Hii hali ikiendelea, tutarajie majanga kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka aka Mwendokasi

Nashukuru sana kwa majibu yenye matumaini.

Jana jumapili nimepanda basi ambalo kiuhakika ni bovu sana. Linatoka Kivukoni kwenda Mbezi. Zile nguzo za kusapoti abiria wanaosimama ndani ya basi zimelegea mno na nati zimechomoka kimsingi ukaguzi wa mara kwa mara wa koufundi unahitajika ktk mabasi haya.

Pia wale walinzi wa vituo wawe wanafanya routine ndani ya vituo kwani wakati wa msongamano wa abiria pia wezi hujipenyeza na kukwapua mali za abiria wanapokuwa ktk kupanda basi.
Exactly [emoji817] kuna kikundi cha vijana wapo wanne au zaidi Huvizia gari zilizojaa wanaingia kwa pamoja na kumbana mlengwa kwa kumzunguka Kwan mda huo huwez kujidhibiti mfukoni zaidi ya kushikilia juu ili asianguke. wakifanikiwa kumuibia wanapeana kwa style ya ajabu Sana na kushuka kituo kifuatacho. wamejipanga hasa kufanikisha ufedhuli huo.vituo wanavyopenda kukaa ni magomeni mapipa,Fire na Mansese
DART Mwendokasi
 
Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Ama baada ya Salamu hizo za upendo, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Kama Mtanzania Mzalendo kwa nchi yangu (na uzalendo ni pamoja na kuusema ukweli kama ulivyo), nimeona niongelee hii kero ya usafiri wa Mwendokasi (japo nina ukakasi na hilo jina maana kiukweli halisadifu kabisa), hasa hasa nyakati za jioni na asubuhi wakati wa watu kutoka au kwenda kazini, kumekuwa na mrundikano mkubwa sana wa abiria hasa hasa kwenye vitu vikuu vya Gerezani, Kivukoni, Kimara na Mbezi. Hali hii imekuwa ikiwapa tabu sana abiria na walinzi uchwara (mara nyingi wamekuwa wakizidiwa nguvu na abiria) ambao wamewekwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa. Hali hii hupelekea abiria kugombania kuingia ndani huku wakisukumana hatari! Yaani jioni kama una Afya mgogoro, bora tu uangalie aina nyingine ya usafiri na wala usijiangaishe na huo unaoitwa Mwendokasi.

Hadi wakati mwingine unabaki unashangaa kwamba hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinalipwa na kodi zetu havilioni hili au mpaka maafa matokeo ndo wachukue hatua?

Hivi ule utaratibu wa kwamba hadi abiria wawe wengi ndo basi liletwe uliwekwa na nani? Na kama yupo, nathubutu kumwita ni mpumbavu kwa sababu kwanza anahatarisha maisha ya Watanzania na pili, anawachelewesha watu aidha kwenda kujitafutia riziki zao na au kurudi nyumbani mapema kujumuika na familia zao wakiwamo watoto kabla hawajalala.

Maombi yangu kwa serikali pamoja na vyombo vyake:

1. Hebu leo jioni/usiku nendeni wenyewe mkashuhudie hili ninalolisema

2. Shughulikieni kero mtakazozishuhudia

Ahsanteni sana.

Nawapenda nyote.
Dart wabadilike utakuta basi linaondoka tupu kivukoni -kimara likiacha abiria bila sababu,madereva wanajidai sana
 
Hii inaonesha uendeshaji wa mambo yetu ulivyoduni. Lakini tazama tunavyojisifia! Ungetegemea wingi wa abiria iwe baraka na faida kwa mwenye mali ya Mwendkokasi lakini hapana. Hajali. Viongozi wake wakuu ni kama Viongozi wa Benki. Wako ofisini wamevaa suti mithili ya banker. Fikiri siku moja Prof. Sarungi akiwa Waziri wa Afya alipofika sehemu ya ajali ya gari mbaya akaamua kujiunga na madaktari kufanya operesheni! Wa Mwendokasi je hawezi hata kuiga? Pale stesheni ya Fire ambapo ni holding centre na exchange ya wasafiri wengi wa Muhimbili, Kivukoni, Kariakoo hakuna mtu anatoa taarifa abiria wakirundikana pale. Gari zote zinakuja zimejaa hakuna mtu anatoa taarifa kituo kipi kimezidiwa. Usafirishaji gani ambao hauna "feedback mechanism" kwa ajili ya kufanya uamuzi jinsi hali inavyojitokeza? Shule ipi ya usafirishaji abiria wenzetu walisoma? Mwendokasi ilianza vizuri lakini hakuna "consistence"; muda unavyopita tunarudi kule kule tulikotoka, kwenye "ustaarabu" wa ujinga na kutojali wajibu! Tunaaibisha. Hatusafiri tukaona dunia nyingine, siyo Kenya, wanaendeshaje usafiri wa binadamu???
 
Ndugu yangu nashukuru kwa kutambua kuwa tatizo ni uchache wa Mabasi, hatua zinachukuliwa ili kuhakikisha Mabasi yakutosha yanapatikana ili wananchi waendelee kutumia na kufurahia usafiri wa umma kama lengo la kuanzishwa kwa mradi huu lilivyokusudia.
Hamko serious, toka mmeanza kusema mtaongeza mabus ni muda sasa. Lakini badala yake mabus yanazidi kupungua. Mna matatizo yale yale ya miradi yote ya umma kuendeshwa kwa Uduni na hasara. Hakuna mabus yoyote mtaongeza, na hapo ndipo uwezo wenu umefikia mwisho. Namna pekee ya kunusuru huo Mradi ni kupewa mtu binafsi. Nyie ni bure kabisa.
 
Exactly [emoji817] kuna kikundi cha vijana wapo wanne au zaidi Huvizia gari zilizojaa wanaingia kwa pamoja na kumbana mlengwa kwa kumzunguka Kwan mda huo huwez kujidhibiti mfukoni zaidi ya kushikilia juu ili asianguke. wakifanikiwa kumuibia wanapeana kwa style ya ajabu Sana na kushuka kituo kifuatacho. wamejipanga hasa kufanikisha ufedhuli huo.vituo wanavyopenda kukaa ni magomeni mapipa,Fire na Mansese
DART Mwendokasi
Unapokutana na kikundi ama kama una wasiwasi juu ya mwenendo wa abiria fulani tafadhali toa taarifa kwa kutumia namba ya bure ya DART 0800110147 ili askari wetu wapewe taarifa na kufika mara moja katika eneo husika, kwa pamoja tukemee vitendo vya namna hii katika usafiri wa umma.
 
Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Ama baada ya Salamu hizo za upendo, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Kama Mtanzania Mzalendo kwa nchi yangu (na uzalendo ni pamoja na kuusema ukweli kama ulivyo), nimeona niongelee hii kero ya usafiri wa Mwendokasi (japo nina ukakasi na hilo jina maana kiukweli halisadifu kabisa), hasa hasa nyakati za jioni na asubuhi wakati wa watu kutoka au kwenda kazini, kumekuwa na mrundikano mkubwa sana wa abiria hasa hasa kwenye vitu vikuu vya Gerezani, Kivukoni, Kimara na Mbezi. Hali hii imekuwa ikiwapa tabu sana abiria na walinzi uchwara (mara nyingi wamekuwa wakizidiwa nguvu na abiria) ambao wamewekwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa. Hali hii hupelekea abiria kugombania kuingia ndani huku wakisukumana hatari! Yaani jioni kama una Afya mgogoro, bora tu uangalie aina nyingine ya usafiri na wala usijiangaishe na huo unaoitwa Mwendokasi.

Hadi wakati mwingine unabaki unashangaa kwamba hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinalipwa na kodi zetu havilioni hili au mpaka maafa matokeo ndo wachukue hatua?

Hivi ule utaratibu wa kwamba hadi abiria wawe wengi ndo basi liletwe uliwekwa na nani? Na kama yupo, nathubutu kumwita ni mpumbavu kwa sababu kwanza anahatarisha maisha ya Watanzania na pili, anawachelewesha watu aidha kwenda kujitafutia riziki zao na au kurudi nyumbani mapema kujumuika na familia zao wakiwamo watoto kabla hawajalala.

Maombi yangu kwa serikali pamoja na vyombo vyake:

1. Hebu leo jioni/usiku nendeni wenyewe mkashuhudie hili ninalolisema

2. Shughulikieni kero mtakazozishuhudia

Ahsanteni sana.

Nawapenda nyote.
Hii shughuli wangemkabidhi Bakhresa!
 
Hii inaonesha uendeshaji wa mambo yetu ulivyoduni. Lakini tazama tunavyojisifia! Ungetegemea wingi wa abiria iwe baraka na faida kwa mwenye mali ya Mwendkokasi lakini hapana. Hajali. Viongozi wake wakuu ni kama Viongozi wa Benki. Wako ofisini wamevaa suti mithili ya banker. Fikiri siku moja Prof. Sarungi akiwa Waziri wa Afya alipofika sehemu ya ajali ya gari mbaya akaamua kujiunga na madaktari kufanya operesheni! Wa Mwendokasi je hawezi hata kuiga? Pale stesheni ya Fire ambapo ni holding centre na exchange ya wasafiri wengi wa Muhimbili, Kivukoni, Kariakoo hakuna mtu anatoa taarifa abiria wakirundikana pale. Gari zote zinakuja zimejaa hakuna mtu anatoa taarifa kituo kipi kimezidiwa. Usafirishaji gani ambao hauna "feedback mechanism" kwa ajili ya kufanya uamuzi jinsi hali inavyojitokeza? Shule ipi ya usafirishaji abiria wenzetu walisoma? Mwendokasi ilianza vizuri lakini hakuna "consistence"; muda unavyopita tunarudi kule kule tulikotoka, kwenye "ustaarabu" wa ujinga na kutojali wajibu! Tunaaibisha. Hatusafiri tukaona dunia nyingine, siyo Kenya, wanaendeshaje usafiri wa binadamu???
Umeongea vzr sana ndugu yangu.
Kikubwa ndugu zetu wa Mwendokasi wapo na bila shaka watayafanyia kazi mapendekezo haya
 
Unapokutana na kikundi ama kama una wasiwasi juu ya mwenendo wa abiria fulani tafadhali toa taarifa kwa kutumia namba ya bure ya DART 0800110147 ili askari wetu wapewe taarifa na kufika mara moja katika eneo husika, kwa pamoja tukemee vitendo vya namna hii katika usafiri wa umma.
changamoto ni namna ya kuipiga hiyo simu Mkuu, maana unakuta hata kujipapasa wakati mwingine huwezi kabisa kutokana na jinsi huwa mnaturundika kwenye mabasi yenu
 
Hoja ya population haina mashiko ni defensive sana. Nadhani mtoa hoja alilenga uandaliwe utaratibu mzuri wa kutumia usafiri ule na sio 'randomly' kama ilivyo sasa.

Kwani Dar Ina population kubwa kuliko Tokyo yenye watu 28 mil?
Na usafiri wa umma upo, mbona hawagombei?
Kwenye utaratibu mzuri kila kitu huenda vzr.
Shida ya usafiri wetu ni utaratibu mbovu, period.
 
Ukitaka kujionea vizuri nenda kituo cha Gerezani au Fire ,foleni kubwa kusubiri magali likija watu wanajazana hakuna hata nafasi ya kupumua vizuri .

Kuna siku nilipita na kujionea hayo nikajisemaa hii nchi haikosi top ten katika Raia wanaoteseka zaidi duniani.
Well said, tunateseka sana raia wa nchi hii.
Karibia kila kitu tunapambania!
 
Nishawahi kusikia kuwa wanapigiwa simu gari lije kituoni abiria wakijaa, noma sana,haya mabasi ni kero tupu,sijui kwanini waliyaita hivo haha watu wanakaa kituon mpaka wanachelewa kufika makazini/makwao kusubiria mwendo wakobe ufike,yani bora apewe muekezaji tu,abiria wengi bus chache matokeo yake likitokea gonjwa wote mnaugua huko!
Mungu anatupenda sana Watanzania, maana vinginevyo wote ambao huwa tunatumia mwendokasi, tungekuwa tayari ni wagonjwa wa kifua kikuu au magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na msongamano wa watu.
 
Usafiri huu umekuwa kero kuliko hata ule wa daladala!
Kituoni unaka hadi saa 1 bila kupata usafiri!
Zinajaza mno mno hadi karaha!
Mwendokasi wakati mwingine ni usafiri wa wenye nguvu, kama huna nguvu ni shida sana
 
Back
Top Bottom