Ndg yangu mtoa post! Nimeisoma post yako kidogo tu nikajua unakoelekea! Jibu la hoja yako ni dogo tu " Acha kazi hizo unazofanya zenye ujira mdogo" sheria yetu ipo wazi inaruhusu tu na wewe kuzamia humo mjengoni! Vinginevyo utaendelea kushangaa na kulalamika!
Sijui kama ulifikiri vizuri kabla ya kutoa/kuandika wazo hili...
Maana yako ni kwamba;
å Walimu wote waache kazi zao "wazamie" huko unakokuita "mjengoni"....., right?
å Madaktari, manesi na wahudumu wa afya waache kazi zenye malipo na mafao kiduchu "wazamie kiduchu",.... right?
å Polisi waache kazi zao za kulinda usalama wako wewe RAIA na kigari chako hicho mtumba " wazamie mjengoni"....., right?
å Wamachingaz, mamantieliz, wauza nyanya magengeni nk nk waache shughuli zao hizo wote "wazamie mjengoni" wafuate malipo na mafao makubwa, ...right?
## Mjengo unawahitaji watu 370 tu. Watanzania tupo almost milioni 60. Wote "tuzamie mjengoni" mkubwa? Uko serious kweli wewe kushiriki mjadala huu? Au unaleta utani hapa?
## Sasa hawa wote wakiacha na wazamie kwa umoja wao huko mjengoni unadhani maisha yatakuwaje? Nani atafunga vidonda vyako hospitalini? Nani afundishe watoto wako shuleni?
## Tunaishi kwa kutegemeana. Tunahitaji serikali. Tunahitaji Binge/wabunge. Tunahitaji walimu. Tunahitaji manesi. Tunahitaji polisi. Tunahitaji machingaz, wauza nyanya magengeni, maduka, nk nk
¶ Ndiyo maana nimekushangaa kuwa labda hujafikiri vizuri kabla ya kuandika...
¶ What is being discussed here, is a real problem dude. Wapo watu maelfu wanaumia. Tuna serikali. Tuna Rais. Tuna vyombo vya maamuzi kwa niaba ya wananchi kama bunge. Lakini hawafanyi kazi yao....
¶ Badala yake they are all selfish; Rais, wabunge, mahakama na wengine wote wenye "nguvu ya maamuzi" ya kubadilisha hali yoyote....
¶ Wanajitazama wao tu huku raia wengine wakitaabika kwa kukosekana mtu kiongozi mmoja tu mpenda HAKI na USAWA na anayejali na atoe kauli tu yenye mamlaka na kuokoa watu walio kwenye taabu na shida...!
¶ Maana ya kuwepo kwa wafalme au watawala na kuunda serikali zao ktk mataifa mbalimbali duniani ni ili ku - regulate mambo haya, kuleta HAKI na USAWA miongoni mwa makundi yote....
¶ Hatusemi kuwa binadamu anaweza kufanya mambo kwa ukamilifu na usahihi kwa 100%. HAPANA...
¶ Kiasili binadamu ni mbinafsi, hata hivyo Tanzania yetu mambo haya ni TOO MUCH maana mpaka nahodha anatawaliwa na roho ile ile hatari ya UBINAFSI.....
NB: Soma post za watu uone jinsi ambavyo wengi wameguswa na jambo hili. Kuna mama mmoja nasikia tangu mwaka 2018 hajalipwa mafao yake pengine hata hayazidi milioni 50 na ni mgonjwa anaelekea hata kufa kwa stress...!