Hii kitu ya mabasi yote kuhamia stendi ya Magufuli imeumiza wengi

Tutasikia matukio mengi humo barabarani hadi tuchoke
Katika harakati za kuitafuta Mbezi.
 
Mkuu kwa hili nasimamia na serikali.
Huwezi ukaweka mabus mitaani kama unahitaji mji kuwa well planed.
Hapo tatizo ni wamiliki wa mabus.wanaleta ugumu kwa abiria wao.
Serikali imekataza mabus makubwa kushusha au kupakia abiria mitaani.,hili sio tatizo kwa abiria ila nintatizo kwa wamiliki.
Wamiliki wanatakiwa wawe na mini bus ambazo zitakuwa zinawabeba abiria toka huko mitaani na kuwapeleka Magufuli terminal,, nadhani hili ndy tatizo kwao kwenye hili.
Mubus yote yaanze main terminal.
Huu ndy utaratibu inchi nyingi africa.
Zambia lusaka wana inter city bus terminal.
Zimbabwe Harare wana Road Port.
Pretoria south Africa wana Bosman bus station.
Joberg wana Park station..
Durban wana Durban station..
Daresalam tuna Magufuli bus terminal..
Kwann hatulitaki hili?

Kote huko Buses zina kuwa na ofisi na yard zao mitaani ila kupakia ni main bus terminal tu..
Na hakuna malalamiko yeyote.
 
Hawa watu sijui kama wanafikiria vizuri Dar sio sawa na mwanza au mbeya. Dar kuna watu zaidi ya milioni 5 barabara zimejaa mafoleni kutegemea stendi moja sio sawa. Wanajiangalia wao tu wapate mapato hawaangalii usumbufu watakaopata wananchi
 
Bongo siasa nyingi,stendi yenyewe inaitwa magufuli hizo nchi zingine ulizotaja hawana huo ujinga
 
Kwa dar unakaa sehemu Gani na ukienda mkoani hua unapandia wapi bus?
 
Hawa watu sijui kama wanafikiria vizuri Dar sio sawa na mwanza au mbeya. Dar kuna watu zaidi ya milioni 5 barabara zimejaa mafoleni kutegemea stendi moja sio sawa. Wanajiangalia wao tu wapate mapato hawaangalii usumbufu watakaopata wananchi
Mbona ndege unafika masaa nanne kabla ya safari?
Unapaswa ujipange siku ya safari..
 
Acha uongo, hakuna watu walikataa kuhamia digital, halafu TV sio huduma ya lazima kuwa nayo.
Sawa ,sipo kwa ajili ya kubisha mkuu.

Mijadala kibao ilikuwepo online watu kupinga kuhamia Digital.
 
we unasafuri weka bajeti zako za kufata gari stendi
 
wewe utakuwa ni mpiga debe wa pale Magufuli stand ama utakuwa ni mlinzi wa wanaofaidika na mapato ya pale getini
Hahaaa Daaaah ,mimi nipo Minjingu porini napiga mishe za kuchoma mkaa ,sina interest yeyote na mabasi kwenda kupaki MAGUFULI terminal...Si mtumiaji wa usafiri huo ,nikitaka kwenda Town natumia magari ya mkaa au Fuso zinazopakia mazao.

Nipo kwenye kundi sogozi moja ambalo kila siku wanapost Mabus/Malori yanaua raia/bodaboda kwa road ,hapo ndipo nakazia kwamba tukiondoa hayo malori/mabasi town/vichochoroni tutaokoa vifo vingi sana.

Shadeeya mpaka J3 tunaenda kwenye ule uzi kuulizia MAOKOTO 🙂 🙂
 
Umeshamfikiria mtu anayekaa chanika, gezaulole au tuangoma na anataka kusafiri kwenda mwanza ua arusha
Suluhu ya hiyo siyo kwenda kupakia abiria kwenye uchochoro na kupita uraiani kwa kasi na kuua watu ,vyombo vinaanzia safari uchochoroni bila kukaguliwa na Vehicle inspector.

Solution ni kujenga terminal nyingi kila Side ya majiji tusitegemee terminal moja tu ila ni Muhimu mabasi kuanzia TERMINAL.
 
Swali la kujiuliza mbona hii kitu imekomaliwa Sana!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…