Kipimo ni chako? Mbona umeambatanisha kimoja bila kuweka na chako kama mlipima wote wawili?
Maana yake unajua kabisa majibu yakitoka hivi ni positive na ikitoka vile ni negative. Ama la, umekibeba mtandaoni na kuja kusumbua watu humu.
Anyway, turudi kwenye uzi.
Kwanza, hongera kwa kujenga tabia ya kupima na kujua hali yako na mwenza wako.
Pili, kipimo hicho kinaitwa Bioline HIV 1/2 3.0 Maalum kwa ajili ya kupima uwepo wa virusi katika damu ya binadamu.
Tatu, endapo kilitumika kikamilifu na kusomwa ndani ya dakika 10-15 kina uwezo wa kutoa majibu sahihi kwa kiasi kikubwa. Haswa kwa uwepo wa virusi (positive), kinatoa majibu kwa usahihi kwa zaidi ya asilimia 90.
Hata hivyo, huenda kikatoa majibu ya kuongopa endapo hakitatumika kikamilifu au kusomwa nje ya muda sahihi. Wanaojipima pia si wataalam sana katika kuitumia, hivyo hutokea mara kadhaa kuleta majibu yenye utata.
Mfano;
Kuna mteja alichukua vipimo anakojua yeye. Akaenda huko na jamaa yake. Wakapima na majibu yalikuja negative. Wakafanya yao, na mwanaume akatangulia kuondoka.
Sasa mwanamke kamaliza kuoga na kujiandaa kuondoka, wakati anajiandaa kuondoka kiherehere kimamtuma tena kukitazama kipimo cha mwenzi wake.
La haula, inaonyesha mistari miwili. Huyo, alikuja kwa ghafla kama aliyechanganyikiwa. Analia kwa sauti ya kujutia, Daktari naomba niokoe, nimeukwaa.
Kumsikiliza anachotaka yeye ni PEP, si kingine. Kachanganyikiwa. Mwenzako yupo wapi? Hata simu hana, kaacha alipopata raha za dunia.
Baadae nilikuja kufahamu, alisoma nje ya muda unaopaswa. 1
Nne, mhusika atapaswa kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Apimwe kwa kipimo tofauti.
Tano, kama kaupata wala asijali. Virusi hivi havitishi na kuogofya sana. Bado ana nafasi ya kutimiza ndoto zake endapo atafuata matumizi sahihi ya dawa na kujikubali.