Hii nchi imegawanywa kuanzia kipindi cha Magu, Samia anaendeleza dhambi hiyo kuhusu ujenzi wa miundo mbinu

Acha wivu wewe, ulitaka kule linakojengwa daraja kusijengwe bali kufanyweje ,, we dai serikali ipeleke maendeleo sio iache sehemu fulani ipeleke kiteto, kila sehemu ina deserve miundombinu
 
Ninaunga mkono hoja. Ni kweli roho ya chuki imekuwepo huko nyuma kwa kiasi fulani angalau kwa kufichaficha,. Na kinachotuponza watanzania ni kufikiri hii nchi ni mali ya kikundi fulani cha watawala.
Awamu ya tano iliathiriwa kwa kiasi kikubwa na matokeo hafifu kuwahi kutokea tangu tuanze mfumo wa vyama vingi, na badala ya kutafuta solution ya nini walipaswa kufanya,wao wakajaa chuki kwa wote waliowanyima kura.
Ninakumbuka wakati wa uchaguzi wa Zambia,2002 Levi Mwanawasa alishinda kwa kura kidogo sana.
Yeye hakugombana na waliomnyima kura,alideal na mtangulizi wake Frederick Jacob Titus Chiluba, ambaye ndiye alikuwa chanzo cha matokeo mabovu.
Mmesimsikia hata huyu Mchengerwa,kudai eti maendeleo ya Arusha yameathiriwa na siasa za maji taka,sasa kwa akili za kiongozi kama huyo ambaye hajui hata mchango wa utalii kupitia Arusha ambao unafaidisha nchi nzima yeye anafikiria kuikomoa Arusha wanaoumia ni wanaarusha peke yao.
Kuna maeneo ya kimkakati kiuchumi unazuia barabara kisa siasa.
Huyu mama angalau alianza kuonyesha matumaini, lakini ameona mbele ni giza akaamua taratibu kurudi kule kwa mtangulizi wake. Kaanza na mbinu zile zile na watu wale wale.
Muogopeni sana Mungu,tendeni haki, tayari ameshatuonyesha ana uwezo kiasi gani. Yeye akiamua hatajali mlie hata mzimie,nchi itaendelea tu.
 
Kituko utasikia mbunge wa Kiteto naye ananadi flyover za Dar eti Mama anaupiga mwingi!
 
Mkoa wa Manyara ulianza lini labda???Na ukumbuke kuwa maendeleo ni hatua.Huwezi linganisha Manyara na Mbeya,Morogoro,Dodoma ambayo ni mikoa ya zamani.Muda ukifika Manyara nako kutatengenezwa tu.
 
Kwako wewe tanganyika imepata uhuru 2015?
 
Nyerere Mwinyi Mkapa na Kikwete walijenga hizo barabara Magufuli akaja kuzibomoa?

Kama walikuwepo hao na hawakujenga, huo ubaguzi wa Magu unakujaje?

Hizi ni chuki tu au kuna ujinga hapa?
Nani hakujenga wewe labda umezaliwa juzi na bila Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete nchi hii isingekuwa ya neema kama unavyoiona leo.
 
Well written/said
 
Acha uongo na chuki kwa Magu. Magu kwenye miundo mbinu alijitahidi sana sasa unazungumzia mkoa wa Manyara tu, kwamba Nchii hii barabara zote za mikoa zimejengeka sipokuwa Manyara tu? Itakuwa hujasafiri Mikoa mbali mbali Nchii. Barabara za Nchii hasa huku mawilayani bado zinachangamoto sana, tembea Miko hata 20 ya Tanzania na uingie huku wilayani utaelewa
 
Umeongea ukweli mtupu nchi ya wajinga viongozi wajinga.
 
Kwa nini huongelei lami zilizojengwa babati /manyara kipindi cha Magufuli?
Huu ni uchambuzi wa chuki
Amejawa na Chuki, anazungumzia barabara moja tu wkt wana barabarq ya kiwango sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…