Hii safu ya viongozi wa ACT-Wazalendo inafikirisha sana!

Kati ya uliowataja ndiye umeleta huu uzi, et lengo chama kisipotee kwenye mitandao, hovyo kabsaa
 
Vipi Zitto hakushtukia hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wa Nchi nae hakushtukia hii?-
Btw, ni kwamba haujui kwamba ACT ina wafuasi wengi kutoka Zanzibar, na hata ukiangalia hayo majina, wengi ni ex-CUF, au ndo basi tu kutaka kushadadia propaganda za Lumumba?!
 
Mbona kama safu ya uongozi wa taasisi ya kidini?

Hivi ACT hakuna wakristo huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hapa chini ni safu ya viongozi wa nini?!
 
Hao ulio wataja hapo wana experiences katika siasa,especially now siasa za kukunuana eti uunge juhudi, Chama kinahitaji viongozi kama hao wasio tetereka kwa pesa ya dafu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi jiwe huwa anawacheki halafu anachekaje??
IHHIIIIIIIIIIIIII!!!!!!!
nimekuelewa mleta mada
Atawacheka kama ana makengeza manake sioni tofauti yoyote kati ya ACT na CCM inayoongozwa na Jiwe kwa kuangalia hii safu:-
Tena bora hata hao ACT ambao atakae kutumia akili yake sawasawa, fasta atajua kwamba ACT ina wafuasi wengi waliokuwa CUF, hususani CUF!

Sasa mtu atashangaaje kuona majina aina hiyo?!
 
Buraza usi panic .mm nilikua nataka kujua jiwe anachekaje basiiii.
Siasa mm wapi na wap.
Hizo nawaachia nyie
 
Wakati taifa letu linazidi kusonga mbele kidemokrasia,kuna kila dalili za kuvunjika kwa umoja wakitaifa ambao ndio msingi na tunu kuu ya Tanzania.
Aidha kuna dalili za ukabila na ukanda nazo zinajitokeza kwenye siasa zetu ,na kuna mawakala wanazipalilia humu nchini.

Kwa kuepuka mivutano isyokuwa ya lazima huko mbeleni kwa vizazi vijavyo
inatupasa tufikiri vyema ni namna gani mambo haya tunayawekea misingi isiyotetereka.

Kimsingi ,katiba yetu imeweka wazi kuwa uongozi wa nchi hii hautatolewa kwa kabila wala dini fulani, na kufanya hivyo ni makosa kisheria,
Iweje basi baada ya mutu kuchaguliwa kwa taratibu za kikatiba ya nchi atokee mtu aanze kuimba wimbo wa kabila, kanda au dini?
Jee Kufanya hivyo kwa kutuhumu nako si kosa kisheria?
 
Hii ACT Wazalendo haina tofauti na ile CUF ya kabla ya Ukawa.Lakini sijashangaa sana kwa kuona hivyo kwa kuwa CUF kabla ya Ukawa ndiyo hiyo hiyo iliyounda ACT Wazalendo ya sasa.CUF B.Naamini watakuwa na majibu mazuri ya kuaminisha watanzania kuwa wao siyo wabaguzi wa ki...d....ni.
 
Hii vipi kama ni baraza la maaskofu vile

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Hii vipi kama ni baraza la maaskofu vile View attachment 1409183

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
Mngekuwa makini mngetumia fursa hiyo kwenye chama chenu kuwa tofauti.Hii maana yake hamjajifunza chochote.Bora ya hao CDM ambao pamoja na mapungufu yao,wameonyesha dira.Tumaini jipya.Hata hivyo kwenye hiyo orodha ya CHADEMA naona viongozi wajuu kabisa,Makamu mwenyekiti na naibu Katibu Mkuu.WAPO.
 
Kipi walicho nacho tofauti au hiyo dira unayosema chama kina mpaka wachungaji wa kanisa ukristo wa wazi uchaga wa dhahiri ukanda nk halafu unadai tumaini jipya una chekesha sana cdm kimejaa uchaga na udini wake jibu utaliona uchaguzi ujao watakuwa watazaji hakuna mbadala wa CCM labda ipite miaka elfu mbili mingine

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Mmh! Kweli orodha hiyo inafikirisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Why are you still living in dark continent?

Jog on!
 
Mkuu, kama kweli ulitabiri hivyo na hivi ndiyo yanaenda Kutokea basi wewe unastahili uitwe muonaji,

Kwa sehemu nyingine Kifo cha Chadema hata wao wamechangia, mkuu, nakumbuka siku moja nilitaka kukwidwa kwenye basi nikisafiri kutoka Dar kwenda Lupilo kwenye mashamba yangu, Wakati huo ndiyo lilikuwa kumewaka Moto bungeni, yaliyokuwa majambazi ya CCM yakiaibika Kwa kujiudhuru Kwa hoja nzito za kina ZZK kina Lisu na wengine wengi vijana machachari wa Chama changu nyakati hizo Chadema

Kwa hakika kila mtu alikuwa akiliona anguko la CCM lile pale, Chadema ikipiga jalamba kuingia Ikulu bila ya Shaka,

Tulibishana na mtu humo kwenye basi,jamaa bhana akakasirika si akataka kunipiga, na Kwa Chadema kipindi hicho ilikuwa ikiungwa mkono na watu wengi Sana kipindi hiko, kustukia tumekuwa wengi, jamaa akanywea na hoja tuliyokuwa tukiiongelea ni Yale mafisadi papa ya CCM kipindi hicho yaliyokuwa yametangazwa pale mwembe yanga

Chadema, mahali ilipokuja kuniboa na nahisi ndio sehemu pekee ilipojikwaa na kuwakatisha tamaa wengi, na pale walipomkaribisha mmoja la fisadi tulilokuwa tukilipigia kelele Sisi Chadema,

Ukweli bila kuficha, binafs nilianza kumpenda mtu mmojammoja na si Chama, mpaka sasa Chadema kuna watu wangu nawapenda na nimshabiki wao mzuri tu, pia CCM Wapo nao wakubali, hivyo Mimi binafsi sina Chama,sidaiwi na mtu, na hicho ndicho kilichochangia Kwa sehemu Chama changu cha Zamani kuanza kutokuaminika

Kama CCM inakiua Chama hiki Ila hata wao wajue kabisa wamechangia pia kukiua hiki Chama chao
 
Mimi nauliza 1. kiongozi mkuu na mwenyekiti nini tofauti ya kazi zao? 2. Kiongozi mkuu kwa kingereza cheo chake tumuiteje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…