Hili la kifo cha Dkt. Faustine Ndugulile limeniumiza sana, shida ni nini?

Hili la kifo cha Dkt. Faustine Ndugulile limeniumiza sana, shida ni nini?

Viongozi hawa nao. Wanaiba. Wanalipana mahela mengi na marupurupu kibao. Wanakula vinono. Ni kutoka kiyoyozi home mpaka kiyoyozi cha kwenye vi eite. Mazoezi hata yale ya kutembea tu hakuna. Wengi wana BP, cholesterol na ni pre-diabetic. Insulin resistance imeshaanza. Lakini wao wanatanua tu kwa nyama choma na vinywaji vya kila aina.

Na wengi wao ukiwaona sura zao hazina nuru. Likely wamo kwenye gridi ya taifa na wanaishi kwa kula njugu mawe. Na ubaya wa njugu mawe ni kwamba siku likibumburuka linabumburuka kweli maana inafika mahali viungo vinachoka. Na culprit mkubwa ni figo, ini na hata moyo.

Mbali na sarakasi za hata kuondoana wao wenyewe kwa wenyewe kimya kimya lakini wengi wao wanaishi maisha ya hatari sana maana kwa mwanaume ukivuka 50 inabidi uwaangalie sana maadui hawa watatu - cholesterol, Hypertension na diabetes. Na ikibidi ubadilishe kabisa mtindo wa maisha...

Anyway. Safari yetu wanadamu hapa duniani ni fupi; na kila mtu ni kwa zamu yake. Apumzike salama daktari huyu msomi. Kama taifa tumepoteza mtu wa muhimu sana kabla hata hajashika nafasi yake ambayo ingemtambulisha yeye na nchi yetu. Na jana Yanga walipigwa magoli mawili. Na leo Simba wanacheza. Ndiyo mjadala wa kitaifa. Mengine yote hayana maana. Hili nalo litapita. Na maisha yataendelea tu.

Maisha!

Hata sijui yana maana gani!

Fumbo tata ajabu!
Sahihi kabisa Kaka
 
Mkuu nadhani kupelekwa India au SA siyo hoja,lakini umma ungekuwa unajulishwa tatizo ni nini kama ulivyosema kwenye hoja yako.
Na inavyoonekana huenda Mawazi na Wabunge na viongozi wengine wa taasisi mbali mbali wanatembea wanaumwa kuliko tunavyofikiri.
Na huenda walio wengi ni HIV victims ndiyo maana wanaogopa kutibiwa katika hospitali zetu!
Sawa inawezekana.
 
Wasiwasi wangu ni maneuver yalifanyika pale pale Congo, kwenye ulimwengu wetu tiba na Afya, human being ni very weak creature , na tunaijua anatomy ya human being exactly tunavoijua body smell zetu
Kifo cha human kinaweza kuwa induced slowly and within a specified period of time , as you suggested ulinzi wake ulipaswa kuwa priority kwa Taifa, shida kubwa CCM hawana kitu vichwani ni anaupiga mwingi ameweza ameshinda uchawa uchawa

West , North Africa ni very cruel creatures , I know them and some of them ninafanya nao
Kazi, selfishness

Faustine hakuwa na elimu kubwa kuwazidi wao, and he had very few published papers , while others walikuwa na more than 100 papers ……but akashinda kwa jitihada za URT, hi ilikuwa ni red light tumpe ulinzi.
Na ulinzi sio mapolisi, no one deal na gun now days , Ulinzi wa kisayansi sijui kama naeleweka

Tunasema tuna maafisa vipenyo, maafisa vipenyo are not trained to be smart but Dumb , ni kazi kupeleka umbeya here and there .walipaswa kuona hiyo post ina maslah makubwa kwa taifa, they should be ahead of time na kuuona ukweli. Sio Afisa kipenyo anazunguka na boda boda kufuatilia maisha ya watu , ni kuwafanya kuwa wajinga zaid. Kila kitu ni Sayansi and technology

Hapo TZ ni watanzania wangapi wapo kwenye makampuni ya UN , WHO ….. kufika huku ni kipengele kwa sababu hatuna watu kwenye decision making ndani ya hizo area. Utakuta UN ipo TZ but waajiriwa wengi sio watanzania

DG WHO was a lot na kila mwaka anapewa chances za kuajiri watanzania wenye uwezo, Kama vile Rais anavopewa viti maalum na kuteua

Endeleeni kufanya Siri na kupeleka watu india na South Africa

Faustine Ndugulile, A DG-WHO that never was
Unaonngea point nzito sana yani Hadi inauma.
Tuaishi nao mtaani hawawazu vitu nyeti kiasi hicho.... Upeo mdogo sana sifa nyingi
 
Moja ya sehemu ambazo sitamani kusikia kiongozi wenye maono ameenda kwa matibabu ni India na SA, these places ni very corrupt na system govt za nchi nyingi ikiwemo Tanzania. Kama kweli wewe ni mtu potential and public figure , those are not places to go . Bora uende hapo MNH.
Je unadhani hapa wahusika watakuelewa na utaeleweka kweli?. Wakati protokali inamruhusu kwenda matibabu nje ya nchi?
 
Mpaka mtu aende india ina maana alikuwa mgonjwa wa muda mrefu. Lolote lingeweza tokea. Lakini kwa nini wanakombilia sana india. Wajifunze tundu lissu kidogo ambaye hakwenda india baada ya lisasi zote zile. Hakwenda india bali alienda kwingine kabisa na penye uhakika.
Hizo ni assumption mtu anaweza kuwa na case ya mda mfupi tu na akakimbilia huko
 
Mke wa Faustine ambae ni Program Manager pale NBTS, Magdalena Swai nilifanya nae kazi kwa karibu akiwa kama Program manager NBTS na dada yangu mkubwa huku mm nikiwa Junior pale Ocean Road Cancer Institute na kabla sijakimbilia Ottawa, Canada na kuachana na Utumishi wa Umma.

Faustine kuwa DG-WHO Africa, ni fursa na Watz wengi wangeingia huko , ila jamaa amelala kabla hata ya kukalia kiti cha enzi . kuna thin layer kati ya mafanikio ya ndoto yako na mstari wa kuzimu, a very thin layer. Carefully !

Cha kusikitisha kabisa ni haijulikani Faustine ameanza kuumwa lini na ameumwa nini. Ukiwa kiongozi na nyie viongozi tabia ya kufanya siri ugonjwa wenu hata mnapoumwa kikawaida muwe sana makini, wakati mwingine watu wanatembea humo humo, ukishakuwa kiongozi na public figure vitu kama magonjwa sio siri, ijulikane unaumwa nini.

Faustine ameenda India no one knows , tunakuja kupewa taarifa za Maiti, Mafuru kaenda India, tunakuja kupewa taarifa za maiti.

Moja ya sehemu ambazo sitamani kusikia kiongozi wenye maono ameenda kwa matibabu ni India na SA, these places ni very corrupt na system govt za nchi nyingi ikiwemo Tanzania. Kama kweli wewe ni mtu potential and public figure , those are not places to go . Bora uende hapo MNH.

Magufuli amepekekwa Hospitali , mkafanya siri, tunakuja kupewa info za maiti, yaani haijulikani mnauliwa au mnakufa. Mbona wenzetu nje kiongozi akiumwa inajulikana na inajulikana ameenda wapi, hata JK alipoumwa tupo tulioenda pale Hopkins kumcheki! This is how a leader should be , sio unafanya fanya siri then wanakuua huko unaletwa maiti na kuwekwa upande wa mizigo wa ndege.

wanajua wazi watz wamezoea tu kupewa taarifa za msiba. Hii ni mbaya sana you guys need to change. Kuna viongozi wengi sna ni wagonjwa na tumewapa nafasi kubwa za uongozi na mpo na watu wanatamani hizo nafasi au ni maadu but mnafanya siri hali zenu mnawasafirisha kwa siri then mnakuja kutupa taarifa za msiba !

Kama mnawakatishana uhai je?

Post ya Faustine ilikuwa na upinzani mkubwa sna, na fitna tulizozifanya kama taifa zinajulikana…….na kwa umoja wa taifa akashinda, lakini mapambano hayaishi hapo, kuna some people loses the battle but not war …… tulipaswa kuendelea kumlinda Faustine ….. worst enough na kwa usiri wa hovyo mkaja kumpeleka India, a very corrupt places kwenye system za govt nyingi.

Moja ya benefits alizokuwa anakwenda kupata ni salary not less than 130M on monthly , international health insurance, watoto wote wanasomeshwa majuu, wife analipwa 60% of the salary yake, anapewa nafasi 14 kila mwaka za kuajiri from his country, lots of benefits with the country recognition , it was not just a post for him , it was a post for the country.

Kuna kitu hakipo sawa kwenye hilo taifa!

Poleni watanzania, tumenyang’anywa tonge mdomoni.
Umewaza kitu kama mimi ila vidole vyangu vilikuwa vizito kuposti!
 
Wasiwasi wangu ni maneuver yalifanyika pale pale Congo, kwenye ulimwengu wetu tiba na Afya, human being ni very weak creature , na tunaijua anatomy ya human being exactly tunavoijua body smell zetu
Kifo cha human kinaweza kuwa induced slowly and within a specified period of time , as you suggested ulinzi wake ulipaswa kuwa priority kwa Taifa, shida kubwa CCM hawana kitu vichwani ni anaupiga mwingi ameweza ameshinda uchawa uchawa

West , North Africa ni very cruel creatures , I know them and some of them ninafanya nao
Kazi, selfishness

Faustine hakuwa na elimu kubwa kuwazidi wao, and he had very few published papers , while others walikuwa na more than 100 papers ……but akashinda kwa jitihada za URT, hi ilikuwa ni red light tumpe ulinzi.
Na ulinzi sio mapolisi, no one deal na gun now days , Ulinzi wa kisayansi sijui kama naeleweka

Tunasema tuna maafisa vipenyo, maafisa vipenyo are not trained to be smart but Dumb , ni kazi kupeleka umbeya here and there .walipaswa kuona hiyo post ina maslah makubwa kwa taifa, they should be ahead of time na kuuona ukweli. Sio Afisa kipenyo anazunguka na boda boda kufuatilia maisha ya watu , ni kuwafanya kuwa wajinga zaid. Kila kitu ni Sayansi and technology

Hapo TZ ni watanzania wangapi wapo kwenye makampuni ya UN , WHO ….. kufika huku ni kipengele kwa sababu hatuna watu kwenye decision making ndani ya hizo area. Utakuta UN ipo TZ but waajiriwa wengi sio watanzania

DG WHO was a lot na kila mwaka anapewa chances za kuajiri watanzania wenye uwezo, Kama vile Rais anavopewa viti maalum na kuteua

Endeleeni kufanya Siri na kupeleka watu india na South Africa

Faustine Ndugulile, A DG-WHO that never was
Mkuu umeongea kwa umakini mno na kupangilia hoja yako kwa weledi. sisi kama Taifa tumepoteza hazina kubwa sana, Mungu ampokee Ndugulile
 
Hujasoma vema post, hupasw kufanya lobbying, one of the benefits ni unapewa upendeleo wa watu wako being a DG WHO

Hiyo ni one of his responsibilities ndan ya job description yake
Yaani ajira 12 ndio benefits za nchi? Nilidhani ingetupa connection ya kudivert miradi ya WHO/US-CDC kuja Tanzania!!

Mkuu miradi mikubwa duniani ni lobbying ona Kenya wameshawishi taasisi nyingi za magharibi kufungua African offices hapo Nairobi. Hawaji hivi hivi ila kwa connections kupitia diaspora wao kwenye hayo mashirika.

Sisi tunakazania eti ajira 12 na mshahara wa 130M!! Kwamba huyo Ndungilile kaenda WHO kisa mshahara? Kwani pesa walizoiba hao CCM si ana mabilion mpaka sasa!! Mshahara ni nini kwake?
 
India iko overrated sana na Watanzania

Mtu una hela na mtumishi mkubwa tu serikalini eti unaenda India

Huwezi kusikia kiongozi mkubwa wa mataifa ya Ulaya, Far East Asia, Latin America au Middle East ameenda India

Huu utamaduni wa kwenda India sijui tumeutolea wapi?
Kuna kit hukielewi ndugu yangu..kwann wat hua wanapelekwa India zaid ya nchi zingine izo ulizozitaja.
Nchi za Dunia ya tatu hii zinamambo mengi sana mtu ana ukimwi ila sio ukimwi ngoma ngum
..,Sasa waindi kama ni vitu havieleweki wanaeka sawa kwanza mazingira ndo tunaendelea na tiba za kizungu.
 
Back
Top Bottom