Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Hii nchi haina usawa: Mbunge miaka mitano, mafao zaidi ya Tshs. 200M, mwalimu miaka 32 kazini, mafao Tshs. 70M, miezi sita hajalipwa

Mtoa mada unataka usawa na wakati mpaka sasa mhusika mkuu anapiga kelele majukwaani na kwenye mikutano yake ya kuwataka wananchi wawe Wazalendo kwa kulipa kodi! lakini katika hali isiyo ya kawaida, kuna tetesi ya kwamba yeye mwenyewe mshahara wake eti haukatwi kabisa hiyo kodi!

Awamu hii imetuamsha wengi. Kutokana na kutamalaki kwa unafiki na ubinafsi, ni wakati sasa na sisi kujiongeza ili siku moja watoto wetu wasije kuyalaani makaburi yetu.
 
Kuna clip moja huwa naiona Star TV inasema baada ya SHETANI KUINGIA MOTONI ATAKAYE FUATA NI MWANASIASA huwa namwelewa sana.
 
Unataka kusema aliposema ameshusha mshahara wake ilikuwa danganya toto?
Angepokea kima cha chini angalau laki 8, sasa wewe 20m unasema umepunguza wakati mwingine anapokea laki 2 miaka 5???
 
Ndg yangu mtoa post! Nimeisoma post yako kidogo tu nikajua unakoelekea! Jibu la hoja yako ni dogo tu " Acha kazi hizo unazofanya zenye ujira mdogo" sheria yetu ipo wazi inaruhusu tu na wewe kuzamia humo mjengoni! Vinginevyo utaendelea kushangaa na kulalamika!

Sijui kama ulifikiri vizuri kabla ya kutoa/kuandika wazo hili...

Maana yako ni kwamba;

å Walimu wote waache kazi zao "wazamie" huko unakokuita "mjengoni"....., right?

å Madaktari, manesi na wahudumu wa afya waache kazi zenye malipo na mafao kiduchu "wazamie kiduchu",.... right?

å Polisi waache kazi zao za kulinda usalama wako wewe RAIA na kigari chako hicho mtumba " wazamie mjengoni"....., right?

å Wamachingaz, mamantieliz, wauza nyanya magengeni nk nk waache shughuli zao hizo wote "wazamie mjengoni" wafuate malipo na mafao makubwa, ...right?

## Mjengo unawahitaji watu 370 tu. Watanzania tupo almost milioni 60. Wote "tuzamie mjengoni" mkubwa? Uko serious kweli wewe kushiriki mjadala huu? Au unaleta utani hapa?

## Sasa hawa wote wakiacha na wazamie kwa umoja wao huko mjengoni unadhani maisha yatakuwaje? Nani atafunga vidonda vyako hospitalini? Nani afundishe watoto wako shuleni?

## Tunaishi kwa kutegemeana. Tunahitaji serikali. Tunahitaji Binge/wabunge. Tunahitaji walimu. Tunahitaji manesi. Tunahitaji polisi. Tunahitaji machingaz, wauza nyanya magengeni, maduka, nk nk

¶ Ndiyo maana nimekushangaa kuwa labda hujafikiri vizuri kabla ya kuandika...

¶ What is being discussed here, is a real problem dude. Wapo watu maelfu wanaumia. Tuna serikali. Tuna Rais. Tuna vyombo vya maamuzi kwa niaba ya wananchi kama bunge. Lakini hawafanyi kazi yao....

¶ Badala yake they are all selfish; Rais, wabunge, mahakama na wengine wote wenye "nguvu ya maamuzi" ya kubadilisha hali yoyote....

¶ Wanajitazama wao tu huku raia wengine wakitaabika kwa kukosekana mtu kiongozi mmoja tu mpenda HAKI na USAWA na anayejali na atoe kauli tu yenye mamlaka na kuokoa watu walio kwenye taabu na shida...!

¶ Maana ya kuwepo kwa wafalme au watawala na kuunda serikali zao ktk mataifa mbalimbali duniani ni ili ku - regulate mambo haya, kuleta HAKI na USAWA miongoni mwa makundi yote....

¶ Hatusemi kuwa binadamu anaweza kufanya mambo kwa ukamilifu na usahihi kwa 100%. HAPANA...

¶ Kiasili binadamu ni mbinafsi, hata hivyo Tanzania yetu mambo haya ni TOO MUCH maana mpaka nahodha anatawaliwa na roho ile ile hatari ya UBINAFSI.....

NB: Soma post za watu uone jinsi ambavyo wengi wameguswa na jambo hili. Kuna mama mmoja nasikia tangu mwaka 2018 hajalipwa mafao yake pengine hata hayazidi milioni 50 na ni mgonjwa anaelekea hata kufa kwa stress...!
 
Ingetungwa sheria kuwa mbunge ukichukua tu mafao marufuku tena kugombea ubunge maishani mwako.Chukua pensheni baada ya kujiridhisha kuwa hurudi tena katika siasa.Sasa mtu kila miaka mitano anakula pensheni hii sio poa
Mtu yupo bungeni vipindi 4-6 na kila kipindi analipwa pension, hii haki kweli? Ndiyo maana wataalamu wanaacha kazi zao wanaenda kupasha mikono na kusinzia hovyo hovyo
 
hata wabunge wetu wameshindwa kabisa kuwa watetezi wa wapiga kura wao! ni vyema wafanyakazi wote wakaungana na kutowapa ubunge wanaogombea kwa awamu ingine. tuwape wapya na tuwape jukumu la kwenda kupigania haki za wafanyakazi wanaoteseka.
 
Madaraja lazima yawepo. Hatuwezi kuwa sawa

Ni kweli, hilo haliepukiki....But not to this extent....

Hutuongelei usawa wa wote tuwe wabunge au mawaziri ama Marais kwa wakati mmoja. HAPANA...!!

Sawa wewe mbunge FIRST CLASS au DARAJA "A", kwa miaka mi5 tu ya utumishi una mafao ya Tshs. 230,000,000

Mwalimu ama nesi ama Daktari " THIRD CLASS" ama "DARAJA " C", miaka 32 ya Utumishi wa umma huohuo, mafao yake Tshs. 75,000,000...

å Kwanini hawa RAIA DARAJA LA KWANZA (wabunge, mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi, RCs, DCs nk) mafao makubwa milioni 1000, 900, 500, 230 na wanajilipa haraka haraka kabla hata kustaafu rasmi??

å Kwanini sisi RAIA DARAJA LA TATU (walimu, manesi, polisi, madaktari, nk nk) miaka 38, 35,32, ama 25 ya utumishi, mafao milioni 80, 70, 50, 15, 10 na hata 5 lakini inachukua miaka, miezi kadhaa kulipwa? Why? Why?

Usawa tunaoutaka kwa steji hii ni kila mtu kwa kiwango chake kikubwa au kidogo akipate kwa wakati huo huo unaotakiwa...!!
 
Alafu utasikia wanakwambia kuwa binadamu wote ni sawa
Hii nchi haina usawa. Hii nchi haijapata kiongozi wa kuleta usawa ingalau kwa nusu tu miongoni mwa wananchi.

Tumesikia wimbo huu wa kinafiki kuwa, Rais John Pombe Magufuli ni Rais na kiongozi wa wanyonge, wananchi wa hali ya chini.

Si kweli, ni uongo mtupu na ni propaganda za kisiasa tu kwa ajili ya wapambe na wanafiki wachache wanaomzunguka huku uhalisia wa mambo ukiwa tofauti.

Mfano wa kuthibitisha hili ni huu;

Bunge limevunjwa juzi tarehe 16/6/2020. Hawa wabunge lililovunjwa juzi wameingia kazini mwaka 2015. Wamefanya kazi yao miaka mitano (5) tu toka mwaka 2015 hadi mwaka huu 2020.

Inasemekana mafao ya kiinua mgongo kwa miaka mitano tu kila mmoja ni zaidi ya Tshs. 250,000,000.

Na inasemekana wakati Rais Magufuli (eti Rais wa wanyonge) anahutubia ndani hiyo juzi kulivunja bunge hilo, tayari mzigo wa fedha wa kila mbunge ulishaingia kwenye Bank Account yake.

Hebu tazama upande wa pili wa wanyonge halisi kinachotokea.

Huko Sengerema (na naamini kwingine kote Tanzania nzima), yupo mwalimu aliyefanya kazi miaka 32 (1988 - 2020) kwa taabu na shida nyingi. Amestaafu tangu mwezi Januari, 2020. Baada ya kukokotolewa kwa mafao yake ya mkupuo atapata kama Tshs. 75,000,0000 hivi.

Kinacholeta shida ni kuwa, tangu huyu mwalimu masikini astaafu kwa mujibu wa sheria mwezi january hadi Juni hii mwaka huu, 2020 (miezi 6 sasa) bado anasotea mafao yake haya kidogo, hajalipwa.

Sasa swali la kujiuliza ni hili;

Kati ya wabunge hawa ambao bunge linavunjwa leo huku mafao yao yakiwa yaneshalipwa jana na huyu mwalimu ambaye kastaafu miezi sita (6) iliyopita na bado hajalipwa vijisenti vyake vya mafao, ni nani hasa mnyonge?

Na huu usawa katika nchi hii uko wapi? Iweje mbunge aliyefanya kazi miaka mitano tu alipwe mafao ya kiinua mgongo kikubwa hivyo kwa takribani mara tano ya mwalimu ama nesi ama daktari aliyefanya kazi kwa miaka 35?

Huyu mtetezi wa wanyonge (Bwana Magufuli) anatetea wanyonge na unyonge upi hasa?

Mimi nasema Tanzania haina kiongozi Rais mtetezi wa wanyonge. Haijapata na hakuna kizuri wala kiongozi mzuri atakayetokana na CCM ili kubadilisha hali hii na kuleta tofauti na usawa.
 
Mtoa mada unataka usawa na wakati mpaka sasa mhusika mkuu anapiga kelele majukwaani na kwenye mikutano yake ya kuwataka wananchi wawe Wazalendo kwa kulipa kodi! lakini katika hali isiyo ya kawaida, kuna tetesi ya kwamba yeye mwenyewe mshahara wake eti haukatwi kabisa hiyo kodi!

Awamu hii imetuamsha wengi. Kutokana na kutamalaki kwa unafiki na ubinafsi, ni wakati sasa na sisi kujiongeza ili siku moja watoto wetu wasije kuyalaani makaburi yetu.

Ndiyo nataka HAKI na USAWA....

Lakini pia natahadharisha na kuwapa taarifa waliokuwa hawajui kuwa kuna INJUSTICE hii inaendelea nchini petu

Hata kama USAWA (equality) ni ngumu kuwepo ktk jamii kwa sababu ya nature ya binadamu ya "roho ya ubinafsi", lakini ingalau HAKI basi kwa kile mtu anachostahili....

Kidogo changu, ingalau nitendee HAKI kunipa kwa wakati. Usinitaabishe na kunisumbua miaka nenda rudi sipewi/silipwi kwa visingizio visivyo na miguu wala kichwa....

Hiyo hapana. We must shout. Tuungane na ku - shout...
 
Kwani nimekulazimisha kunijibu? Ondoa jazba kama mtoto, ...

Lieleze jukwaa ni kwanini wewe unadhani kusiwe na usawa?

Sera na ilani ya chama chako cha CCM (chama cha wanyonge chenye Rais wa wanyonge - Magufuli, huku kwa mlango wa nyuma akiwanyonga) inasemaje kuhusu HAKI KWA WOTE na USAWA miongoni mwa jamii?

Je, inasema HAKI na USAWA haiwezekani miongoni mwa jamii ya Watanzania?

Halafu pls, mimi sina jazba. Ni wewe ndiye mwenye jazba. Maandishi yako yamebeba elements hizo....
 
hata wabunge wetu wameshindwa kabisa kuwa watetezi wa wapiga kura wao! ni vyema wafanyakazi wote wakaungana na kutowapa ubunge wanaogombea kwa awamu ingine. tuwape wapya na tuwape jukumu la kwenda kupigania haki za wafanyakazi wanaoteseka.
Wanatetea matumbo yao, ukitaka kujua wanavyo tetea maslahi yao waguswe wao pension ipunguzwe utawasikia hapo!

Sent from my SM-T800 using JamiiForums mobile app
 
Chama tangia uhuru bado kinatawala hadi leo?
 
Rule No. 1
Never loose money

Rule No. 2
Never forget Rule No. 1
 
Back
Top Bottom