Hii ina maana gani ni positive au negative?

Hii ina maana gani ni positive au negative?

Kipimo ni chako? Mbona umeambatanisha kimoja bila kuweka na chako kama mlipima wote wawili?

Maana yake unajua kabisa majibu yakitoka hivi ni positive na ikitoka vile ni negative. Ama la, umekibeba mtandaoni na kuja kusumbua watu humu.

Anyway, turudi kwenye uzi.
Kwanza, hongera kwa kujenga tabia ya kupima na kujua hali yako na mwenza wako.

Pili, kipimo hicho kinaitwa Bioline HIV 1/2 3.0 Maalum kwa ajili ya kupima uwepo wa virusi katika damu ya binadamu.

Tatu, endapo kilitumika kikamilifu na kusomwa ndani ya dakika 10-15 kina uwezo wa kutoa majibu sahihi kwa kiasi kikubwa. Haswa kwa uwepo wa virusi (positive), kinatoa majibu kwa usahihi kwa zaidi ya asilimia 90.

Hata hivyo, huenda kikatoa majibu ya kuongopa endapo hakitatumika kikamilifu au kusomwa nje ya muda sahihi. Wanaojipima pia si wataalam sana katika kuitumia, hivyo hutokea mara kadhaa kuleta majibu yenye utata.

Mfano;
Kuna mteja alichukua vipimo anakojua yeye. Akaenda huko na jamaa yake. Wakapima na majibu yalikuja negative. Wakafanya yao, na mwanaume akatangulia kuondoka.

Sasa mwanamke kamaliza kuoga na kujiandaa kuondoka, wakati anajiandaa kuondoka kiherehere kimamtuma tena kukitazama kipimo cha mwenzi wake.

La haula, inaonyesha mistari miwili. Huyo, alikuja kwa ghafla kama aliyechanganyikiwa. Analia kwa sauti ya kujutia, Daktari naomba niokoe, nimeukwaa.

Kumsikiliza anachotaka yeye ni PEP, si kingine. Kachanganyikiwa. Mwenzako yupo wapi? Hata simu hana, kaacha alipopata raha za dunia.

Baadae nilikuja kufahamu, alisoma nje ya muda unaopaswa. 1

Nne, mhusika atapaswa kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Apimwe kwa kipimo tofauti.

Tano, kama kaupata wala asijali. Virusi hivi havitishi na kuogofya sana. Bado ana nafasi ya kutimiza ndoto zake endapo atafuata matumizi sahihi ya dawa na kujikubali.
 
inaonekana ukimwi wa miaka hiyo ulikua wa moto sana sio😃😃🤔
Ukimwi wa miaka ile ulikuwa hatari sana maana hakukuwa na madawa ya kufubaza kama ilivyo sasa.

Ndiyo maana wengi waliopata Ukimwi miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni hawakutoboa kufika walau 2008

Siku hizi unakutana na mrembo Kisu kweli ukiambiwa anao utakataa maana anatumia dawa za kufubaza hivyo vigumu kumtambua kwa macho
 
Fafanua chief, fafanuaaaa!🤣🤣
Kama siku ya kuzwaliwa ilivyo moja, siku ya kufa ni moja.. na siku ya ukimwi huwa ipo moja. Ndio maana unaweza kuta mtu anajaza Shabiby zote kwa alio wahi kuwala ila hana maambuzikizi.. maana yake kuna ile siku yake ya kupata ukimwi alikwepa huo mshale.. somo gumu sana.. hadi uwe na PhD.. ya mambo flani 😅😅😅😅 ila kama umehitimu cuba utapata picha.. huwa ni siku moja tu ( ukihepa hiyo siku ) utausikia kwenye bomba tu
 
Ukimwi wa miaka ile ulikuwa hatari sana maana hakukuwa na madawa ya kufubaza kama ilivyo sasa.

Ndiyo maana wengi waliopata Ukimwi miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni hawakutoboa kufika walau 2008

Siku hizi unakutana na mrembo Kisu kweli ukiambiwa anao utakataa maana anatumia dawa za kufubaza hivyo vigumu kumtambua kwa macho
Kwakweli umakini unahitajika sana 🤦‍♀️🤦‍♀️
 
Haiakisi maana kama mbuzi ana ukimwi yanini kujisumbua na kipimo?
Lakini ndiyo vimekuwa vikitumika miaka na miaka sasa.

Na siku ukiambiwa unao kama haujapewa Ushauri na Nasaha vya kutosha unaweza kujikutana unatamani hata Ujiue wakati huo huo unaanza kuwahesabia Wapenzi Ulionao.

Sijui Cecy, Sijui Anne, Sijui Betty, Siju Amina, sijui Rahma

Yaani utakuwa full stressed 😫 🙌
 
Back
Top Bottom