Hiki ndicho kinachotuponza sisi Yanga. Tuambiane ukweli tu

Kwa hiyo timu ikiingia kwenye mfumo isipigwe tano? Ulikuwepo wakati wanaomba kulegezewa? Unataka kusema hizo timu haziwezi kufungwa na Yanga?

Yanga ina kikosi kizuri sana na bado itaendelea kuimarika.
Kipindi Yanga inacheza shirikisho mpk fainali, Simba ilicheza mpaka robo fainal CAF champion league
Simba anacheza shirikisho fainali, Yanga ameishia makundi ya champion league.
Timu ya Olympic inayojivunia ubingwa wa medali, ligi ya ndani inafunga timu mpaka goli na 8 ila ikitoka nje, inapigwa 3-0 (Boulzdad), 2-0 (Al hilal).
 
Simba mlipigwa 5 na kwa miaka 4 hamjaokota point kwa yanga. Swali huwa mnalegea na kwa mnalegea?? Mfupa mnaofeli nyinyi eti mmtwishe fountain gate?? Shame on you
Kwa hiyo Yanga naye alilegea akajua ile sheria CAF bado ipo, ukitolewa CAF champion league, unaenda shirikisho. Matokeo yake mkaishia makundi
 
Unapata wapi muda wa kuandika pumba hizi?
 
Mwenye akili VS MBUMBU
Nguvu moja---Nyuma mwiko
Mwenyenchi---Mwananchi
Simba Queens--Yanga Princess
.
.
.
.
Mbumbu hayupo ila Mbumbumbu wapo alishawatambulisha baba yao mzee Aden. Hatupingi anachosema mzazi anayewajua watoto wake
 
Kuna timu kwa miaka mitatu inajivunia kupata kombe la kuunda group la whatsapp na kibegi kwenda mlima Kilimanjaro. Hii nchi kuna watu kama wamerogwa🤣🤣🤣🤣

Bzdad walipigwa 4 pia au unajisahaulisha? Na tukitaja historia kaize chiefs walishawapiga 5 wakiwa nafasi ya 10 kwenye ligi yao.
 
Bahasha fc wenye akili wanaongezeka
 
Una uhakika wewe ni mwana yanga?cz kwao kusema ukwel ni mwiko kama ilivyo kwa ccm
 
Pumba tupu. Yaani timu inamuogopa Bacca unaiita timu bora. Hivi ni Looser or loser?

Mashabaki pekee wanaobadirisha shirikisho kuwa champions league wanaposhiriki wao.Haya bwana 🤣🤣🤣
Subirini simba wamalizane na mechi za kimataifa ndio mtajua kama wanamuogopa huyo bacca au la, kama viongozi wenu walizoea kuwatuma wachezaji wenu wawaumize wachezaji muhimu wa simba kwa makusudi ili wasifike mbali basi safari hii wamegonga mwamba, kwa uchezaji huu wa yanga hakuna mchezaji wa simba anayewaogopa simba hii siyo ile ya mwanzo wa msimu ya kina mutale na mavambo ambayo mlihangaika kupata ushindi mkaishia kushangilia kagoli ka kujifunga tu
Yaani kuwakamia ndo mara nne? mfano wewe leo upigwe na mtu halafu uone amekubahatisha, ukakutana nae tena awamu ya pili akakupiga, ya tatu, ya nne bado uone anabahatisha tu! mi ni shabiki wa madrid ila kwa sasa nakubali barcelona ni bora zaidi yetu.
Sasa inategemea huyo mtu mnayepigana huwa anakukuta katika hali gani je kama kila mkikutana huwa hauko vizuri unaumwa unadhani atakuwa anakushinda sababu ya ubora, ni vile tu mliwakuta simba msimu uliopita walikuwa na kikosi kilichochoka na msimu huu walianza na kikosi kipya, halafu si huwa mnadai madrid ni bora sababu wana makombe mengi kuliko barcelona sasa mbona mnabadili kauli tena
Unapata wapi muda wa kuandika pumba hizi?
Hilo swali mlitakiwa muanze kujiuliza na kuulizana mashabiki wa uto kwanza
 
Wewe bwege kweli fainali ya shirikisho tulifaika kwa kulegezewa?
Huyu mtoa mada ni kolo wahed, Yanga haijalegezewa na timu yoyote ushindi inaopata ni ubora wa wachezaji na benchi la ufundi, simba haina mbinu mpira ni mchezo wa wazi tunaona wanavyostruggle hawafungi mpaka wasaidiwe na marefa,

Mahali tulipokosea uto mashindano ya kimataifa msimu huu ni upangaji mbovu wa timu, kudharau timu mbovu na kukosa intensity, msimu ujao uto tutafika mbali na kuondoa mada za kijinga kama hizi, kinachotakiwa ni wachezaji wa Yanga waoneshwe jinsi walicheza mechi na tp Mazembe taifa Ile ya marudiano, Ile mechi Yanga ilikaza kuanzia kukaba na kushambilia ilikuwa vita kamili to Mazembe hakuna kupumua na ni namna Ile Yanga inapaswa kucheza mechi zote za kimataifa kuanzia leo. Kocha mpya aoneshwe Ile mechi mwanzo mwisho, mi nilikuwa uwanjani na wanangu na niliona kuwa nina haki kushabikia Yanga, ni timu kali inaweza kushinda mechi yoyote wachezaji wa uto wakiamua kuwa kila mechi ni fainali na ushindi ni lazima, uwezo huo wanao, na ushahidi ni mechi za Simba, hata wajitutumue vipi lazima wakandwe na Yanga maana wachezaji wetu hawakubali kushindwa na kolowizard
 
Walikimbia kwa sababu Yanga hakufikia dau analotaka kolo. Wakaona bora wasicheze mpaka tutakapo kuwa tayari kufikia dau lao.
Yanga kama ni mbovu hiyo trh 8 mlikimbia nini?, Unaweza kumkimbia mnunua mechi?.
 
Hongera sana kwa kujitoa kwenye orodha ya wakosa akili, sasa mmekuwa watatu JK, Mzee Manara na wewe!
 
🚮
 
Kumbe unakubali kuwa simba ilikua mbovu, sasa mbona mlikua hamkubali kuwa yanga ilikua bora zaidi yenu! halafu km nyinyi wenye uwekezaji mkubwa mulikua hamutuwezi ndo mulikua munaamini hizi timu ndogo ni bora zaidi yenu na zina uwezo wa kutufunga, halafu kuhusu madrid ina uefa cl 15 unataka ifanane na barcelona yenye uefa 5! tena mwaka 2000 fifa waliipa madrid tuzo ya club bora ya karne.
 
Ndio labda kama hukuelewa hoja yangu mimi hoja yangu ni kwamba hatua ambayo yanga wanafika wakiwa na kikosi bora simba wana uwezo wa kufika wakiwa na kikosi dhaifu, yanga mlifika hatua ya fainali cafcc mkiwa na kikosi bora tena mna striker kama mayele lakini simba wamefika hatua hiyo hiyo wakiwa na kikosi dhaifu tena wakiwa wanajenga timu wakiwa na wachezaji wengi wapya, msimu uliopita pia hivyo hivyo yanga mliokuwa na kikosi bora mliishia robo fainali cafcl sawa na simba tu ambao walikuwa na kikosi dhaifu na bado na kikosi chao hicho hicho dhaifu wameweza kupanda kwenye ranks za caf na kuwa timu namba nne kwa ubora africa huku yanga yenye kikosi bora ikiwa haipo hata top ten.. tatizo siyo uefa tatizo ni kwamba kwa sasa madrid wameshafungwa na barcelona mechi nne mfululizo sasa kama hoja ni ubovu kwa sababu ya kufungwa mara kadhaa na mpinzani wako mkubwa basi maana yake ni kwamba madrid nao kwa sasa ni wabovu
 
Mi sio miongoni mwa wanaoamini kuwa hii simba ya sasa ni dhaifu na yanga ni bora, mpaka sasa zikikutana mi nawapa 50 kwa 50, halafu na spain kwa sasa barcelona ni bora dhidi ya madrid, ifike wakati tujifunze kuheshimu ubora wa mpinzani sio kuleta ushabiki tu.
 
Oohh kumbe mkibanwa vizuri huwa mnakubali ukweli sasa toka mwanzo ulichokuwa unabisha ni nini, si ulitoka kusema kwamba simba ni mbovu kisa imefungwa na yanga mara nne mfululizo na madrid ni bora kisa ina makombe mengi kuliko barcelona, ndio mjifunze kwamba ubora wa timu huwa unaamuliwa na mambo mengi na siyo vigezo mnavyoviweka mashabiki wa yanga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…