Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,459
- 100,799
Basi mimi sikuwahi kuamini kuwa kuna Watu wanalipwa ili waitetee CCm mitandaoni! Kumbe ni kweli? Sasa mbona mmefanya mambo "mengi mazuri" kuna haja gani tena ya kuwalipa vijana wawatetee? Kwanini mpoteze muda na resources kuwaweka watu wawateee mitandaoni? Chadema mbona hawafanyi hivyo?Malengo yetu ya kuweka watetezi mitandaoni tokea wakati wa JK na Nape yalikuwa ya msingi na muhimu.
Bahati mbaya recruitment imekuja haribiwa sana na Polepole kuweka watu wajinga. Huwezi kumtumia mtu mjinga kukutetea mbele ya wenye akili.
Upinzani wapo wapuuzi wengi, lakini wengi ni vijana wasomi na wanaotumia akili hivyo kushindana nao kwa ujinga kama wa hawa wapuuzi wa Pole pole kama Bia yetu ni kujiaibisha tuu.
Lakini hata hivyo CCM bado tuko Imara, tukisafisha huu uchafu uliopo nafasi ya kuweza kuongoza tena bado ipo
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nadhani CCM hamjiamini, mna kila kitu lakini bado hamjiamini na wala hamuaminiani! Kuna dhambi inawatafuna! Huwezi kuniambia au kurudia maneno yale yale kila siku ya kusafisha uchafu, uchafu gani huo ambao hauishi? Nini chanzo cha huo uchafu? Kama wenyewe kwa wenyewe hamuaminiani, mnawezaje kuaminiwa na wananchi? Uimara wa CCM Ni upi huo unaousemea? Wa kutukana na kubeza kila hoja mitandaoni??
Kwahio, unanithibitishia kuwa kama mnaweza kuweka mamluki mitandaoni dhahiri hata wale waliounga juhudi nao mmewaanunua! Sijawahi nasema sikuwahi kufikiria kuwa CCM pamoja na kukaa madarakani miaka yote hio mnaweza kuwa na siasa za kishamba kiasi hiki. Kwahio wakija kutukana kumbe they are paid? Bia yetu stroke na wengine!
Chakaza tpaul Sky Eclat @ethrocyte na wengine njoo muone confession ya mwana CCM! Naapa mimi nilikua najua buku saba fc ni joke kumbe ni kitu cha Kweli? Wazalendo feki wa kulipwa.
Mshangai kama hawa vijana wanalipwa ili wawatetee kuna siku watalipwa ili waiuze nchi, mark my word.