Hiki anachofanya Masanja Mkandamizaji sio sahihi kabisa

Matapeli tu hawa.. na wapo watanzania wanaowaamini!
 
Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha Masanja Mkandamizaji na vijana wengine nadhani ni wafuasi wake katika kanisa lake lile liko pale Leaders club. Clip inaonyesha wako ktk shule fulani nmeshindwa kujua ni shule gani exactly lakini kwa mazingira inaweza kuwa Arusha, anaonekana Masanja anaomba na watoto wanaanguka kimapepo.

Hii kitu sio sahihi kabisa kwa mazingira ya eneo la elimu na pia kwa mazingira ya watoto wadogo. Sijui uongozi wa shule waliweka wapi akili na fikra zao kuruhusu hili.

Binafsi nmeona ni jambo lisilo na mantiki kabisa. Sioni kabisa logic ya hii kitu kabisa. Inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia hapo baadae kwa wanafunzi na hata shule husika pia.

Tunajua jinsi baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kutumia nguvu tofauti tofauti kujifanya wanakemea mapepo na watu wakianguka ovyo, huwa sijui lengo hasa ni lipi lkn kwa watu wazima wenye akili timamu ambayo hawajapelekwa pale kwa bakora, walienda kwa matakwa yao ni sawa.

Lakini kwa watoto wadogo kama wale hakika sio jambo sahihi kabisa. Unless hiyo shule iwe na shida fulani inayohitaji maombi kama yaliyofanywa na Masanja na watu wake.

Lakini kwa uchunguzi kidogo nimebaini ni kama tour huyu Masanja anafanya katika mashule kufanya anachokifanya. Hapa namaanisha kuzunguka katika mashule na kuombea na watoto kuanguka ovyo. Nadhani si sahihi na shule sio eneo sahihi kwa haya anayofanya Masanja.

Naona ni busara kwa wenye mamlaka kuzuia hii kitu kufanyika katika mashule.
Anazunguka kwenye mashule ili kutesti kwanza nguvu zake kama ziko sawa ndo aingie kitaani mkoa kwa mkoa aje kuombea vidume na mikurumbembe ya mjini.
Maana akikurupuka kuingia mitaani bila kufanya testi ya mitambo anaweza kukutana na makubwa.!
Kuna jamaa aliibukaga kijijini kwetu miaka hiyo akajifanya nabii eti akawatukana wachawi wa kijiji kwamba yeye hawamuwezi haikupita hata siku tatu alikutwa uchi wa mnyama amelala mku.ndu juu chini ya mwembe wa shule ya msingi na inasemekana alichezea "kifiro"
 
Maombi kwa muktadha wa kujua na kueneza neno la Mungu sidhani ni tatizo. Hilo jambo lipo. Mashehe kwa wachungaji kufundisha n kuabudu mashuleni lakini hili ni tofauti. Huku ni kukemea mapepo kwa makanisa ya mitaani yafanyavyo. Nmeshindwa kuiweka hapa ile clip jaribu kuitafuta utaiona then utajua ninachozungumzia
Mkuu serikali haina dini ila inatambua uwepo wa dini na imani za watu, na ndo mana ata mashuleni kuna muda umetengwa maalumu na kuingizwa kwenye time table kwa ajili ya vipindi vya dini.

Apo sidhan kama kuna tatizo
 
Anazunguka kwenye mashule ili kutesti kwanza nguvu zake kama ziko sawa ndo aingie kitaani mkoa kwa mkoa aje kuombea vidume na mikurumbembe ya mjini.
Maana akikurupuka kuingia mitaani bila kufanya testi ya mitambo anaweza kukutana na makubwa.!
Kuna jamaa aliibukaga kijijini kwetu miaka hiyo akajifanya nabii eti akawatukana wachawi wa kijiji kwamba yeye hawamuwezi haikupita hata siku tatu alikutwa uchi wa mnyama amelala mku.ndu juu chini ya mwembe wa shule ya msingi na inasemekana alichezea "kifiro"
wazee wa kamati ya roho mbaya walifanya yao
😂😂😂😂😂😂
 
Kuna video imesambaa mtandaoni ikimuonyesha Masanja Mkandamizaji na vijana wengine nadhani ni wafuasi wake katika kanisa lake lile liko pale Leaders club. Clip inaonyesha wako ktk shule fulani nmeshindwa kujua ni shule gani exactly lakini kwa mazingira inaweza kuwa Arusha, anaonekana Masanja anaomba na watoto wanaanguka kimapepo.

Hii kitu sio sahihi kabisa kwa mazingira ya eneo la elimu na pia kwa mazingira ya watoto wadogo. Sijui uongozi wa shule waliweka wapi akili na fikra zao kuruhusu hili.

Binafsi nmeona ni jambo lisilo na mantiki kabisa. Sioni kabisa logic ya hii kitu kabisa. Inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia hapo baadae kwa wanafunzi na hata shule husika pia.

Tunajua jinsi baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu kutumia nguvu tofauti tofauti kujifanya wanakemea mapepo na watu wakianguka ovyo, huwa sijui lengo hasa ni lipi lakii kwa watu wazima wenye akili timamu ambayo hawajapelekwa pale kwa bakora, walienda kwa matakwa yao ni sawa.

Lakini kwa watoto wadogo kama wale hakika sio jambo sahihi kabisa. Unless hiyo shule iwe na shida fulani inayohitaji maombi kama yaliyofanywa na Masanja na watu wake.

Lakini kwa uchunguzi kidogo nimebaini ni kama tour huyu Masanja anafanya katika mashule kufanya anachokifanya. Hapa namaanisha kuzunguka katika mashule na kuombea na watoto kuanguka ovyo. Nadhani si sahihi na shule sio eneo sahihi kwa haya anayofanya Masanja.

Naona ni busara kwa wenye mamlaka kuzuia hii kitu kufanyika katika mashule.
attach hyo clip
 
Nini maana ya makanisa rasmi ? Wakati Yesu anaondoka duniani aliacha kanisa gani rasmi unalolijua wewe ? Umeingia chaka hakuna unachokijua kuhusu injili ya Yesu Kristo na siku za mwisho, maana alisema katika siku za mwisho injili itahubiriwa kila mahali ili uwe ushuhuda kwa kila mtu. Wewe kwa andiko lako hili huwezi kuzima moto wa injili. Maana ni kama moto uliotupwa duniani hakuna wa kuuzima. Narudia tena kukusihi kwamba mwamini Yesu ili awe Bwana na Mwokozi wako vinginevyo unapoteza muda tu.
Kwanza usinibwatukie. Nikuulize kitu labda utajielewa na kuacha kubwatuka. Wakati wa ukuaji wako (utoto wako) uliwahi kushuhudia uotaji wa haya makanisa mitaani kama ilivyo sasa? Kulikuwa na makanisa rasmi na yanajulikana. Nadhani jibu umelipata.
 
Back
Top Bottom