Hii hali ikiendelea, tutarajie majanga kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka aka Mwendokasi

Exactly [emoji817] kuna kikundi cha vijana wapo wanne au zaidi Huvizia gari zilizojaa wanaingia kwa pamoja na kumbana mlengwa kwa kumzunguka Kwan mda huo huwez kujidhibiti mfukoni zaidi ya kushikilia juu ili asianguke. wakifanikiwa kumuibia wanapeana kwa style ya ajabu Sana na kushuka kituo kifuatacho. wamejipanga hasa kufanikisha ufedhuli huo.vituo wanavyopenda kukaa ni magomeni mapipa,Fire na Mansese
DART Mwendokasi
 
Dart wabadilike utakuta basi linaondoka tupu kivukoni -kimara likiacha abiria bila sababu,madereva wanajidai sana
 
Hii inaonesha uendeshaji wa mambo yetu ulivyoduni. Lakini tazama tunavyojisifia! Ungetegemea wingi wa abiria iwe baraka na faida kwa mwenye mali ya Mwendkokasi lakini hapana. Hajali. Viongozi wake wakuu ni kama Viongozi wa Benki. Wako ofisini wamevaa suti mithili ya banker. Fikiri siku moja Prof. Sarungi akiwa Waziri wa Afya alipofika sehemu ya ajali ya gari mbaya akaamua kujiunga na madaktari kufanya operesheni! Wa Mwendokasi je hawezi hata kuiga? Pale stesheni ya Fire ambapo ni holding centre na exchange ya wasafiri wengi wa Muhimbili, Kivukoni, Kariakoo hakuna mtu anatoa taarifa abiria wakirundikana pale. Gari zote zinakuja zimejaa hakuna mtu anatoa taarifa kituo kipi kimezidiwa. Usafirishaji gani ambao hauna "feedback mechanism" kwa ajili ya kufanya uamuzi jinsi hali inavyojitokeza? Shule ipi ya usafirishaji abiria wenzetu walisoma? Mwendokasi ilianza vizuri lakini hakuna "consistence"; muda unavyopita tunarudi kule kule tulikotoka, kwenye "ustaarabu" wa ujinga na kutojali wajibu! Tunaaibisha. Hatusafiri tukaona dunia nyingine, siyo Kenya, wanaendeshaje usafiri wa binadamu???
 
Ndugu yangu nashukuru kwa kutambua kuwa tatizo ni uchache wa Mabasi, hatua zinachukuliwa ili kuhakikisha Mabasi yakutosha yanapatikana ili wananchi waendelee kutumia na kufurahia usafiri wa umma kama lengo la kuanzishwa kwa mradi huu lilivyokusudia.
Hamko serious, toka mmeanza kusema mtaongeza mabus ni muda sasa. Lakini badala yake mabus yanazidi kupungua. Mna matatizo yale yale ya miradi yote ya umma kuendeshwa kwa Uduni na hasara. Hakuna mabus yoyote mtaongeza, na hapo ndipo uwezo wenu umefikia mwisho. Namna pekee ya kunusuru huo Mradi ni kupewa mtu binafsi. Nyie ni bure kabisa.
 
Unapokutana na kikundi ama kama una wasiwasi juu ya mwenendo wa abiria fulani tafadhali toa taarifa kwa kutumia namba ya bure ya DART 0800110147 ili askari wetu wapewe taarifa na kufika mara moja katika eneo husika, kwa pamoja tukemee vitendo vya namna hii katika usafiri wa umma.
 
Hii shughuli wangemkabidhi Bakhresa!
 
Umeongea vzr sana ndugu yangu.
Kikubwa ndugu zetu wa Mwendokasi wapo na bila shaka watayafanyia kazi mapendekezo haya
 
changamoto ni namna ya kuipiga hiyo simu Mkuu, maana unakuta hata kujipapasa wakati mwingine huwezi kabisa kutokana na jinsi huwa mnaturundika kwenye mabasi yenu
 
Kwenye utaratibu mzuri kila kitu huenda vzr.
Shida ya usafiri wetu ni utaratibu mbovu, period.
 
Well said, tunateseka sana raia wa nchi hii.
Karibia kila kitu tunapambania!
 
Mungu anatupenda sana Watanzania, maana vinginevyo wote ambao huwa tunatumia mwendokasi, tungekuwa tayari ni wagonjwa wa kifua kikuu au magonjwa mengine yanayoambukizwa kwa njia ya hewa na msongamano wa watu.
 
Usafiri huu umekuwa kero kuliko hata ule wa daladala!
Kituoni unaka hadi saa 1 bila kupata usafiri!
Zinajaza mno mno hadi karaha!
Mwendokasi wakati mwingine ni usafiri wa wenye nguvu, kama huna nguvu ni shida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…