Hii kitu ya mabasi yote kuhamia stendi ya Magufuli imeumiza wengi

Vipi wale wa trenii SGR
 
Nchi Hizi za kijamaa zinajenga hizi mnaita stendi Ili kukusanya pesa Sasa Kila mtu akiwa na stendi yake inakuwa Haina maana.

Binafsi sikubaliani na mambo ya stendi Moja,inakera kama ni lazima kuwa na stendi basi ziwe nyingi kulingana na direction ya njia kuu zilivyo.
 
Leo imekuaje
 

Mwisho wa siku hizi tabu zote chanzo ni kukosekana kwa ujenzi unaofuata masterplan...

Wakazi wamejenga holela, wakati serikali inapambana ku centralize huduma zake...wapi na wapi???
 
Mkuu Sasa kuna Abiria atakaeshuka Hapo Magufuli ?
Kwasababu mfano mimi nakaa Sinza siwezi kushuka Magufuli nikiwa na Mizigo nitabski kwenye Bus mpaka Shekilango na Abiria wa Mabibo, Manzese, Magomeni wanafanya hivyo hivyo yani Bus litakua linaingia ndani Stand ya Magufuli na kutoka bila Abiria kutelemka
 
Kaka ujue wengine tunaishi mbali na hata kitu inaitwa usafiri binafsi hatuna 😉 halafu kiswahili swahili tukisafiri ni lazima tubebe watoto na mizigo sasa kuanza kuitafuta Mbezi kwenda kupanda basi hiyo ni shughuli pevu hasaa.

Kiufupi kwa wakazi wa nje ya Mji huu ni mwiba mkali.
 
Yani bus linafananishwa na ndege, Raha sana
 
daah.

Kaka hao wa ndege ungewatoa hapo.
Nao wana haki sista ya kupelekewa huduma karibu kama wa mabasi wanavyotaka.

Wa kigamboni wajengewe uwanja GEZAULOLE ,wa Bagamoyo/Bunju wajengewe Uwanja KEREGE ,Kisarawe/Pugu/Gmboto watatumia huo huo wa KIPAWA

Wa Mbezi beach/GOBA/MADALE/MBEZI kimara wajengewe uwanja MBEZI MSUMI.
 
Mkuu ni bora hizi Kampuni zingejenga ofisi zao yani mfano Aboud atatufe eneo lake ajenge Standi yake ila Serikali iweke Muongozo tu na Sheria za Usalama na Mazingira, yani Tufanye kama Timu za Mipira ya Miguu tu Mfano Azam yeye kachagua kujenga Uwanja wake Chamanzi, Simba kachagua Boko, JKT kachagua Mbweni, Hii itasaidia kuwapa Urahisi Wateja na Kampuni za Ma busi watachagua sehemu nzuri ili Boashara zao ziende na Serikali inatakiwa kuweka Vigezo vya Umbali kutoka Kituo A na Kituo B ili kuepuka Msongamano, mfano Kampuni A inajenga Mwenge, Kampuni B inajenga Manzese, na Kampuni C inajenga Banana Ukonga, kampuni C inajenga Chang'ombe.
 
Chalamila ni mkurupukaji wa hovyo kabisa.

Imagine abiria anayetoka Mwanza na bus, afike Dsm saa saba usiku, atoke Magufuli Stand aende nyumbani Mbagala ambapo bus alilokuja nalo linaenda pia Mbagala kwenye yard yao.

Bus linaenda Mbagala tupu huku abiria akitakiwa kuteremka tena atafute usafiri mwingine wa kumpeleka Mbagala, huku bus alilokuja nalo likienda tupu!.

Chalamila amezidi ujinga.
 
Namimi ndio maana naona hii kitu italeta shida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…