Hii Mikopo ya Bajaji sasa imekua kama kausha damu, tuwe makini

Ukitapeliwa ni tamaa zako zimekupeleka huko wewe unataka serikali ikufungie ndani usiende kwa matapeli?
Ni kama kusema serikali izuie watu kufanya ngono maana watapata ukimwi
 
acha wakope tu maana serikali haina mpango na raia wake, kila mtu ajipambanie mwenyewe...serikali haiwezi kopesha wala haiwezi simamia hii mikopo umiza kwa raia wake....Acha wakope waendelee kumuomba Mungu awasaidie ktk maisha yao ya hapa duniani
 
Hata kama wanatengeneza wenyewe hiyo hela ni kubwa sana hapo unaingia kwenye kitanzi cha wazi wazi. Kwanza huo ni zaidi ya wizi na unyanyasaji wa kiuchumi
 
Kwa mkataba huu ata mke anatoka speed Mungu tusimamie
 
Ni kama ile mikopo ya simu

Kausha damu ya mswahili hasa
 
Hawa pamoja na wanao nunua simu za mikopo akili zao zina fanana
Kuna jirani yangu mdada siku natoka job namuona duka la simu za mikopo anafuraha huyo anapiga picha ya selfie na muuzaji ( katika ununuaji wa simu za mkopo moja ya kipengele muhimu cha kupewa tambo ni lazima upige picha ya selfie na muuzaji kwa ushahidi)

Moyoni nikasema wololoyaeeeee hata mwezi haukuisha namuona na kitochi chake safi tu anadunda mchezo umemshinda.

Nb hivi vitu vya mkopo ukituliza akili utajikuta unavinunua kwa bei ya mara mbili mpaka tatu yake ni bora mtu awekeze kidogo kidogo dukani mpaka ikitimia achukue tambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…