Hili la Wachaga kutoajiriwa Serikalini na Taasisi za Umma awamu ya tano, Mbowe anadanganya umma?

Hili la Wachaga kutoajiriwa Serikalini na Taasisi za Umma awamu ya tano, Mbowe anadanganya umma?

Status
Not open for further replies.
Inasikitisha kujadili mambo mazito ukiwa na taarifa hafifu. Waziri Msuya alikuwa mbunge wa Mwanga, ni mji mdogo kando ya barabara kubwa ya kutoka Dar kwenda Arusha, SIO mlimani pili swala la umeme sio jambo la kushangaa kwa eneo hili, bwawa la Mungu liko karibu na kituo kikubwa cha kuzalisha umeme Pangani. Raslimali ni nyingi Kaskazini kama ilivyo Serengeti/Usukumani- zote ni za taifa na Nyerere alituanganisha! Leo hii ni wapi utaenda umkose mchagga au msukuma. Lakini unapokuwa kiongozi na kudhihaki kabila fulani, kuonyesha chuki, ndio tatizo kubwa, na hili naamini ndilo analozungumza Mbowe. Unakumbuka yule mama aliyekuwa analalamika kudhulumiwa, Hayati alipomuuliza mdhumulaji ni nani, yule mama akasema Mushi- Hayati alihamiki vipi? Pamoja na utani lakini ilidhihirika alikuwa na issue na kina Mushi! Kwa nini tusiache haya mazungumzo hayana tija
Mungu akubariki sana mkuu Njilembera ,umeandika kwa hekima sana. Ushauri mzuri sana.
 
"Watu wengi wa Magu wa karibu hawakuwa wasukuma.
Mfano:

  • Mfugale
  • Kijazi
  • Kabudi
  • Pole pole
  • Bashiru"
Wewe Mkaruka ,hapo juu unazungumzia teuzi ama ajira!?
Mbona unaonyesha ukilaza wako hadharani!!??
Ukiwa kilaza,usipende kuongea au kuandika sana maana utajulikana na kuchekwa ewe mjane.
Mbowe anazungumzia Ajira au Teuzi ?

Na kama ni ajira anazungumzia ajira zipi ? Za UTUMISHI ?

Au hizi za mass employment kama Afya na Ualimu ?
 
Kama kasema hivyo basi chanjo ya corona ina madhara zaidi ya nilivyofikiri
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Mungu akubariki sana mkuu Njilembera ,umeandika kwa hekima sana. Ushauri mzuri sana.
Ukimchukia JPM basi pia umchukie NYERERE aliyeweka MIZANI bora juu ya maslahi mapana ya kila MTANZANIA......

Kama si kuyafanya aliyoyafanya JKN basi taifa hili lingekuwa Kama KENYA ama SUDAN KUSINI.....

#KaziIendelee
 
Mwaka 2001 Wanafunzi wa kozi ya Unesi katika chuo Kikuu kishiriki pale Muhimbili wachagga walikua 24 Kati ya wanafunzi 28.

Unategemea nn katika soko la ajira?

Mkoa wa Kilimanjaro ndio Mkoa uliokua ukiongoza kwa shule za msingi na sekondari kuanzia miaka ya 1970-2010.

Fanya hesabu.

Ilikuwa ni fahari kwa kila familia ya Mchagga kuwa na Mtoto mwenye Digree au Padri katika miaka ya 1970-2010.

Takriban vitivo vyote pale UDSM 1970-2010 vilikua na aidha mkuu wa kitengo mchagga au msaidizi wake.

*********
Tuhuma za Mwenyekiti Mbowe...

Inawezekana kutokana na facts hizo hapo juu wimbi kubwa la wachagga walifanikiwa kuingia kwenye ajira rasmi na zisizo rasmi.

Mwendazake kuzuia ajira kwa wachagga serikalini, inawezekana ukawa ni ukweli ambao hauwezi kuthibitishwa popote... Zaidi ya hisia tu kama ambavyo wenyeji wa Mkoa wa Mara waliingia kwenye majeshi ya ulinzi na usalama.

VYOVYOTE IWAVYO
Yumkini ilikua ni wakati sasa wa kulitizama Taifa katika sura tofauti na ndipo mwendazake akaoneokana kuajiri ma Homeboy zaidi. Kitendo ambacho ni sahihi kwani kwa aina ya utendaji aliokuwa akiuhitaji alikua hana budi kuchukua watu ambao watakua loyal kwake.

APPROACH YA MBOWE
Bwashee angeweza kutafuta namna nzuri ya kuliongelea hili na sio kwa namna ambavyo ameamua kuli present kwa jamii ambayo madhara yake ni kwamba;

Makabila 130+ hayawezi ku sympathize na kabila moja ambalo kimsingi sio wanyonge wala masikini.

Tamko lake linaweza kuanza kuibua hisia za makundi mengine ambayo yamesahaulika na mfumo.

Mfano;
Waislamu, Wakristo lakini KKKT, Wanawake na kundi lenye watu wenye mahitaji muhimu (walemavu, Albino na Wasioona)

MY TAKE
CHADEMA kwa sasa kinahitaji Mwenyekiti mwenye vision kubwa zaidi. Uwezo wa Mbowe kwa sasa unafikirisha sana.

Wasalaam
 
Hakuna uganga wala Uchawi juu ya nyumba ya Israeli..

Wachaga hawakipigana vita na Mwendazake, maana Mungu aliaahidi, for the battle is not yours ...

Ajaribu mwingine nae apendwe zaid....
kama usemayo yanakweli, why mungu hafanyi hivyo kwa mabeberu yanayotufanyia dhuluma, kutunyonya na kututawala kwa mabavu miaka nenda rudi?

je, hizo vita mungu hupigana dhidi ya watu weusi pekee na si weupe?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom