Hii hali ikiendelea, tutarajie majanga kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka aka Mwendokasi

Nashukuru sana kwa ushauri Mkuu.
Lakini suala ni kwamba kila mmoja akinunua pikipiki au gari, si ndo mambo yatakuwa changamoto zaidi kwa maana ya foleni, n.k.
Nchi kama Japan, usafiri wa Umma ni wa uhakika na haraka zaidi kulinganisha na usafiri wa binafsi
Ata mwanzo mwendo Kasi ulikuja na watu wengi kwakuw waliona unamanufaa kutumia wengin waliuz magari na kupak nyumbn kwakuw waliona atleast huduma inaridhisha lakn kwa sasa hakuna mwenye Gari gari anaetaman kupand mwendo kaz analazmka

So watu watavyo Anza kumilik vyombo vyao wao lazm watie akili Aku kungekuw na wawekezaji wa wawili huu ujinga usingekuwepo kias hiki
 
Yaani kama ni wewe ni mstaarabu, hii Mwendokasi yetu hii huwezi kupanda, maana mara nyingi Principle ya Survival of the fittest ndo huwa ina-apply. Halafu unashangaa sana mtu akiwa anapambana kuingia na akishaingia, utafikiri ni watu wawili tofauti! Mwingine akibahatika kupata nafasi, Analala kabisa na usingizi!
Sasa unabaki kushangaa kwamba yale mapambano ya kuingia ndani ndo yamemsababishia uchovu, au alikuwa anapambana apate kiti ili afidie usingizi ambao aliukosa nyumbani?!!
😁😁😁😁😁
 
Acha kamba, aliyekwambia Nigeria ni nchi ndogo kwa Tanganyika nani? ongea mambo ukiwa na data sahihi siyo porojo.
Kwa ukubwa wa eneo yuko sahihi Mkuu.
Labda kiuchumi, kisiasa na wingi wa watu
 
Umeelezea vyema. Yaani usafiri wa daladala ni bora zaidi kuliko huu wa MWENDOKASI. Natamani CEO wake Dr Mihede akague vituo na mateso wanayopata abiria na baadae ajitafakari.
CEO anajua kila kitu sema yeye akili zake kaziweka kwenye target ya mapato tu,hajali hata Kama wateja wake wanateseka yeye hana habari mradi target yake per day inasoma vizuri!!
 
Kweli hii huduma ilipoanzishwa ilizingati ubora na wengi iltupa matumaini ya kuleta mageuzi na ustaarabu wa usafiri wa umma mijini. Wengi tuliamini matumizi ya usafiri binafsi utapungua
Kweli Mkuu.
Wakati mwingine huwa naona hakukuwa na maana ya abiria kupangishwa mistari endapo kungekuwa na mabasi ya kutosha!
 
Tipo bize na mapokezi ya Mabingwa wa Afrika. Hayo malalamiko yako andika barua Rasmi kupitia Kwa Mjumbe wako, kisha Mtendaji Kata halafu peleka halmashauri
 
CEO anajua kila kitu sema yeye akili zake kaziweka kwenye target ya mapato tu,hajali hata Kama wateja wake wanateseka yeye hana habari mradi target yake per day inasoma vizuri!!
Kweli Mkuu.
Wanaojali zaidi mapato kuliko kuboresha huduma kwa abiria
 
Tipo bize na mapokezi ya Mabingwa wa Afrika. Hayo malalamiko yako andika barua Rasmi kupitia Kwa Mjumbe wako, kisha Mtendaji Kata halafu peleka halmashauri
Waliokufa kiume?!
 
Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Ama baada ya Salamu hizo za upendo, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Kama Mtanzania Mzalendo kwa nchi yangu (na uzalendo ni pamoja na kuusema ukweli kama ulivyo), nimeona niongelee hii kero ya usafiri wa Mwendokasi (japo nina ukakasi na hilo jina maana kiukweli halisadifu kabisa), hasa hasa nyakati za jioni na asubuhi wakati wa watu kutoka au kwenda kazini, kumekuwa na mrundikano mkubwa sana wa abiria hasa hasa kwenye vitu vikuu vya Gerezani, Kivukoni, Kimara na Mbezi. Hali hii imekuwa ikiwapa tabu sana abiria na walinzi uchwara (mara nyingi wamekuwa wakizidiwa nguvu na abiria) ambao wamewekwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa. Hali hii hupelekea abiria kugombania kuingia ndani huku wakisukumana hatari! Yaani jioni kama una Afya mgogoro, bora tu uangalie aina nyingine ya usafiri na wala usijiangaishe na huo unaoitwa Mwendokasi.

Hadi wakati mwingine unabaki unashangaa kwamba hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinalipwa na kodi zetu havilioni hili au mpaka maafa matokeo ndo wachukue hatua?

Hivi ule utaratibu wa kwamba hadi abiria wawe wengi ndo basi liletwe uliwekwa na nani? Na kama yupo, nathubutu kumwita ni mpumbavu kwa sababu kwanza anahatarisha maisha ya Watanzania na pili, anawachelewesha watu aidha kwenda kujitafutia riziki zao na au kurudi nyumbani mapema kujumuika na familia zao wakiwamo watoto kabla hawajalala.

Maombi yangu kwa serikali pamoja na vyombo vyake:

1. Hebu leo jioni/usiku nendeni wenyewe mkashuhudie hili ninalolisema

2. Shughulikieni kero mtakazozishuhudia

Ahsanteni sana.

Nawapenda nyote.
Kutokuwajibika ipasavyo kwa watu fulani fulani, baadae tunaambiwa kubinafsisha ndio itakuwa suluhisho.
 
Mwaka jana nilipanda mwendo kasi hapo Gerezani kwenda Kimara aisee nilipata siti ila ile kujaza ilikua imejaza ni balaa

(Nje ya mada kidogo)kilicho niuma gari ilikua imejaza warembo wengi sana, gari ingepata ajali ingekua hasara kwa taifa.
Ukipanda usafiri wa umma ndo unayaona vizuri maua yaliyo ipamba dunia unaweza usioe maana kila unapogeuka unaona kila demu ni mzuri zaidi ya mwenzake
 
Attachments

  • 016F8D80-22ED-428D-89AD-558A1E5BC972.jpeg
    016F8D80-22ED-428D-89AD-558A1E5BC972.jpeg
    32.9 KB · Views: 1
Wampe mwamba u-CEO?!
Nina imani akipewa ndani ya muda mfupi, mambo yatanyooka
 
Mwaka jana nilipanda mwendo kasi hapo Gerezani kwenda Kimara aisee nilipata siti ila ile kujaza ilikua imejaza ni balaa

(Nje ya mada kidogo)kilicho niuma gari ilikua imejaza warembo wengi sana, gari ingepata ajali ingekua hasara kwa taifa.
Ukipanda usafiri wa umma ndo unayaona vizuri maua yaliyo ipamba dunia unaweza usioe maana kila unapogeuka unaona kila demu ni mzuri zaidi ya mwenzake
😁😁😁😁😁
 
Mzee, ungejitahidi kuweka kwa kifupi sana ili kuepuka mfululizi wa sentensi zisizo na aya wala vituo sahihi.

Hamna unachoweza shauri kwa sasa kikasikika, masikii yao yamejaa NTA, midomo imejaa ASALI.

Pambana ujikwamue wewe binafsi, ndio tulipofika sasa! Ongea shida yako wewe!
Naked truth🪓🪓🪓
 
Back
Top Bottom