LGE2024 Hii ya Samia kupanga foleni kujiandikisha inafikirisha kidogo

LGE2024 Hii ya Samia kupanga foleni kujiandikisha inafikirisha kidogo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
HIi imenishangaza yaani akili yangu imegoma kuelewa.

Yaani, mtu alikuwa anaelekea kujiandiandikisha kupiga kura, huko barabarani msafara wake umesababisha watu na magari kusimamishwa ili kuruhusu “mheshimiwa awahi” aendako (hili ni la ajabu pia lakini tumeshalizoea hakuna namna ya kulibadilisha kwa sasa)

Kilichonistaajabisha hadi kufikia kuandika huu uzi ni yeye baada ya kufika huko kwenye kujiandikisha eti akapanga foleni, yaani eti aliowakuta hawakumpisha.

Naona kama vile wananchi wamekosa adabu, iweje ushindwe kumpisha mheshimiwa apite mbele wakati huko barabarani watu wamempisha na kusababisha kuchelewa kwenye shughuli zao na wengine wagonjwa wamechelewa kufika hospitali kwa wakati kupata matibabu.

View attachment 3122399
Hao wote ni waigizaji wenzake. Wacheza sinema
 
Maigizo hayo jombaa!
 
Umeongea mengi ya maana. Lakini angeenda stright bila kupanga foleni pia angekuwa amehamasisha watu wakajiandikishe.
Hakukuwa na haja ya yeye kupanga foleni wakati huko barabarani hajapanga foleni tumesimamishwa ili tumpishe. Hoja yangu ipo hapo.

Hapana pale ni technic kubwa sana ya kuwavutia watu kujiandikisha .
Watu wengi hawajiandikishi wala kupiga kura kwa sababu hawataki kukaa muda mrefu kwenye foleni ya kujiandikisha . Sasa pale Rais akawaonyesha wetu kuwa hilo zoezi ni muhimu sana pamoja na kwamba linaweza kumpotezea mtu muda wake.

Pale Dr. Samia ameonyesha uvumilivu katika kutimiza haki yake ya kupiga kura.

Angekuja moja kwaoja isingekuwa habari.

Na watu wangesema kuwa wakubwa wao hawapotezi muda lakini wadogo wanapanga foleni hivyo ni bora kuwaachia hao wenye nchi wapige kura.

Kwa hili mama ameupiga mwingi
 
Wanawahadaa Watanzania wasiokuwa na uelewa

Wanaowahadaa ni wale wasioona mantiki ya Rais kujiandikisha na kuhamasisha watu kujiandikisha.
Yaani hata Nyerere mbona alikua anapanga foleni kupiga kura ?

CCM pamoja na kuvamiwa na genge la mafisadi lakini ni chama kinachowasomesha sana Makada wake katika siasa.

Hiyo ni moja ya hamasa kubwa sana.
Wapinzani watashindwa sio kwa sababu ya wizi wa kura wala nini bali ni kwa sababu wanategemea mbinu za CCM ziwabebe wakati CCM hakina mpango wa kuwasadia wapinzani kupata ushindi.

Yaani wapinzani wanakosa ubunifu wakati wa uchaguzi .

Chadema Enzi za Kina Zito,Mkumbi, Dr.Slaa., Baregu, n.k.

Kuna mkoa mmoja wetu waliona Wazee ndio wanaowachagulia maCCM ,walichofanya ni vijana walioficha kadi za wazazi wao siku ya kupiga kura. CCM chale. Sasa hizi ni mbinu za akuanaaye mmalize.
 
Mungu anamuona mtu hata yule mlevi wa maandamano kila haramu halafu akasalitiwa na watu wake mwenyewe:pedroP:
Hapo ndipo ulipo ulipofikia au kuna ziada?
Hata kama uchawa lazima za asili huwa zinabaki.
Aliyeongelea maandamano nani?
 
HIi imenishangaza yaani akili yangu imegoma kuelewa.

Yaani, mtu alikuwa anaelekea kujiandiandikisha kupiga kura, huko barabarani msafara wake umesababisha watu na magari kusimamishwa ili kuruhusu “mheshimiwa awahi” aendako (hili ni la ajabu pia lakini tumeshalizoea hakuna namna ya kulibadilisha kwa sasa)

Kilichonistaajabisha hadi kufikia kuandika huu uzi ni yeye baada ya kufika huko kwenye kujiandikisha eti akapanga foleni, yaani eti aliowakuta hawakumpisha.

Naona kama vile wananchi wamekosa adabu, iweje ushindwe kumpisha mheshimiwa apite mbele wakati huko barabarani watu wamempisha na kusababisha kuchelewa kwenye shughuli zao na wengine wagonjwa wamechelewa kufika hospitali kwa wakati kupata matibabu.

View attachment 3122399
Hizi sura zinaonekana ni CCM daima 🤣
 
Ajira yake ni siasa hivyo lazima aoneshe juhudi kuhamasisha watu wataoendelea kumfanya apate mkate wake wa kila siku...
 
huyu mama ni lulu ya taifa wallah

anatukumbusha watanzania yaliyo ya msingi kabisa
 
Hapo ndipo ulipo ulipofikia au kuna ziada?
Hata kama uchawa lazima za asili huwa zinabaki.
Aliyeongelea maandamano nani?
ni yule mlevi mkubwa wa kile chama ndie hasa anependa kuongelea maanadamano haramu :pulpTRAVOLTA:
 
Na watu wangesema kuwa wakubwa wao hawapotezi muda lakini wadogo wanapanga foleni hivyo ni bora kuwaachia hao wenye nchi wapige kura.

Kwa hili mama ameupiga mwingi
Kule barabarani tulivyosimamishwa muda mrefu ili apite, Tulisema kuwa wakubwa hawana utu, wanasababisha watu kuchelewa kwenye shughuli zao. Na kusababisha wagonjwa wachelewe kupata matibabu na pengine kupelekea kufa.
 
Mkuu, kuwa na heshima kidogo na kiongozi wetu mkuu wa nchi.
Uzi ilivyoanzishwa hakutaja jina aliandika kiongizi fulani, soma pia comment #1, hata hiyo picha haikuwepo,

Uncertainty is catalyzed by disaster, information ,(media) and people, (normal and smart people)
 
Foleni aloanza mzee JPM pale chamwino ingieni maktaba. Muda wa kuomba kura huu.
 
Mimi sina tatizo na kutii mamlaka, nimeshangazwa na hao wapanga foleni kwanini wasimpishe mheshimiwa ahudumiwe haraka kama ambavyo wananchi wengine barabarani walimpisha bila tatizo?
Anatengeneza picha sawa na ile ya Mwalimu Nyerere miaka ya nyuma alipoamua kupanga foleni siku ya kupiga kura.

Mwanasiasa anakuwa na maisha yale yale ya kina Diamond na Ali Kiba, ya kufikiria magazeti ya kesho yatapambwa vipi na habari pamoja na picha yake.
 
Back
Top Bottom