulegemew kuwa mazur Zaid huko mbelen lakn wapi

Kama wew ni kijn unawez jiongz Aya PIKPK ya misele /lakn umakn muhim
 
Usafiri wa umma Dar es salaam ni wa kidhalilishaji.

Watu wanasokomezwa kila kituo mwishowe mnajikuta mnapumuliana visogoni na mgongoni hata ng'ombe wakienda machinjioni hawabanani vile.

Huo mradi wangempa mwekezaji auendeshe, serikali imeshindwa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
kama Abiria ni wengi maana yake biashara hiyo ni nzuri, kwanini wasiongeze mabasi ??!! Hiyo ni kuwadhalilisha watu na hakuna wa kuwasemea mpaka atokee msamaria mwema kwenye social media apaze sauti !! And yet nobody cares about it !!
Labda mpaka tuandamane au tugome kama walivyofanya wafanyabiashara wa Kariakoo ndo serikali itusikilize Mkuu..
Yaani ndo maana mtu mmoja akasema kuishi kwenye nchi maskini kama ya kwetu ni ngumu mara kumi (10x harder) kulinganisha na kuishi kwenye nchi iliyoendelea.
Yaani unalazimika ku-struggle for almost everything!!
 
Kiukwel usafr wa mwendo Kasi jiji dar ni kipengele kwa sasa , Tulipotoka na tulpo sasa ndio mbaya zaid labda tulegemew kuwa mazur Zaid huko mbelen lakn wapi

Kama wew ni kijn unawez jiongz Aya PIKPK ya misele /lakn umakn muhim
Nashukuru sana kwa ushauri Mkuu.
Lakini suala ni kwamba kila mmoja akinunua pikipiki au gari, si ndo mambo yatakuwa changamoto zaidi kwa maana ya foleni, n.k.
Nchi kama Japan, usafiri wa Umma ni wa uhakika na haraka zaidi kulinganisha na usafiri wa binafsi
 
Nikumbushe huduma yoyote ya kijamii unayodhani imekidhi mahitaji ya jamii kwa 100% hapa Tanganyika!
Tunalipa kodi kwa lengo la kuboreshewa huduma Mkuu. Na bahati nzuri au mbaya, Tanzania, kila mtu ni mlipa kodi hadi watoto ambao bado hawajazaliwa wanalipa kodi. So, viongozi wetu wajitahidi pia kutuboreshea huduma za kijamii maana ni haki yetu. Tunastahili huduma bora.
 
Back
Top Bottom