GUI1
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 4,007
- 5,290
Aisee ni wapi nimesema haya unayo uliza?Kwa nini nikimbie? Kwa hiyo ulitaka Mwalimu na Mbunge wawe na kipato sawa? Ni wapi hilo linafanyika labda?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee ni wapi nimesema haya unayo uliza?Kwa nini nikimbie? Kwa hiyo ulitaka Mwalimu na Mbunge wawe na kipato sawa? Ni wapi hilo linafanyika labda?
Angepokea kima cha chini angalau laki 8, sasa wewe 20m unasema umepunguza wakati mwingine anapokea laki 2 miaka 5???Unataka kusema aliposema ameshusha mshahara wake ilikuwa danganya toto?
Ndg yangu mtoa post! Nimeisoma post yako kidogo tu nikajua unakoelekea! Jibu la hoja yako ni dogo tu " Acha kazi hizo unazofanya zenye ujira mdogo" sheria yetu ipo wazi inaruhusu tu na wewe kuzamia humo mjengoni! Vinginevyo utaendelea kushangaa na kulalamika!
Mtu yupo bungeni vipindi 4-6 na kila kipindi analipwa pension, hii haki kweli? Ndiyo maana wataalamu wanaacha kazi zao wanaenda kupasha mikono na kusinzia hovyo hovyoIngetungwa sheria kuwa mbunge ukichukua tu mafao marufuku tena kugombea ubunge maishani mwako.Chukua pensheni baada ya kujiridhisha kuwa hurudi tena katika siasa.Sasa mtu kila miaka mitano anakula pensheni hii sio poa
Madaraja lazima yawepo. Hatuwezi kuwa sawa
Hii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi.
Tumesikia wimbo huu wa kinafiki kuwa, Rais John Pombe Magufuli ni Rais na kiongozi wa wanyonge, wananchi wa hali ya chini.
Si kweli, ni uongo mtupu na ni propaganda za kisiasa tu kwa ajili ya wapambe na wanafiki wachache wanaomzunguka huku uhalisia wa mambo ukiwa tofauti.
Mfano wa kuthibitisha hili ni huu;
Bunge limevunjwa juzi tarehe 16/6/2020. Hawa wabunge lililovunjwa juzi wameingia kazini mwaka 2015. Wamefanya kazi yao miaka mitano (5) tu toka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020.
Inasemekana mafao ya kiinua mgongo kwa miaka mitano tu kila mmoja ni zaidi ya Tshs. 250,000,000.
Na inasemekana wakati Rais Magufuli (eti Rais wa wanyonge) anahutubia ndani hiyo juzi kulivunja bunge hilo, tayari mzigo wa fedha wa kila mbunge ulishaingia kwenye Bank Account yake.
Hebu tazama upande wa pili wa wanyonge halisi kinachotokea.
Huko Sengerema (na naamini kwingine kote Tanzania nzima), yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi. Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 75,000,0000 hivi.
Kinacholeta shida ni kuwa, tangu huyu mwalimu masikini astaafu kwa mujibu wa sheria mwezi january hadi Juni hii mwaka huu, 2020 (miezi 6 sasa) bado anasotea mafao yake haya kidogo, hajalipwa.
Sasa swali la kujiuliza ni hili;
Kati ya wabunge hawa ambao bunge linavunjwa leo huku mafao yao yakiwa yaneshalipwa jana na huyu mwalimu ambaye kastaafu miezi sita (6) iliyopita na bado hajalipwa vijisenti vyake vya mafao, ni nani hasa mnyonge?
Na huu usawa katika nchi hii uko wapi? Iweje mbunge aliyefanya kazi miaka mitano tu alipwe mafao ya kiinua mgongo kikubwa hivyo kwa takribani mara tano ya mwalimu ama nesi ama daktari aliyefanya kazi kwa miaka 35?
Huyu mtetezi wa wanyonge (Bwana Magufuli) anatetea wanyonge na unyonge upi hasa?
Mimi nasema Tanzania haina kiongozi Rais mtetezi wa wanyonge. Haijapata na hakuna kizuri wala kiongozi mzuri atakayetokana na CCM ili kubadilisha hali hii na kuleta tofauti na usawa.
Sahihi kabisa kiongoziJiwe nae ni wale wale tu wanamtukuza tu lakini nae hana lolote mnafiki tu. THE BEAUTIFUL ONES ARE NOT YET BORN
Kazi yao ni kutukuza tuNdugu mchawi wa Afrika ni waafrika wenyewe
Unaongelea miezi sita ? Kuna wengine wana mwaka wanafatalia hawajalipwa
Nitajie nchi iliyo na usawa kati ya Wanasiasa na watu wa kawaida, ...
Bunge lina umuhimu wake sana, tatizo ni pale linapogeuzwa kuwa kikao cha chama, na kudumisha kila fikra ya mwenyekiti!!!Mimi kusema kweli sionagi umuhimu wa wabunge.
My point of view.
Mtoa mada unataka usawa na wakati mpaka sasa mhusika mkuu anapiga kelele majukwaani na kwenye mikutano yake ya kuwataka wananchi wawe Wazalendo kwa kulipa kodi! lakini katika hali isiyo ya kawaida, kuna tetesi ya kwamba yeye mwenyewe mshahara wake eti haukatwi kabisa hiyo kodi!
Awamu hii imetuamsha wengi. Kutokana na kutamalaki kwa unafiki na ubinafsi, ni wakati sasa na sisi kujiongeza ili siku moja watoto wetu wasije kuyalaani makaburi yetu.
Kwani nimekulazimisha kunijibu? Ondoa jazba kama mtoto, ...
Wanatetea matumbo yao, ukitaka kujua wanavyo tetea maslahi yao waguswe wao pension ipunguzwe utawasikia hapo!hata wabunge wetu wameshindwa kabisa kuwa watetezi wa wapiga kura wao! ni vyema wafanyakazi wote wakaungana na kutowapa ubunge wanaogombea kwa awamu ingine. tuwape wapya na tuwape jukumu la kwenda kupigania haki za wafanyakazi wanaoteseka.