Hii Mikopo ya Bajaji sasa imekua kama kausha damu, tuwe makini

Hapo ulikuwa unategwa wewe ila bora ulivyoshtuka.
 
Hongera kwa uthubutu, vipi kuhusu kijiwe ulichopo kwa siku unalaza kiasi gani baada ya makato yote. Nahitaji kuingia kwenye hiyo sekta kama huto jali naomba unitafutie hiyo chombo namba D iliyo simama.
 
Mwambieni Mama samia awakopeshe bure bila riba...yaani ukae na hela ya mtu miaka miwili unataka irudi kama ilivyo ? Hapo nusu ya hizo bajaj zitapotea kimazingira sababu ya utapeli wa watanzania halafu zilizobakia ndio faida
 
Mkuu mm nilifika ofisini kwao hicho nilichoandika kwenye bandiko sijaongeza chumvi ni kile nilichoanbiwa na mtoa huduma na nilikuta jamaa wanalipa huku wakidai hiyo hesabu inawezekana kwa siku
Sina lengo la kuwaharuibia biashara hawa jamaa
Mkuu achana nao usiwasanue sana, Mtu m bishi muacha hvo hvo, si ipendi riba hata chembe, maana yake hyo bajaji within 2 years iyo bajaji isha choka na kuchoka, itabidi uanze ku weka sawa, it's too bitter, maana hiyo bajaji lazima iende mwendo wa ngiri,
 
Hongera kwa uthubutu, vipi kuhusu kijiwe ulichopo kwa siku unalaza kiasi gani baada ya makato yote. Nahitaji kuingia kwenye hiyo sekta kama huto jali naomba unitafutie hiyo chombo namba D iliyo simama.
Kijiwe siyo kizuri. Kikubwa nimejiunga Bolt na Farasi.

Ila pia ninafanya research ya vijiwe venye hela.
 
Ukifikiria vizuri utagundua hao jamaa wanao toa bajaji wanasaidia sana.

Mtaani kuna kampuni zinatoa mikopo kwa riba ya 10 to 40% kwa Mwezi

Lakini ukipiga hesabu vizuri hao jamaa ni kama wamekupa mkopo kwa riba ya 5% Kwa Mwezi

Lakini pia wamekupa na idea ya biashara ambayo ni Bajaji.

UKWELI MCHUNGU

Nawasilisha povu ruksa.
 
Eeh wadanganye hivyo hivyo,Bajaj yenyewe ni RE hiyo mpaka anamaliza huu utumwa haitakaa miaka miwili haijafa

Nikuulize,dereva akipitisha siku mbili hajaleta hesabu huwa anachukuliwa hatua gani?faida ya kwanza ya boss wa mtaani anasomesheka kwamba hesabu leo amepelekea mwanae mgonjwa hospital sasa kwenye kampuni athubutu kufanya hivyo aone.
 
Eeh wadanganye hivyo hivyo,Bajaj yenyewe na RE hiyo mpaka anamaliza huu utumwa haitakaa miaka miwili haijafa

Nikuulize,dereva akipitisha siku mbili hajaleta hesabu huwa anachukuliwa hatua gani?faida ya kwanza ya boss wa mtaani anasomesheka kwamba hesabu leo amepelekea mwanae mgonjwa hospital sasa kwenye kampuni athubutu kufanya hivyo aone.
 
Ajira hazipo, tufanyeje?

Kukaa bila kazi hatuwezi...
Ajira za nini? Nchi ina kila raslimali. N uongozi tu mbovu. Piganeni muwe na viongozi wazuri kwanza na msiache viongozi au chama kitawale muda mrefu. Kuwe na mashindano. Bajaji siyo suluhisho kwani kila siku zinazidi kuingia mpya mtaani na wateja hawaongezeki kwa kasi. Itafika kipindi bajaji haitaingiza hata elfu 5 kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…