Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Hii ndoto ilinifanya nikasilimu

Mungu ni Cheo katika nafsi kuu 3.

1. Mungu Baba (Yehova/Yawe....majina zaidi ya 27).

2. Mungu mwana (Yesu/Neno/Kweli/Mwanakondoo/Mikaeli....).

3. Roho Mtakatifu.

Mfano halisi wa utatu wao mtakatifu ni yai 1 lililo na ganda/gamba la nnje + nyama nyeupe + kiini.

Ukimwomba Mungu hukusikia ila Yesu kapewa mamlaka zaidi sababu alijitoa nafsi yake kufanyika kafara ya damu msalabani ili uokolewe toka dhambini na upate uzima wa milele (maisha baada ya kifo cha hapa duniani).

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
BULLSHIT! 🤢🤮🤣🤣🤣
 
Ukisoma Quran utagundua manabii wote kuanzia Adam,Ibrahim,Mussa, Suleiman,Yakub,Issa na wengine wote walikuwa waislam.
Adma ndie muislam wa kwanza
hebu tuthibitishie kuwa kitabu hicho ni cha kweli. na sisi tutakuthibitishia kuwa chetu ni cha kweli. sisi tunaamini chako ni cha uongo hivyo hatuna hata sababu yakukiamini kilichomo ndani yake.
 
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una waislam tupu. nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.
Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu.
Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.
Allahu akbar.

PS: yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
hii avatar yako si ukute wewe ni yule afande wa zanzibar alikuwa anafumuliwa?
 
Mkuu endelea kujifunza uislam nazan mpk mda huu ujajutia uamuzi wako unaeza kua balozi mzuri wa kufundisha hawa vichwa ngumu wanaozani uislam ni vita
Vipi kuhusu makundi ya Kigaidi yanayosema " Allahu Akbar".?
 
Karibu katika quran na sunnah.
Uislamu maana yake Kusalimika.

Achana na propaganda za dini hii kuhusishwa na Ugaidi

Hivi unajua kuwa kuoa mke zaid ya mmoja kuna hekma kubwa sana kwa Alie tuumba.

Wacha hiyo, hivi unajua uislamu ndio dini iliyokuna kufundisha watu kujilinda vizuri na najisi( kinyesi na mikojo).

Ntaendelea wacha kwanza nimalizie kazi.

Kwahiyo waislamu hamnyi wala hamkojoi?[emoji28]
 
wasi wasi wangu vipi ungeota unaona watu wanaume wanakatwa😂😂😂😂.
 
True story: Tea time,

Nilizaliwa katika ukristo na kukulia kwenye ukristo.

Mwaka Jana nilihamia Tanga kikazi, mtaa niliokuwa Ninaishi ulikuwa una waislam tupu. nyumba nliyokuwa Ninaishi ilikuwa jirani na msikiti, Kila siku pale msikitini walikuwa wanaimba aya za Quran Usiku kucha. Sijui kwanini lakini Ile sauti ilikuwa ni nzuri sana masikioni na ilinifanya nikawa najisikia amani sana nilalapo.

Mwaka huu mwezi fulan nikiwa nimelala, nikaota ndoto ya ajabu iliyonifaonya nisilimu wiki hiyo.
Ndoto yenyewe ilikuwa hivi:

Niliota Mimi na kaka yangu wa Arusha tukitembea maeneo ya mtaani kwetu hapo Tanga. Tukakutana na kundi kubwa la watu wa Kila aina matajiri kwa masikini wakiingia katika ule msikiti jirani.
Pamoja na tofauti zao za kiuchumi lakini wote waliingia ndani katika ule msikiti na kuwa kama kitu kimoja. Hakukuwa na madaraja mule ndani, hakukuwa na mabenchi ila wote waliingia kama watoto wadogo wakijisalimisha kwa Muumba wao. Ni kama vile pesa,vyeo,umaarufu waliviacha nje ya msikiti.

Nikapita jirani nikasikia ndani Quran inasomwa na wote wakistaajabu maajabu ya hiki kitabu kilichoandikwa Karne nyingi zilizopita.

Nikapita kwa pembeni nikielekea zangu nyumbani, ila kwa nje nkakutana na mtu akawa ananialika tuingie kuswali, nikakataa kwa visingizio vingi kama vile Nawahi sehemu,sijui kuswali,siku nyingine nk. Nk.

Lakini yule mtu akanisisitiza na kuniambia kuwa nikiingia Mungu atanitoa gizani na kuniweka kwenye njia ya haki.

Mi nkaondoka lakini nkamuacha kaka angu akiongea na yule mtu. Ndoto ikaishia hapo.

Kaka angu niliokuwa sijawasiliana naye takriban wiki 3 na sikumwambia kuhusu hiyo ndoto,lakini wiki hiyo hiyo nilisikia kuwa kaka angu wa Arusha amesilimu.

Kiukweli nilistaajabu sana na kujiuliza ni nini hiki na maana yake nini?

Baada ya Tafakuri ya mda mrefu niliamua kwenda kwenye huo msikiti labda nitakutana na yule mtu wa ndotoni na hiyo ndiyo ikawa njia iliyonipelekea kurudi kwenye uislam(Kila mtu huzaliwa muislam).

Katika kumtafuta yule mtu Kuna shehe nilimsimulia, akaamua kuchukua jukumu la kunifunza na kunielezea maajabu ya Quran na kiukweli Ile ndoto + maajabu ya Quran ilinifanya nikasilimu.
Bado naendelea kujifunza mengi mapya katika hii Imani ya kweli na haki.
Allahu akbar.

PS: yule mtu Bado sijampata
PS #2: Braza wa Arusha anajua namimi nimesilimu lakini sijamuhadithia kuhusu Ile ndoto.
Wanawake wakitanga ni mafundi sana. Hao ndio sababu kuu yakusilim kwako. Wakubwa tumeelewa sana justification tu unaitafuta.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Siku ukiishi karibu na kanisa utaota pia unaingia kanisani.After all is not big deal wewe kwenda huko kwani wapo wanaotoka kwenye uislam na kuwa wakristo
 
Back
Top Bottom