Hii ni haki kweli? Nimekuta gari yangu inadaiwa wala sijui kosa, sina taarifa yeyote

Hii ni haki kweli? Nimekuta gari yangu inadaiwa wala sijui kosa, sina taarifa yeyote

Hiyo kesi mpelekee RTO
Hawa ma RTO nao ni wapumbavu tu! Mimi kuna jamaa alinibambikizia gari yangu deni mwaka 2022 sasa leo ni mwaka wa nne huu sijalilipa. Eti gari yangu imekamatwa imezidisha abiria wakati siyo gari ya abiria. Na mbaya zaidi imeandikiwa deni mkoa mwingine ambako tangu nimeingia nchini sijawahi kufika huo mkoa. Wakanielekeza kupeleka malalamiko yangu kwenye dawati la malalamiko pale Makao makuu nikaunganishwa na Afande anaitwa Saburi naye akanioeleka kwa RTO wa mkoa husika ambako deni lilitokea, sasa huko nikawa mnapigwa rongorongo tu. Mwisho wa siku wananiambia trafiki aliyeandikia hilo kosa amestaafu kwa hiyo sina budi kulilipa. Nawauliza lakini mwenye leseni siyo yupo kwa nini msihamishie deni kwake, hawataki wanadai mwenye leseni alishaitelekeza mpaka imeisha muda wa matumizi. Sasa hapa najiuliza na mimi niweke mgomo kulipa hilo deni? Ni hela ndogo lakini kwa nini ulipie uzembe wa mtu?
 
Gentleman,
sio rahisi gari lako ukalitumia mwenyewe pekee mwaka mzima,

inaweza kua ulilipeleka gereji, baada ya marekebisho, wakati fundi gereji analitest barabarani akakutana na hiyo kitu halafu akapiga kimya,

inawezekana ulipeleka gari lako car wash, muosha magari wa eneo la ofisi yako au makazi yako ulie mzoea na kumuachia funguo za gari, alitumia gari lako na kukutana na hiyo kitu,

inawezekana ulisindikizwa airport na gari lako, na aliekua akirudi nalo home akakutana na hiyo kitu,




inawezekana ulitoa gari lako kwa nia njema tu kusaidia jambo fulani muhimu, mathalani kumpeleka mgonjwa hospital, kupeleka wageni wako mahali fulani kwa kumtumia dereva wako unaemuamini akakutana na hiyo kitu n.k n.k.

Sinarioz za kutokea kwa hiyo kitu ni nyingi na hata ulalamike namna gani, ni ngumu mno kuchomoka.

Nadhani ni muhimu sana kulipa, na kuchukua changamoto hiyo kama fursa muhimu sana kwako ya kuongeza umakini zaidi wa matumizi ya chombo chako cha usafiri 🐒
Mwenye gari kasema hajatumia mwingine zaidi yake we unalazimisha sio rahisi hvi unakichaa au
 
Hapana. Na hakika ndugu, mwaka huu hakuna aliendesha gari yangu . Narudia tena hakuna, wala sijawahi acha sehemu yeyote, ni uhuni umefanyika, na kwa nini serekali ina ruhusu kuandika faini kwa kutumia plate number? Ni rahisi sana kuwepo na uonevu.
Hakuna serikali mkuu, acha kujisumbua kuilalamikia hiyo Serikali isiyokuwepo
 
Ingia kwenye web ya kuangalia madeni (tms check) utaona hiyo faini iliandikwa wapi, tarehe, na leseni iliyoandikiwa km vyote huvijui nenda ofisin ya trafick onana na RTO Mungu akiwa upande utafutiws hilo deni
Namba ya malipo ikitoka, kufuta hilo deni bila kulipwa ni mchakato. Hakuna namna, ni kukubali tu kulilipa vinginevyo atatumia gharama kubwa na muda kuthibitisha ukweli ili deni kufutwa.
 
Ni ndogo sana, unamiliki gari unashindwa kulipa 60000?
Teh teh ngoja uanze kujitegemea utajua hujui. Mara nyingi haya yanazungumzwa na watu ambao hawana majukumu.
Kuwa na gari siyo tiketi ya kulipia bills hovyo
Siyo tiketi ya kutopanda dala dala au bajaji even boda think wise bruh.
 
Hiyo ni ishu ya kawaida Sana Mimi mwenyewe imenitokea mwezi uliopita gari ilikuwa na deni la Tsh 60,000/= Yule traffic aliprint mkeka nikaenda zangu makao makuu ya polisi usalama barabarani.
Ukifika pale kuna dawati la malalamiko ya makosa ya kuandikiwa fine,
Baada ya masaa 24 deni liliondoka, ni ishu ndogo Sana ukienda pale makao maku
 
Back
Top Bottom