Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Matapeli tu hawa.. na wapo watanzania wanaowaamini!
 
Anazunguka kwenye mashule ili kutesti kwanza nguvu zake kama ziko sawa ndo aingie kitaani mkoa kwa mkoa aje kuombea vidume na mikurumbembe ya mjini.
Maana akikurupuka kuingia mitaani bila kufanya testi ya mitambo anaweza kukutana na makubwa.!
Kuna jamaa aliibukaga kijijini kwetu miaka hiyo akajifanya nabii eti akawatukana wachawi wa kijiji kwamba yeye hawamuwezi haikupita hata siku tatu alikutwa uchi wa mnyama amelala mku.ndu juu chini ya mwembe wa shule ya msingi na inasemekana alichezea "kifiro"
 
Mkuu serikali haina dini ila inatambua uwepo wa dini na imani za watu, na ndo mana ata mashuleni kuna muda umetengwa maalumu na kuingizwa kwenye time table kwa ajili ya vipindi vya dini.

Apo sidhan kama kuna tatizo
 
wazee wa kamati ya roho mbaya walifanya yao
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
attach hyo clip
 
Nini maana ya makanisa rasmi ? Wakati Yesu anaondoka duniani aliacha kanisa gani rasmi unalolijua wewe ? Umeingia chaka hakuna unachokijua kuhusu injili ya Yesu Kristo na siku za mwisho, maana alisema katika siku za mwisho injili itahubiriwa kila mahali ili uwe ushuhuda kwa kila mtu. Wewe kwa andiko lako hili huwezi kuzima moto wa injili. Maana ni kama moto uliotupwa duniani hakuna wa kuuzima. Narudia tena kukusihi kwamba mwamini Yesu ili awe Bwana na Mwokozi wako vinginevyo unapoteza muda tu.
Kwanza usinibwatukie. Nikuulize kitu labda utajielewa na kuacha kubwatuka. Wakati wa ukuaji wako (utoto wako) uliwahi kushuhudia uotaji wa haya makanisa mitaani kama ilivyo sasa? Kulikuwa na makanisa rasmi na yanajulikana. Nadhani jibu umelipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…