Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Hii Taarifa ya NHIF kama ni ya kweli basi Tanzania tuna tatizo

Bilashaka MCT wameingilia kati kwasababu ya kesi ya Dr.Mavula na mgonjwa wa thyrodectomy.Nahisi tu lakini.
Ilikuwaje hii issue?
Tusio ijua tupe intro kidogo.
 
Wacha tukachague hospital zenye hadhi basi ili wawe wanapapaswa vizuri hamna kwenda kule kwa wakulima.

Hapa gongo la mboto nafanya utafiti kati ya rugambwa au kitonka nikite kambi wapi.
Kitonka mara 1000 zaidi
 
Ndyo maana ikawekwa mara tatu mkuu kwa mwezi, au hakijaeleweka Nini?
Wamesema kwenye kituo kimoja ndani ya mwezi, wakati Kuna watu wanasafiri kila wiki. Na hata hivyo kwa nn mara 3?? Mimi najuaje kamaa nitaumwa mara 4 au 5??
 
Ni heri watuletee fomu za kujiondoa kama ni kweli hii inshu maana wanaochanga ni wengi ila watumiaji ni wachache.
 
AAR na STRATEGIES wateja wao huwa hawana tabia za kujirudia rudia kwenye vituo vya afya kupata huduma,, ila NHIF leo yupo hapa, kesho pale, kesho kutwa huku, ndyo maana wameamua kuwadhiti, hata wewe jiulize ndugu yangu, mtu hata dose hii hajamaliza kashahamia kwingine, huko nako hajamaliza dose aliyopewa kaenda kwingine, unakuta mtu mmoja kahudhuria mara 10 au zaidi vituo vya afya kwa mwezi!

NSSF wao huo utaratibu wa kutibiwa kituo kimoja tu na mara 3 wanao muda mrefu Sana, wateja wao hawasumbui washazoea.

Kwa Sasa kinachowafavour AAR na STRATEGIES, wao hawanalimit nyingi hasa upande wa dawa na vipimo, kwa hyo unaweza tibiwa vizur ukakaa Zaid ya miezi 3 hospital hupajui!

Ila Kuna viashiria nmeviona juzi juzi ndyo maana nasema Ni suala la muda huko kwao
Kama nia ni kudhibiti kwenda different hospital kwa tatizo moja inatakiwa mfumo uonyeshe kuwa huyu katibiwa kituo A na doctor atamchukua maelezo kwanini kaja kituo B kwa same problem then ataamua kumrudisha kwa doctor wake kufata referral letter na sio huu ujinga kumtangazia mwananchi kuwa anapaswa kwenda hospital mara 3 kwa mwezi.

Tatizo hapa nimegundua watu wenu wa Tehama ni bongolala hawataki kuumiza vichwa na kuweka mfumo utakaoonyesha taarifa kamili za awali za mgonjwa kabla hajaanza kuhudumiwa kwenye kituo B.
 
Kikwete na CCM walikomba pesa zote kwenye mifuko ya pensheni na Kisha kuondoa fao la kujitoa, kwa janja ile ile Hangaya ameufikisi mfuko wa Bima ya Afya na kuja na mbinu ile ile....hahahaha!
NHIF imedilisikaaaaaaa, waambieni wat
 
samahani ndugu zangu mlioajiriwa na serikali hii ambayo kwakweli sisi tulio nje ya mfumo mnatusaidia sana pale tunapohitaji huduma yenu na kisha sisi na ninyi ndio tunaochangia kuwalipa mshahara kwa kodi.
wakati mwingine huwa naona huruma pamoja kimaisha mnatuzidi kwa maisha ya uhakika na mikopo mnayopata kupitia kazi zenu na mkimudu maisha angalau kwa kiasi cha kamba zenu.
lakini ifike wakati niwashauri ikiwezekana muanze kufikiria kujitoa kwenye huu utumwa wa kuajiriwa na kutegemea serikali ikiwezekana muwe radhi unapofikisha miaka 51 muanze kufikiria kujiajiri na inapofika 55 muwe mmejiajiri rasmi kuliko kuendelea kukaa na kulalamika kila kukicha.
mfano mzuri waangalieni vyeti feki waliokubali na kusema wacha maisha yaende wamejipanga na wengine wako vizuri wakiendesha maisha vizuri zaidi wakijituma kwa ufanisi.
ifike wakati waajiriwa tambueni uwezo wenu na mjipange kwa malengo makubwa natamani kuwa na watu wanaofikiria miaka 50 ijayo hata kama hawatakuwepo lakini they have build the stone for future stand!
acha malalamiko wanasiasa hawawezi kukusaidia ila kitu kwa kuwa wao wanapenda watu wanaolalamika kisha wawabembeleze ili wasiwaze kesho yao na wao wawatawale kirahisi kizazi hadi kizazi!
MWENYEZI MUNGU awatie nguvu sana katika wajibu wenu unaofanya kwa taifa na siku zote mkumbuke hatamu ndio utamu wa safari kwa aliye juu ya punda au farasi na wajuzi wa lugha wakapunguza makali ya kuita farasi wakasema tu usiwe fara ili waelewe wachache kuwa usiwe farasi ukapandwa ukaleta ugomvi kwa aliyekuita!
msionielewa nawaombeni msiniumize kwa matusi na wale walionielewa watumie busara kuwajibu.
kwa pamoja tutaweza!
 
Halafu lilivyo lijinga utalisikia: "....awamu iliyopita mfuko ulikuwa unaendeshwa mikopo na sio michango ya wanachama...watu walikopa ili kulinda vibarua vyao....."

Komredi Kinana Oyeee! Burembo Oyeeee!, Steven Wassira aka Tyson Oyeeeee! Makamba Mkubwa Mzee wa Asali Oyeeeee!
 
Kama nia ni kudhibiti kwenda different hospital kwa tatizo moja inatakiwa mfumo uonyeshe kuwa huyu katibiwa kituo A na doctor atamchukua maelezo kwanini kaja kituo B kwa same problem then ataamua kumrudisha kwa doctor wake kufata referral letter na sio huu ujinga kumtangazia mwananchi kuwa anapaswa kwenda hospital mara 3 kwa mwezi.

Tatizo hapa nimegundua watu wenu wa Tehama ni bongolala hawataki kuumiza vichwa na kuweka mfumo utakaoonyesha taarifa kamili za awali za mgonjwa kabla hajaanza kuhudumiwa kwenye kituo B.
Mkuu, mfumo upo, taarifa za wagonjwa zinakuwa submitted kwenye mfumo
 
NHIF ina ubaguzi katika utendaji wake. Inapendelea waajiriwa wanaokatwa kutoka mishahara. Wao ndiwo wanapata huduma kubwa.
Kama umejiunga mchangiaji binafsi, huduma zimegaiwa kwa daraja 3. Na hatà ukichangiya kifurushi wanaita TIMIZA, ambacho ndicho cha juu huduma nyengine hupati hata kama mchango wako ni mkubwa kuliko anavyokatwa muajiriwa.
 
Back
Top Bottom