So ulitaka kila mwaka tufike unapo taka wewe?
Oohh sorry nilisahau kumbe malengo yenu yalikuwa kuingia makundi, maana huko kwingine ninyi hampataki bali napataka mimi sasa, halafu kwa hali hiyo ndio mnajifananisha na simba aise
Tangu lini timu bora ina wasiwasi kuingia vitani, mbona Yanga ilipambana ikiwakosa Aucho, Pacome na Yao Yao na iliupiga mwingi tu kule South Africa hadi Makolokolo mlibaki mmeduwaa kama mapaka shume yanayokata roho?
Makolokolo mshukuru mmekutana na vitimu visivyoeleweka ndiyomaana mmefika hapo.
Makolokolo = Kamdomo
Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Yani mabeki wenu kina Bacca wanacheza jihad halafu mnasema eti timu bora haina wasiwasi wa kuingia vitani, lengo lenu wachezaji wa simba waumie ili washindwe kusonga mbele, halafu mjitoe ufahamu mseme simba ni wabovu kumbe ukweli mnaufahamu
Tatizo liko wapi ninyi subirini simba wamalizane na mechi za kimataifa halafu waje kucheza derby wakiwa full mkoko mkiwafunga hapo ndio mje mtambe mnavyoweza, halafu unasema yanga ilipambana ilipowakosa kina Aucho unaongea kana kwamba yanga walikuwa na option ya kuahirisha mechi, ila wakaamua kuenda kucheza hivyo hivyo tu
Wakati unajua kabisa timu haina uwezo wa kugomea mechi za caf maana inajua kitakachofuata, mbona hata simba walishacheza na timu ngumu huku wakiwakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu, na bado wakatoboa sasa hapo cha ajabu ni kipi
Mwaka jana ulimaliza nafasi ya tatu ukashindwa kushiriki klabu bingwa mwaka huu matokeo yake ukadondokea shirikisho kati ya wewe na Yanga iliyoshiriki klabu bingwa nani mbovu?
Wewe kupita robo fainali sio maajabu kundi lako halikuwa na timu ngumu kuliko yanga pia hata uko robo fainali ulitoka kwa aibu kwa kuliwa nje ndani na al akhly.
Yanga katolewa kwa penati huku akidhulumiwa goli lake halali kabisa yes ni goli halali kabisa.
Sasa hapo hipi ni timu bora?
Yanga kakufunga mara 4 mfululizo na mara ya tano ukakimbia mechi!
Yanga ndio bingwa mtetezi wa ligi akiwa amechukua mara 3 mfululizo.
Sasa kwa facts hizo simba anaanzaje kuwa bora kuliko yanga?
Sasa mbona unarudia yale yale niliyotoka kukuambia kweli eymael ajengewe sanamu lake, si nimetoka kukuambia hapo kwamba simba msimu uliopita walikuwa na kikosi kibovu ndio maana wakaishia nafasi ya tatu na kuangukia shirikisho msimu huu, lakini pamoja na huo ubovu wa simba bado wakaishia robo fainali cafcl kama yanga tu ambao walidai wana kikosi bora
Lakini pia simba hii ya msimu huu ambayo ina wachezaji wengi wapya na inajenga timu imefika fainali cafcc kama yanga tu ambao wao walikuwa na kikosi bora, kwamba unataka kusema msimu uliopita kundi la simba lilikuwa jepesi sana ndio maana wakapita kuenda robo, hivi mashabiki wa yanga mbona mnapenda kujitoa ufahamu haya vipi na msimu huu ambao mlikuwa kwenye kundi jepesi kuliko yote mmeishia wapi
Hayo mambo ya kutolewa kwa penati wala siyo ajabu hata simba waliwahi kutolewa kwa penati na wydad na mkawacheka na kusema ni wabovu, tulikubaliana kufa ni kufa tu hakuna kufa kiume wala kufa kinamna gani, kuhusu kuwafunga simba mara nne mfululizo hivi una habari kwamba msimu huu barcelona ameshamfunga madrid mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha 5-2 sasa sijui unataka kusemaje
Eti Simba ikifungwa na Yanga inakuwa imekamiwa ila ikishinda ni kwa sababu ya ubora. Derby yoyote ni kwa ajili ya wanaume sio wavulana wavaa nepi wanaolialia. Na kama mnaendelea kuiona Yanga sio bora mtafungwa sana.
Kuhusu Dube mimi nikiwa shabiki na mpenda mpira niliamini kila kocha aliyempanga hakuwa mjinga aliona umuhimu wake lilikuwa swala la muda tu Ukiona foward hakuna clear chances anazozipata na kukosa huyo sio forward. Huenda anajificha nyuma ya mabeki wa timu pinzani kukwepa lawama endapo atakosa. Positioning ya Dube uwanjani inawapa tabu sana mabeki na ndio maana ana assist nyingi pia. Ni sawa na hata kwenye timu yenu ninavyoamini Ateba ana uwezo mkubwa kuliko striker refu. Ateba hana tofauti sana na Mugalu. Anachohitaji ni number 10 wazuri na wale winga ambao watafuatilia anapopokea pasi na kuwahold mabeki wawili wamsaidie. Dube is my man sijawahi kuwa na wasiwasi naye.
Kusema ana magoli ya offside ni utetezi wa striker wenu na magoli ya penati kwa kuwa dube hana. Unaweza kutaja kuna magoli mangapi ya offside ya Dube kama macho yako yanafanya kazi?
Hayo mashindano mnayoenda fainali Yanga ndio timu ya kwanza kwenda fainali kwa timu za Tanzania. Sasa unaposema timu inaishia makundi sijui unazungumzia mashinadano gani.
Haya mashindano mnayojivunia sasa kufika fainali ndio mliyoyaponda Yanga alipofika fainali mkisema nyinyi sio level za kufurahia mashindano ya shirikisho. Leo mnayaona kama mafanikio. Mzee Aden hakukosea kuusema uwezo wenu wa kufikiri.
Ofcourse haya mashindano ya cafcc wakati mnacheza ninyi yalistahili kuitwa loosers cup sababu yalikuwa ni mashindano ya walioshindwa klabu bingwa na kudondokea shirikisho, ila kwa sasa siyo ya loosers kwa sababu timu zinashiriki moja kwa moja kutoka kwenye ligi zao na siyo baada ya kufeli klabu bingwa, nashangaa wengine wanasema eti ni mashindano ya malooser toka kwenye ligi zao kama ni hivyo huko cafcl si wangekuwa wanachukua mabingwa wa ligi pekee mbona wanachukua hadi walioko kwenye nafasi za pili
Sasa Mbali wapi huko mlipo fika ambapo Yanga haija fika?
Kwenye caf ranking timu lako linashika nafasi ya ngapi au kama hamjui umuhimu wa timu kupanda rank muulizeni msemaji wenu, yanga mna consistency gani kimataifa hadi mjifananishe na simba mmeingia robo fainali cafcl msimu mmoja tu msimu uliofuata mkatema bungo, simba wamecheza hiyo robo mara tano mfululizo walau wamevuna pesa za kutosha toka kwa caf baada ya kufika kwenye hatua hiyo