Gentleman,
sio rahisi gari lako ukalitumia mwenyewe pekee mwaka mzima,
inaweza kua ulilipeleka gereji, baada ya marekebisho, wakati fundi gereji analitest barabarani akakutana na hiyo kitu halafu akapiga kimya,
inawezekana ulipeleka gari lako car wash, muosha magari wa eneo la ofisi yako au makazi yako ulie mzoea na kumuachia funguo za gari, alitumia gari lako na kukutana na hiyo kitu,
inawezekana ulisindikizwa airport na gari lako, na aliekua akirudi nalo home akakutana na hiyo kitu,
inawezekana ulitoa gari lako kwa nia njema tu kusaidia jambo fulani muhimu, mathalani kumpeleka mgonjwa hospital, kupeleka wageni wako mahali fulani kwa kumtumia dereva wako unaemuamini akakutana na hiyo kitu n.k n.k.
Sinarioz za kutokea kwa hiyo kitu ni nyingi na hata ulalamike namna gani, ni ngumu mno kuchomoka.
Nadhani ni muhimu sana kulipa, na kuchukua changamoto hiyo kama fursa muhimu sana kwako ya kuongeza umakini zaidi wa matumizi ya chombo chako cha usafiri 🐒