Tulio wengi sisi sio vijana wadogo, tumetoka mbali, Angalia ID zote zenye miaka mingi ni watu wazima sisi.
Wengi ni watu wenye nafasi katika Jamii.
Lakini pia enzi zile computer zilikuwa maofisini kwa watu maalum,Watu walioweza kuwa na access na JF walikuwa watu wa aina fulani tu,Nakumbuka mahali nilipokuwa miaka ya 2000-2003 Computer zilikuwa 2 tu Wilaya nzima, ya ofisini kwangu Mimi na idara nyingine kulikuwa na Expert, naye huyo expert mara nyingi alikuwa anakuja ofcn kwangu kupata huduma ya Internet, ilikuwa ili huwezi kupata connection lazima uwe na line ya simu.