Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Watanzania wote tunashuhudia jinsi Jeshi la Polisi lilivyojipanga katika kuzima maandamano ya amani yaliyoandaliwa na CHADEMA hapo kesho.
Tunashuhudia askari wengi sana wakimwagwa mitaani, huku wakiwa na magari ya washawasha, wakirandaranda na farasi, wengine hata wakiwa wamebeba na silaha za moto.
Swali Moja tu jepesi ambalo nataka kuwauliza Jeshi la Polisi, hivi juhudi kubwa kabisa ambazo mnazitumia, Kwa ajili tu ya kuyazima maandamano ya amani ya CHADEMA hapo kesho, Kwa kuwa nyinyi Jeshi la Polisi na Jeshi lolote Duniani, wajibu wenu namba Moja ni kuwalinda raia na Mali zao, naomba mjiulize hivi hizi juhudi zote mnazitumia, mngezitumia katika kuwatafuta viongozi wa CHADEMA waliotekwa na watu tunaoaminishwa kuwa ni watu wasiojulikana, hivi Hadi leo hao akina Soka wangekuwa tu bado hawajapatikana??
Na Kwa kuwa Jeshi la Polisi mahali popote pale Duniani, wajibu wao namba Moja ni kuwalinda raia na Mali zao na Kwa kuwa Jeshi letu la Polisi wsko wapi na Jeshi limeshindwa kutuambia hao ndugu zetu kina Soka, ambao toka watekwe ni zaidi ya mwezi mmoja, jambo la muhimu la kufanyika ni kuwajibika Kwa kujiuzulu, Waziri wa Mambo ya ndani, Yusufu Masauni na IGP Wambura.
Mungu ibariki Tanzania