Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

H

Wawekezaji wanakuja kujitafutia sisi ajira ni mojawapo ya mahitaji yetu. Yafaa rais ashauriwe vizuri sio twende kwa matakwa ya wawekezaji ambao hata tusipopata kitu kama taifa kwenye uwekezaji wao sio kitu kwao. Wale ambao hawataki sheria na taratibu zetu waachwe bila majuto. Ukweli tunahitajiana sio tujifanye mradi mwekezaji tunamkumbatia.
Pia wapo wawekezaji ambao hutaka walipe watu wao kwa fedha kigeni.

Hatukatai hilo ila ni lazima kila detail iwe wazi ni watumishi wangapi wamo kwenye vitabu vyao vya accounts na wanalipa kodi stahiki kama ilivyopangwa na TRA.

Wengi wao hukwepa hapa penye kodi.

Makampuni kama Amazon wamepigwa faini ndefu kwa kukwepa kulipa kodi khasa Corporation Tax ambayo hutaka kuwepa maana ndipo penye faida kubwa.
 
Hopeful nia ya mama ni njema na wahusika waliopo kwenye authorities watayachukua maangalizo haya na kuyafanyia kazi.
 
Hakuna nchi duniani inayodili na utumikishwaji wa kazi za nyumbani
Una hakika na unachosema?

Hawa watanzania karibia wote waliosoma nje wamefanya kazi hizi unazoziita za kutumikishwa. Huko nje kilichowekwa ni minimum pay per hour, ukimuajili mtu lazima umlipe kiwango hicho.

Kufanya kazi za nyumbani sio utumikishwaji kama unavyodhania kwa mujibu wa sheria, kinachogomba unamlipaje. Ndio maana hapa Tanzania kuna chama cha wafanyakazi wa majumbani kinaitwa nafikiri CHODAWU.
 
Pia aruhusu vijana wakatafute Kazi nje Ili wakuze uchumi wa familia zao.Jiwe aliwazuia kutoka nje Ili wabakie ndani kuisoma namba Ili wamuabudu.
 
Bei ya pasipoti ipungue walau iwe elf 70 Ili wengi waweze kumudu.
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Raisi yupo sahihi kabisa. Watu kutoka nje wanaongeza sana ajira hapa Tanzania. Mara nyingi ajira zao ni rasmi. Wao huajiri wapishi, walinzi wabustani nk. Hawa Watanzania hupata ajira rasmi. Mimi ningeenda mbali na kuruhusu watu wa nje wawe na access hata ya kustaafu na kuishi hapa. Fikiri Mmarekani anayelipwa dola 5,000 kama retirement yake na anaishi Mgamwa pale Iringa Kijini. Fikiri huyu ataajiri wangapi. Na hiyo fedha italeta maaendeleo kiasi gani? Fikiri tukiwa na wastaafu 5000 kwa Tanzania nzima!
Kama kuna Watanzania wanapenda kuishi Ulaya pia wapo Wazungu wanapenda kuishi Tanzania. Tubadilike na tubadili sera zetu.
 
HUYU MAMA SOON ANAENDA KUTUUZA WATANZANIA

Soon Tz itakuwa KAMA LIBYA Ee Mungu TUNUSURU.
 
Allocation ya nafasi zenye kuhitaji wageni yawe na UHALISIA kwa maana ya kuwa kweli mtaalamu husika anahitajika. Sio mtu analeta MWALIMU WA CHEKECHEA kuja kuwa HR wa kampuni.
wa kudeliver.
Hakuna tatizo kampuni private mbona kawaida tu mke wa boss kuwa HR wakati darasa la saba.Kuajiri na kuchuja wataalamu kutumike kwa wageni waomba ajira Kampuni za umma au serikalini au kwenye makampuni yanayouza hisa soko la hisa la Tanzania
Lakini kama mhindi Patel au mchina hu ng anataka kuanzisha duka la mabasi yake ya Yuyong au kiwanda mwachie mwenyewe alete awatakao wewe mtajie idadi tu alete wangapi basi
 
Hata hao watano baada ya miaka 3 walikuwa wanasumbuliwa kurenew vibali.

Muwekezaji akija na wafanyakazi 15 kutoka nje halafu akafungua mradi ukaajiri watu 1000 na kodi analipa hapo kuna shida?

Mama ameshauri akili itumike sio mabavu.
WATU WENYE AKILI KAMA WEWE MPO WACHACHE SANA TANZANIA.
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
Tatizo la RUSHWA mara nyingi linaletwa na Wawekezaji pale wanapotaka kuingiza wataalam zaidi ya watano!! Wachina ndio wamekithiri kwa kupewa vibari vya kazi vya magendo kwani kwenye uwekezaji wao unawakuta wamejazana hata kwenye gereji za kunyoosha magari!! Sheria ikifuatwa hakuna tatizo, lakini watendaji wanaoshuhurikia kutoa hivyo vibari ni lazima wawe waadirifu sana.
 
Hakuna tatizi kampuni private mbona kawaida tu mke wa boss kuwa HR wakati darasa la saba.Kuajiri na kuchuja wataalamu kutumike kwa wageni waomba ajira Kampuni za umma au serikalini au kwenye makampuni yanayouza hisa soko la hisa la Tanzania
Lakini kama mhindi Patel au mchina hu ng anataka kuanzisha duka la mabasi yake ya Yuyong au kiwanda mwachie mwenyewe alete awatakao wewe mtajie idadi tu alete wangapi basi

SHERIA IKO WAZI JUU YA HILO NI SUALA LA UADILIFU WA WATENDAJI WANAOTOA WORKING PERMITTS TU!!!
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
Kwa Mwendo huu wa mama sioni sababu za wewe kugombea urais 2025! Cha kufanya lile DESA LAKO mpe mama afanyie kazi!
 
Nikimnukuu Rais kasema mtu akiomba vibali vya kazi apewe sababu ndo watu Mwekezaji 'anaowaamini'.

Binafsi sina shida kabisa na hili iwapo tutafuata sheria zinavyotaka.

Sheria inasema muwekezaji anaruhusiwa kuja na wageni hadi watano akija na uwekezaji wake; wengine watatakiwa kuajiri wazawa.

Hii sheria haina shida iwapo inafuatwa.

Na sheria inasema iwapo kutakuwa na nafasi ambayo hakuna mzawa anaiweza anaruhusiwa kuongeza mgeni Kwa nafasi hizo.

Nahofia kauli ya Rais Samia inaweza tafsiri kuwa sasa ni ruksa kuajiri wageni as many as you want, bila idadi.

Ni vizuri Mama akashauriwa kutoa maelekezo Kwa mujibu wa sheria.
mkuu hii inaweza kuwa tafsiri yako. najua rais ana timu kubwa sana na wapo watafanya tafsiri sahihi ambazo ndo zitafanyiwa kazi. jamani tumpe ushirikiano 100%
 
Kwani kuna shida gani mwekezaji akipewa idadi tu ya wageni anaopaswa kuwaajiri???

Kama akiambiwa aajiri watu 5 au 10 tu wa kigeni kuna Tatizo gani????
Tatizo si idadi sabbu tayari ipo kisheria.
Tatizo ni urasimu wa kupata hivyo vibali vya kazi vya watu ambao idadi yao iko kisheria
 
Kwenye Hili swala Mama yetu Awe Makini Sana.Na Mimi nitamshauri kwa nyanja Tofauti na ni vitu ambavyo kama Intelligensia yake ikifanyia Kazi itavitambua.
1.Makampuni mengi hao watu wa nje wanafojiwa Sana Vibali kutoka Uhamiaji.

2.Makampuni mengi yanawapa watu wa nje Pesa ya posho tu yaani hela cash au kwenye account hizi ni Pesa za Kitanzania.Ila Mshahara na Marupurupu ya Wafanyakazi wa kigeni mengi yanaingizwa kwenye Account zao za nje kama Pesa za Kigeni na hapa Serikali inapoteza kodi za Kutosha Sana.

3.Kama Serikali inataka kuwasaidia Wazawa na kulinda Ajira zao Basii Sheria ya Awali izingatiwe Ili kulinda Ajira za Watanzania Wengi.

4.Watanzania Wengi wanalipwa Ujira mdogo Sana ukilinganisha na Hao Wafanyakazi wa Kigeni,ambao wengine KWA taarifa za Haraka Haraka Huwa ni vilaza tu huja hawajui kitu na Watanzania ndio hushiriki kuwafundisha.

5.Ukiruhusu Wafanyakazi wa Kigeni na wengi kwenye Taasisi Moja au Mwekezaji basii utegemee Wafanyakazi wa Kitanzania/Raia wa Ndani Kunyanyaswa Sana.Kwani Mifano Tunayo.

Maoni yangu ni Haya.
 
Hakuna Mwekezaji ataleta watu kutoka nje kama atapata reliable work force. Kwa hiyo let’s stop beating around bush and ask our selves why should an investor bring expensive labor force from abroad??
Hawafanyi hivyo kwa taarifa yako. Mtambo wa Songas kuna mhindi alipata contract ya kujenga na alileta wahindi wengi sana ambao walikuwa wanafanya kazi ndogo ndogo ambazo wazawa wangeweza kuzifanya. Na wengi walipangiwa nyumba mitaani ndiyo maana tunajua hili. Kuna ambao walikuwa wanakaa karibu na ninapokaa. Uliza wanaokaa kinyerezi wataconfirm hili..
 
Back
Top Bottom