Ilikuwa siku mmoja nilikuwa kwenye mapenzi na kijana mmoja wa mwanza tulikutana ofisi fulani baada ya mazoea ya pale aliomba namba nikampa tukawa tunawasiliana kawawaid kila siku mpaka nikajikuta nimeingia kwenye mapenzi nikajikuta nampenda sana mimi na wivu jamani ukiwa na mimi unatakiwa uwe mvumilivu kidogo
Tulipanga siku ya mimi kwenda mwaza siku ilipofika nilijipanga vizuri nikiwa na basasha nyingi sana ya kukutana nae na kutokana na utani mwingi kipindi cha nyuma nikawa naona safari ndefu sana
Baada ya kufika siku ya kwaza alinipokea akanipeleka hotel mzuri tu nili lala nae usiku mzima kesho yake morng aliniaga anaenda kazini alinipa pesa ya dharura laki moja kumbee chumba hajalipa nimekaa pale siku tatu mtu hajatokea nikipiga simu apokei kisa sikijui nililipa na kurudi zangu kwetu bila kumpa taarifa
Ndipo nilipo fika akaanza jiongeleshq oh mimi nilikuwa nimebanwa simu iliisha chaji samahani ulitumia kiasi gani nikupe niliona upumbavu nika kata simu mpaka leo siwezi kumsafiria mwanaume ata awe nakaa nae mkoa mmoja ila wilaya tofauti siwezi