Kwa sababu hajafanya kosa lolote ametumia haki yake ya kikatiba na kibinadamu tu kujieleza.
Na ingawa hajajieleza vizuri sana, hoja yake ya kimsingi ina mantiki.
Ukiondoa maneno ya shombo yote na dharau zake, hoja yake ya kimsingi ni kupingana na logical fallacy ya "argument from authority" ya kuheshimu sana vyeti, elimu rasmi.
Kimsingi anasema yeye ni salesman mzuri kuliko wasomi wengi waliosomea marketing and sales kwenye elimu rasmi.
Na unaweza kupima hilo kwa kuangalia matokeo ya kazi zake, si kwa kuangalia cheti gani anacho.
Ukimsikiliza unaweza kuona hana elimu rasmi, unaweza kuona kuwa pengine elimu rasmi ingeweza kumsaidia kujieleza vizuri zaidi, kuwa na class, kuondoa maneno ya shombo na kujikita kwenye mada.
Lakini, pengine hayo maneno ya shombo ndiyo branding yake, ndiyo marketing strategy yake.
Juzi nilimkuta dogo mmoja anaangalia movie moja, based on real events, "Confessions of a Cam Girl" inamuonesha binti Mmarekani kakataa kwenda chuo kikuu, anataka kuwa influencer online, anasema Kim Kardashian alifanikiwa bila ya kwenda chuo. Wazazi wake walikuwa wanamsisitiza aende chuo, yeye anasema wazazi wamepitwa na wakati ulimwengu huu watu wanafanya wanachotaka na elimu inapatikana popote, si lazima kwenda chuo.
Sasa labda Dotto Magari naye kashajitafuta kajipata anaona chuo hakina umuhimu kwake yeye anatakiwa kufundisha watu aina mpya ya marketing, hizo degrees za marketing zilizopo vyuoni zote zinakwenda kizamani wakati yeye ndiye anakwenda na marketing ya kileo ya kimtandao, ndiyo maana tunamuongelwa yeye na si msomi wa marketing hapa.
Mimi sipendi maneno controversial ya shombo, na Dotto inawezekana anasumbuliwa na saikolojia ya "Sizitaki Mbichi Hizi". Lakini, najua kuwa hayo maneno ni sehemu ya haki ya mtu ya kujieleza, ni haki yake ya kikatiba na kibinadamu.
Kama wewe ni msomi kweli, unatakiwa kujua uhuru huu na kupuuza maneno haya. Zaidi, unatakiwa kuchukua maneno ya Dotto kama changamoto kwamba elimu inatakiwa kupimwa kwa matokeo yake, na kama kweli Dotto kawashinda wasoni katika kutangaza biashara, basi hao wasomi inawezekana kawashinda kweli, wajitafakari.
Of course inawezekana Dotto ni chawa tu kapanda kwa uchawa na si mpiganaji kihivyo, hapo napo inabidi wasomi wamjibu kwa facts.