Hii hali ikiendelea, tutarajie majanga kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka aka Mwendokasi

Labda mpaka tuandamane au tugome kama walivyofanya wafanyabiashara wa Kariakoo ndo serikali itusikilize Mkuu..
Yaani ndo maana mtu mmoja akasema kuishi kwenye nchi maskini kama ya kwetu ni ngumu mara kumi (10x harder) kulinganisha na kuishi kwenye nchi iliyoendelea.
Yaani unalazimika ku-struggle for almost everything!!
Kweli kabisa !
 
Sahihi, lakini sasa, wingi wa hao watu kwenye jiji unatokana na wingi wa wakazi wa jiji husika sio?

Nigeria ina eneo dogo kidogo kulinganisha na Tanganyika sio? Population yake ni zaidi ya watu 220m ilhali Tanganyika ni 62m.

Lagos pekee ina 16m, na ukubwa wa ardhi ni ndogo kuliko Dar. Huoni hapa kuwa ukifika Lagos lazima ujue mji umezidiwa ukilonganisha na Dar?

Vituo vitakuwa vinafurika kulingana na population ya mji!
Hoja ya population haina mashiko ni defensive sana. Nadhani mtoa hoja alilenga uandaliwe utaratibu mzuri wa kutumia usafiri ule na sio 'randomly' kama ilivyo sasa.

Kwani Dar Ina population kubwa kuliko Tokyo yenye watu 28 mil?
Na usafiri wa umma upo, mbona hawagombei?
 
Hapa Afrika Mashariki, hakuna nchi iliyotuzidi POPULATION wala LAND MASS.

Dar ni kubwa mara 2 na point kwa Nairobi.

Kwenye USTAARABU sasa, Dar bado ina wastaarabu wengi kuliko miji mingi ya nchi zilizotuzunguka, Zanzibar ikiwemo.

Nairobi nilipita na bus nikielekea Mwanza, enzi zile

Ulicholeta ni kitu kipya yeye ameshauri na wewe anzisha ya kwako inayohusu Safari yako, Ukweli ni kwamba Mwendokasi ni kero. Inaondoa maana nzima ya usafiri wa haraka. Yaani mnasubiri mpaka mnachoka harafu mkiwa wengi ndo basi linakuja mnaanza kugombea kama mabasii ya mbagala ya enzi zile
 
Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Ama baada ya Salamu hizo za upendo, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Kama Mtanzania Mzalendo kwa nchi yangu (na uzalendo ni pamoja na kuusema ukweli kama ulivyo), nimeona niongelee hii kero ya usafiri wa Mwendokasi (japo nina ukakasi na hilo jina maana kiukweli halisadifu kabisa), hasa hasa nyakati za jioni na asubuhi wakati wa watu kutoka au kwenda kazini, kumekuwa na mrundikano mkubwa sana wa abiria hasa hasa kwenye vitu vikuu vya Gerezani, Kivukoni, Kimara na Mbezi. Hali hii imekuwa ikiwapa tabu sana abiria na walinzi uchwara (mara nyingi wamekuwa wakizidiwa nguvu na abiria) ambao wamewekwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa. Hali hii hupelekea abiria kugombania kuingia ndani huku wakisukumana hatari! Yaani jioni kama una Afya mgogoro, bora tu uangalie aina nyingine ya usafiri na wala usijiangaishe na huo unaoitwa Mwendokasi.

Hadi wakati mwingine unabaki unashangaa kwamba hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinalipwa na kodi zetu havilioni hili au mpaka maafa matokeo ndo wachukue hatua?

Hivi ule utaratibu wa kwamba hadi abiria wawe wengi ndo basi liletwe uliwekwa na nani? Na kama yupo, nathubutu kumwita ni mpumbavu kwa sababu kwanza anahatarisha maisha ya Watanzania na pili, anawachelewesha watu aidha kwenda kujitafutia riziki zao na au kurudi nyumbani mapema kujumuika na familia zao wakiwamo watoto kabla hawajalala.

Maombi yangu kwa serikali pamoja na vyombo vyake:

1. Hebu leo jioni/usiku nendeni wenyewe mkashuhudie hili ninalolisema

2. Shughulikieni kero mtakazozishuhudia

Ahsanteni sana.

Nawapenda nyote.
Mrudi sasa mikoani kwenu mkaendeleze
 
DART Mwendokasi
 
Solution nzuri na ya haraka ni Kuongeza idadi ya mabasi.
Basi zikiwa nyingi, kila baada ya muda mchache basi inafika kituoni, kupakia na kuondoka.
Itapunguza au kuondoa kabisa mrundikano wa abiria kituoni.

Hii Mtendaji mkuu anaijua.
Sema ndio hivyo akifanya hivyo gharama za uendeshaji zitaongezeka.
Na wao wanataka pesa zaidi kuliko kutoa huduma.
 
Mwendokasi ilikuja kama luxury ila kwasababu ya usimamizi mbovu nayo yamegeuzwa kama yale tuliyoyazoea miaka yote.
 
Nishawahi kusikia kuwa wanapigiwa simu gari lije kituoni abiria wakijaa, noma sana,haya mabasi ni kero tupu,sijui kwanini waliyaita hivo haha watu wanakaa kituon mpaka wanachelewa kufika makazini/makwao kusubiria mwendo wakobe ufike,yani bora apewe muekezaji tu,abiria wengi bus chache matokeo yake likitokea gonjwa wote mnaugua huko!
 
Labda mpaka tuandamane au tugome kama walivyofanya wafanyabiashara wa Kariakoo ndo serikali itusikilize Mkuu..
Yaani ndo maana mtu mmoja akasema kuishi kwenye nchi maskini kama ya kwetu ni ngumu mara kumi (10x harder) kulinganisha na kuishi kwenye nchi iliyoendelea.
Yaani unalazimika ku-struggle for almost everything!!
Mimi personally, nimeshagoma tayari!
 
Ukitaka kujionea vizuri nenda kituo cha Gerezani au Fire ,foleni kubwa kusubiri magali likija watu wanajazana hakuna hata nafasi ya kupumua vizuri .

Kuna siku nilipita na kujionea hayo nikajisemaa hii nchi haikosi top ten katika Raia wanaoteseka zaidi duniani.
 
Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Ama baada ya Salamu hizo za upendo, naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.
Kama Mtanzania Mzalendo kwa nchi yangu (na uzalendo ni pamoja na kuusema ukweli kama ulivyo), nimeona niongelee hii kero ya usafiri wa Mwendokasi (japo nina ukakasi na hilo jina maana kiukweli halisadifu kabisa), hasa hasa nyakati za jioni na asubuhi wakati wa watu kutoka au kwenda kazini, kumekuwa na mrundikano mkubwa sana wa abiria hasa hasa kwenye vitu vikuu vya Gerezani, Kivukoni, Kimara na Mbezi. Hali hii imekuwa ikiwapa tabu sana abiria na walinzi uchwara (mara nyingi wamekuwa wakizidiwa nguvu na abiria) ambao wamewekwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa. Hali hii hupelekea abiria kugombania kuingia ndani huku wakisukumana hatari! Yaani jioni kama una Afya mgogoro, bora tu uangalie aina nyingine ya usafiri na wala usijiangaishe na huo unaoitwa Mwendokasi.

Hadi wakati mwingine unabaki unashangaa kwamba hivi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo vinalipwa na kodi zetu havilioni hili au mpaka maafa matokeo ndo wachukue hatua?

Hivi ule utaratibu wa kwamba hadi abiria wawe wengi ndo basi liletwe uliwekwa na nani? Na kama yupo, nathubutu kumwita ni mpumbavu kwa sababu kwanza anahatarisha maisha ya Watanzania na pili, anawachelewesha watu aidha kwenda kujitafutia riziki zao na au kurudi nyumbani mapema kujumuika na familia zao wakiwamo watoto kabla hawajalala.

Maombi yangu kwa serikali pamoja na vyombo vyake:

1. Hebu leo jioni/usiku nendeni wenyewe mkashuhudie hili ninalolisema

2. Shughulikieni kero mtakazozishuhudia

Ahsanteni sana.

Nawapenda nyote.
Watendaji kazi wa shirika hili wananufaika na matatizo hayo.

Maana haitaki elimu kujuwa kuwa wakati wa pirika peleka mabasi mengi.
Mie kumbukumbu yangu UDA ilikuwa na mfumo huwo kuwa Asubuhi na jioni mabasi huwa mengi na usafiri unakuwa haraka.
wakati wa mchana mabasi hupunguzwa na usafiri unakuwa mdogo.

hii ndio dawa ya yote hayo, lakini kuna manufaa kwa watendaji.

Au magari ya binafsi yapate kazi
 
Mzee, ungejitahidi kuweka kwa kifupi sana ili kuepuka mfululizi wa sentensi zisizo na aya wala vituo sahihi.

Hamna unachoweza shauri kwa sasa kikasikika, masikii yao yamejaa NTA, midomo imejaa ASALI.

Pambana ujikwamue wewe binafsi, ndio tulipofika sasa! Ongea shida yako wewe!
Ndo kilichobaki hicho mkuu kuna watu wameshauri hadi basi wameishiwa kuitwa mashetani na kuusifia hii serikali subiri ajali ikitokea ndo iundwe tume
 
kama Abiria ni wengi maana yake biashara hiyo ni nzuri, kwanini wasiongeze mabasi ??!! Hiyo ni kuwadhalilisha watu na hakuna wa kuwasemea mpaka atokee msamaria mwema kwenye social media apaze sauti !! And yet nobody cares about it !!
Utasikia hayo mambo yalitokea awamu 5 jumba bovu wanarushiwa awamu 6 mama anafanya kazi nzuri
 
Kutokuwajibika ipasavyo kwa watu fulani fulani, baadae tunaambiwa kubinafsisha ndio itakuwa suluhisho.
Kama kila taasisi ni ya kubinaafsishwa kwa kukosa weledi Nathani tungeanza na ikulu ndo ya kwanza
 
Kama vile walifungua uzi huku jamvini sijui umeishia wapi maana tabu ipo pale pale. Hii nchi inaendeshwa kwa mihemuko kwa sababu siku ikitokea la kutokea utawaona viongozi wote mbele ya kamera za televisheni na kila mmoja na tamko lake kuanzia kuanzia diwani, mtendaji kata, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, spika, mawaziri husika wa hii sekta na mwisho atamalizia waziri mkuu. Utasikia serikali itagharamia gharama zote za ...........................................

Hivi hii nchi kwa nini hatujifunzi kuwa kinga ni bora kuliko tiba kama ilivyokuwa zamani japo matukio mengine yanatokea tu ghafla. Hili la mwendokasi limepigiwa kelele sana lakini hakuna kiongozi wa juu hata mmoja anayechukua hatua. Kuna nini nyuma ya huu mradi mbona wakubwa wanaogopa kuchukua hatua stahiki.

Kama mwekezaji kashindwa kuendesha kwanini wasiruhusu washindani wengine au mpaka watanzania wafe siku moja kwenye mwendokasi ndio hatua zitachukuliwa? Angalau wangeuza baadhi ya ruti kwa mwekezaji mwenye uwezo kama Bakhresa. Abood, n.k. halafu wao wabakie na ruti chache wazoweza kuzimudu?

Ni mtizamo tu.
 
Tumepokea maoni yako ndugu mteja wetu, kama tulivyosisitiza awali ni kwamba serikali yenu sikivu ya Mama Samia Suluhu Hassan haijawaacha wala haijafumbia macho kero zenu, ni kweli huduma kwa sasa haiko sawa kutokana na uchache wa Mabasi , siku sio nyingi mtasikia kutoka kwetu hatua zilizofikiwa katika kuongeza idadi ya Mabasi, tunawasihi mvute subra wakati suala hili linafanyiwa kazi.
 
Solution nzuri na ya haraka ni Kuongeza idadi ya mabasi.
Basi zikiwa nyingi, kila baada ya muda mchache basi inafika kituoni, kupakia na kuondoka.
Itapunguza au kuondoa kabisa mrundikano wa abiria kituoni.

Hii Mtendaji mkuu anaijua.
Sema ndio hivyo akifanya hivyo gharama za uendeshaji zitaongezeka.
Na wao wanataka pesa zaidi kuliko kutoa huduma.
Ndugu yangu nashukuru kwa kutambua kuwa tatizo ni uchache wa Mabasi, hatua zinachukuliwa ili kuhakikisha Mabasi yakutosha yanapatikana ili wananchi waendelee kutumia na kufurahia usafiri wa umma kama lengo la kuanzishwa kwa mradi huu lilivyokusudia.
 
Tumepokea maoni yako ndugu mteja wetu, kama tulivyosisitiza awali ni kwamba serikali yenu sikivu ya Mama Samia Suluhu Hassan haijawaacha wala haijafumbia macho kero zenu, ni kweli huduma kwa sasa haiko sawa kutokana na uchache wa Mabasi , siku sio nyingi mtasikia kutoka kwetu hatua zilizofikiwa katika kuongeza idadi ya Mabasi, tunawasihi mvute subra wakati suala hili linafanyiwa kazi.
Nashukuru sana kwa majibu yenye matumaini.

Jana jumapili nimepanda basi ambalo kiuhakika ni bovu sana. Linatoka Kivukoni kwenda Mbezi. Zile nguzo za kusapoti abiria wanaosimama ndani ya basi zimelegea mno na nati zimechomoka kimsingi ukaguzi wa mara kwa mara wa koufundi unahitajika ktk mabasi haya.

Pia wale walinzi wa vituo wawe wanafanya routine ndani ya vituo kwani wakati wa msongamano wa abiria pia wezi hujipenyeza na kukwapua mali za abiria wanapokuwa ktk kupanda basi.
 
Back
Top Bottom