Hili la vibali vya kazi Rais ashauriwe zaidi

The cure shouldn't be worse than the disease itself.
 
Mna ongea maneno mengi sana!

Jibuni swali hili kuna shida gani Mwekezaji akawekewa kiwango tu cha watu wa kuajiri??? Na mamlaka zikajikita hapo tu???

Mbona TFF wamefanikiwa kwenye suala la wachezaji kutoka nje ya Tanzania na ufanisi tunauona?? Kwa nini ishindikane kwingine???

Mama yuko sahihi , Wawekezaji wawekewe idadi tu ya kuajiri wageni, na mamlaka zijikite kwenye kuangalia kiwango tu cha wageni na sio kusema huyu unaweza kumuajiri huyu hauwezi
 
Hapa uko Sahihi Ndugu yangu.Na mimi nasemea hilo.Ila Uhamiaji Huwa tatizo sana
 
Nia ya Rais ni njema sana ila sio kila mwekezaji ni mwekezaji wengi ni matapeli tu wanatumia loopholes za uwekezaji kujitajirisha,

1. Taarifa wanazotoa sio sahihi.

2. Wanatumia ardhi yetu kuchukulia mikopo na kufanyia mambo yao mengine.

Urasimu unakuwepo kwani mamlaka wakati mwingine zinataka muda ili kuprocess taarifa wanazopewa na the so called wawekezaji, malalamiko yote hayo ya urasimu naamini machache sana ni valid ila wengi wa wawekezaji sio wenye nia ya dhati ya kuwekeza ni wapigaji tu.
 
Hivi Lazio ndogondogo ndio kazi gani?? Private sector investors don’t do charity. Waliona kuna tatizo kwa wazawa kuwa mzawa sio kigezo cha kupata kazi uwe na ujuzi hata kufagia watu huenda shule kufundishwa jinsi ya kufanya usafi.
 
Mimi sipingi kauli
Natamani iwepo clarification..
Je wageni waajiriwe bila kujali idadi?
Au usimamizi uwepo kama enzi za JK..
Mama hapa kakosea sana,Localization imefanikiwa sana kipindi cha Magu,kuna watanzania wengi waliokuwa na sifa hasa za kuwa CFO's ilikuwa haiwezekani siku za nyuma lakini miaka ya Magu iliwezekana,Sheria inaonyesha lazima uonyeshe succession plan ya mtu unayemleta
 
Moja ya motives za foreign direct investment (fdi) ni availability of raw materials na cheap labour in third world compared na mishahara ambayo wangemlipa mtu kutoka dunia ya kwanza...
Mwekezaji sio mjinga kuacha kuajiri wazawa wa hapa ambao mishahara yao ni mara nne hadi tano cheaper kuliko wa kutoka nao kwao..
 
Mimi sipingi kauli
Natamani iwepo clarification..
Je wageni waajiriwe bila kujali idadi?
Au usimamizi uwepo kama enzi za JK..
Mama hapa kakosea sana,Localization imefanikiwa sana kipindi cha Magu,kuna watanzania wengi waliokuwa na sifa hasa za kuwa CFO's ilikuwa haiwezekani siku za nyuma lakini miaka ya Magu iliwezekana,Sheria inaonyesha lazima uonyeshe succession plan ya mtu unayemletaunajua
Unajua watendaji wa hii nchi walivyo🤣🤣🤣
 

Siamini sana kuwa wewe, hao wengine wenye mashaka pamoja na mleta Uzi kwamba mko smart sana kuhusu suala la vibali ZAIDI ya taasisi ya urais ya Mama yetu SSH.
Mama SSH pamoja na wasaidizi wake wanajua sana negative risks (threats) katika suala zima la vibali na nini wafanye (Risk Management).
Mama SSH ameongea kwa kifupi sana kuhusu vibali hivi na hajasema kuwa vibali vitolewe kama njugu bali ameitimisha kwa kusema kuwa sheria zifuatwe.
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
It is on one side and not true on the other side. Kwa sababu ni jukumu is kila nchi ku promote welfare ya watu wake na kutoa nafasi za kazi as much as possible.
Huko ulaya wanacho fanya ni kuwapa odd jobs wageni ambazo wazawa hawataki kuzifanya.
Wanakuwa na policy ambazo hazikuwezeshi wewe kupata kazi zao e.g. umesomea u daktari Muhimbili, huwezi kupata kazi za u Dr kwao, au CPA, na hata u engineer, na ukipata kwenye construction industry utakuwa down the ladder na kipato chako kidogo.
Lakini wao wakija hapa wanapewa mshahara mkubwa, na other fringe benefits wewe nchi kwako ukiajiriwa hata kama ni mtaalamu mshahara wako utakuwa so discouraging, tatizo unakuwa huna option.
 
Na hii sera ya vibali vya kazi sio ya Magufuli ni ya Baba wa Taifa, na Baba wa Taifa alikuwa na karama nyingi mojawapo kusoma vizuri, exposure, busara ya kujua kuishi na watu wengine iwe dini tofauti, kabila , utaifa, Rangi, na dhana ya kuindeleza nchi kiuchumi na watu wake pia. Sio nchi inafanya vizuri lakini watu wake wapo hand to mouth .
Ana hitaji kupigwa shule juu ya hili, internally and externally, hata kwa mataifa ya nchi hizi jirani.
Infact hili suala linahitaji knowledge ya uchumi na mambo mengine.
Sio suala la utashi wa kisiasa.

Na hoja hii inanikumbusha mkataba ya madini ambayo waasisi wake walituambia kwamba shughuli za serikali ni kukusanya kodi, bila kuwa na sera ambazo hizo fedha za madini zita ifaidisha vipi nchi.
Na mazao yetu yataingiaje kwenye soko lao.
 
Soma kwanza hiyo sheria ndo uje na hayo manadharia yako ya Sukuma gang,ila nachoweza sema wewe hujui chochote kwenye haya mambo ya kazi
 
Mimi sipingi kauli
Natamani iwepo clarification..
Je wageni waajiriwe bila kujali idadi?
Au usimamizi uwepo kama enzi za JK..
Mama kwenye maelezo yake mengi anasisitiza suala la kufuata sheria! Bila shaka, alichomaanisha mama ni kuondoa ukiritimba kwenye utoaji wa hivyo vibali lakini sidhani kama anamaanisha vibali vitolewe kiholela!
 

Mkuu Upo Sahihi Mnoo sana Tuuu
Kwanza Sheria Iliopo Haifuatwi!
Makampuni Meeeengi Kama Ya Simu,Vinywaji Cement,Wana Watu weeengi zaidi ya 5
Wanawaita kwa majina Tofauti tuu,Fanya Utafiti Utaniambia!
Its only in Tz tuu
Kenye ambae ni Giant kwa Uchumi East Africa!
Yaani Kwa Mtu wa Nje kupata Kazi Pale ni Issue!
Uwe exceptional!
Hapa Tz Simple tuu wageni wengi wanapata Kazi bila Shifa yoyote hata Kama Kazi hiyo inaweza Fanywa na Mzawa!
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.
Nje ya wapi boss! Naona kama unaleta ulimbukeni vile! Dunia ni kubwa.
 
Mtu aliyewahi kuishi nje kauli ya mama ni nzuri sana ila kwa Mtanzania ambaye hajawahi kuishi nje anaweza kupingana na mama.

Muingiliano wa watu kutoka mataifa tofauti huchochea uchumi.

Wewe Umekaa na Khumbu tuu,
Sijui Kama Umewahi Kutafuta Kazi Hapa Bongo,Au Kufanya Kazi hapa Uone mambo yalivyo kuanzia Uhamiaji!
Makampuni Meeeengi Kama Ya Simu,Vinywaji Cement,Wana Watu weeengi zaidi ya 5
Wanawaita kwa majina Tofauti tuu,Fanya Utafiti Utaniambia!
Its only in Tz tuu
Kenye ambae ni Giant kwa Uchumi East Africa!
Yaani Kwa Mtu wa Nje kupata Kazi Pale ni Issue!
Uwe exceptional!
Hapa Tz Simple tuu wageni wengi wanapata Kazi bila Shifa yoyote hata Kama Kazi hiyo inaweza Fanywa na Mzawa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…