Ndugu zangu watanzania wenzangu nchi hii si moja, hakuna usawa ktk ujenzi wa miundo mbinu. Mwezi wa 8 nilisafiri kutokea Arusha kwenda Dodoma kupitia Kiteto.
Kiteto ni wilaya ndani ya mkoa wa Manyara. Ukitokea Arusha unapitia mji wa Orkesumet ambao ni makao makuu ya wilaya ya Simanjiro. Hilo basi nililopanda lilijaa kupitiliza kuanzia ofisini, hata pa kusimama ilikuwa ngumu bado njiani haiachi mtu. Kulikuwa na basi moja tu kampuni ya Simanjiro Express.
Barabara ni mbaya sana, ni vumbi na mashimo. Hutaamini km maeneo yale watu wanajua maana ya uhuru. Kule bado ni Tanganyika. Kutokea Kiteto kwenda Dodoma kuna njia 2, moja kupitia Kongwa na ya pili kupitia Izava(Kondoa).
Barabara kuu ni kupitia Kongwa kwa Ndugai. Kiteto ni eneo la kimkakati, ni wilaya ya uzalishaji mkubwa wa nafaka, inaunganisha ukanda wa kaskazini na kanda za kati na mashariki mwa nchi. Kutokea Kiteto unaenda Dsm na Tanga kupitia Mkata, unaenda Turiani(Morogoro), unaenda Dodoma, unaenda Babati na kwenda Arusha.
Utashangaa ndani ya nchi moja kuna maeneo kumejengwa madaraja ya njia 4 juu ya maji. Kuna maeneo kuna miundo mbinu ya barabara ya lami, reli ya MGR na kuna reli ya SGR. Ndani ya nchi hii moja. Kuna ubaguzi na uonevu mkubwa sn nchi hii. Mkoa wa Manyara uko nyuma sana kimiundo mbinu umepuuzwa pamoja na kwamba ni mkoa wa uzalishaji mkubwa.
Nani wa kuwasaidia hawa watu.